Waziri Mhagama: Zaidi ya watu milioni 1.5 Tanzania wanatumia ARVs

Waziri Mhagama: Zaidi ya watu milioni 1.5 Tanzania wanatumia ARVs

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Waziri wa Afya, Jenista Mhagama amesema katika kipindi cha Julai 2024 hadi kufikia March 2025, takwimu zinaonesha Watu 1,500,212 kati ya waliopima na kutambua hali zao za maambukizi ya VVU walikuwa wameanza kutumia dawa za kufubaza VVU, sawa na asilimia 98.

Akitoa hotuba kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2025/2026 Bungeni Jijini Dodoma leo June 02,2025, Mhagama amesema "Katika kipindi cha Julai 2024 hadi kufikia March 2025, takwimu zinaonesha kuwa jumla ya Watu 1,530,227 walikuwa wanatambua hali zao za maambukizi ikiwa ni sawa na 90% ya Watu 1,700,000 wanaokadiriwa kuishi na VVU nchini (95 ya kwanza), Watu 1,500,212 kati ya waliopima na kutambua hali zao za maambukizi ya VVU walikuwa wameanza kutumia dawa za kufubaza VVU, sawa na asilimia 98"

"Aidha jumla ya vipimo 874,944 vya kujua wingi wa VVU kwa wagonjwa walioanza kutumia dawa vilifanyika, ambapo vipimo vya wagonjwa 858,272 sawa na asilimia 98 vilionesha kuwa virusi vya UKIMWI vimefubazwa (95 ya tatu)"
 
Ni ndogo sana Tanzania tupo MILION 60 sasa 1.5M sio insue sana
 
Watu milioni moja tu kati ya milioni 60, mbona ni wachache. Ni asilimia sifuri nukta ngapi hiyo?
Hata mimi huwa nashangaa! Nahisi ukipata UKIMWI una mkosi sana aisee! Tangu nianze kupima na wapenzi, sijawahi kumkuta mwenye ngoma mpaka huwa najiuliza wapo wapi!
 
Transfoma hizo mamaé gusa uungwe grid ya taifa uwe marehemu mtarajiwa
 
Acheni kula Tunda kimasihara.
Siku 90 za D.Trump zimeisha, ngoja tusiburi atakuja na solutions gani?
 
Hata mimi huwa nashangaa! Nahisi ukipata UKIMWI una mkosi sana aisee! Tangu nianze kupima na wapenzi, sijawahi kumkuta mwenye ngoma mpaka huwa najiuliza wapo wapi!
Ndiyo hiyo, mkuu hapo juu amepiga hesabu, ni asilimia 2.5

Watu asilimia 2 ni wachache.

Kupata HIV inatokea kwa bahati mbaya sana.

Umkute yule ameathirika kabisa ameliwa fangasi ana vidonda, na wewe uwe na kaupele juu ya uume kachubuke.
 
Ogoopaa,duh! Ngoja nituliee.Ila Pisi nazoo zinawakaaa🤣🤣 .Niwekeze kwenye msosiii nakusaka Pesa.
 
Hiyo takwimu ni ndogo sana tena sana,nadhani wanapaswa kusema ukweli ili kondomu zipate wateja. Kwatakwimu hii watu hawataogopa,waache siasa kwenye ngoma.
 
Ndiyo hiyo, mkuu hapo juu amepiga hesabu, ni asilimia 2.5

Watu asilimia 2 ni wachache.

Kupata HIV inatokea kwa bahati mbaya sana.

Umkute yule ameathirika kabisa ameliwa fangasi ana vidonda, na wewe uwe na kaupele juu ya uume kachubuke.
Wacha we
 
Back
Top Bottom