Ngongo
Platinum Member
- Sep 20, 2008
- 20,654
- 35,887
Heshima sana wanajamvi,
Mbunge wa Rufiji Mohamed Omary Mchengerwa amehudumu katika Wizara kadhaa za Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Katika Wizara zote alizohudumu kaacha kilio kikubwa na simanzi zisizo na kipimo kwa WATANGANYIKA wote.
Akiwa Waziri wa Utawala Bora na Utumishi alihakikisha WaZanzibar wanatengewa 21% ya ajira katika taasisi zote za muungano.Ninapo zungumzia Taasisi za Muungano ni pamoja na TRA, POSTA, BOT, BANDARI .
Fikiria TRA wametangaza nafasi za ajira 200, Zanzibar watatengewa nafasi 42 huku Tanganyika wakiambulia nafasi 158 tu. Katika nafasi hizi 158 iwapo kuna Mzanzibar yupo huku Tanganyika anaweza kuomba bila kikwazo cha aina yoyote.
Ifahamike wazi Tanganyika ina idadi ya watu million 60 huku Zanzibar ikiwa na idadi ya watu wanaokaribia million 1 tu. Waziri Mchengerwa alipokuwa akkifanya maamuzi haya ya hovyo alitumia vigezo gani? Aliamua kuwapendelea WaZanzibar kwakuwa mke wake ni MZANZIBAR!
Mchengerwa alipopelekwa Wizara ya Maliasili na Utalii kaamua kuwamilikisha WAARABU ekta million 8 za misitu bila kufikisha makataba Bungeni. Ni wazi kabisa tena pasipo shaka yoyote Mchengerwa hakustahili kurejeshwa katika baraza la mawaziri kwa kuliingiza taifa katika janga kubwa la kuuza misitu yetu kwa wageni pasipo kufuata utaratibu wa sheria za nchi.
Waziri Mchengerwa kapelekwa TAMISEMI sijui huko anakwenda kufanya kituko gani!. Labda atapigania Wazanzibar wajazwe huko ili kupata uzoefu.