Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Tofautisha kuwa na akili nankuwa na uwezo mkubwa wa kukalili kiti ambacho kitatumia portion ndogo sana katika ubongo ambapo kuna ndio maana ukiondo hayo aliyo yakariri darasani anabaki na kichwa cheupe
 
Yeye mwenyewe Mkenda alipitia mkondo huo huo pale UDSM..
Alihitimu B.A (Economics) akachukuliwa kuwa TA kwenye faculty tofauti, B.Com (Finance), waliokuwa wamefaulu eneo husika wakaachwa!!!
 
Nchi nyingi nafasi huwa zinatangazwa na applicants wanamfanyia usaili. Huyo mwenye first class kama ni fit kwenye kazi basi ataonyesha uwezo wake kwenye usaili.

Tatizo la Tanzania nafasi za lecturers zinatangazwa ni za juniors. Nadra kusikia nafasi ya Senior Lecturer au Professor inatangazwa.

Nchi nyingi hata nafasi ya Vice Chancellor inatangazwa na kufanyiwa usaili. Siyo kama Bongo watu wanapewa tu politically.
 
Kwani lina tatizo gani hili tangazo?
Lugha iliyotumika hapo inaonesha jinsi ambavyo elimu yetu ilivyo duni na watu tuliowaajiri vyuoni hawana sifa stahiki. Pili nashangaa sana kwa mbunge mzima kufanya masters (wao wameandika "Master"!) nyepesi ya kizushi namna hiyo! Tena mtoto wa rais?!!! Hiyo ilipaswa kuwa research work ya final year undergraduate kwa ajili ya B.A. na sio kwa ajili ya M.A. Loh!
 
Msisahau kutazama na hili:

 
Hapo Onyang'inyang Chikungunya itakuwa ilimkatalia kabisa hapo laazima! πŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 

Mkuu, hii mentality imeanzia sehemu inayoaminisha kuwa uongozi ni kipaji na ufahamu hauna athari katika uongozi. Wakataka dereva wa mkuu wa wilaya awe na kiwango cha chini cha elimu (form four) lakini mbunge awe anajua kusoma na kuandika tu (na hitaji hilo linaweza kufikiwa hata na mtu aliyefanya home schooling na kufika darasa la nne tu). Unamfanyaje mtunga sheria kuwa hana uwezo wa hata kusoma na kuelewa muswada lakini ajadili na kupiga kura wa kuipitisha!!??

Tumekuwa na tabia ya kubeza ufaulu na ufahamu na kudogosha matokeo mabaya kwa kuyaita division five nk. Wengine wamefikia kupunguza wigo wa A mpaka kuifikisha 75/100 kutoka 81/100.

Inasikitisha sana.
 
You are WRONG TOTALLY.! PIMBI!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…