Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Waziri Mkenda: Ajira ya Chuo Kikuu isiwe kuangalia GPA pekee lazima wapimwe, wafanye na usaili

Ni KWELI kiasi Fulani unakuta MTU GPA ya KAWAIDA ana uzoefu wa kazi mtu GPA KUBWA yakukariri class lakini KWENYE area of production hamna kitu ila MWISHO WA siku ajira nikujuana tu we kaa pale halafu Kuna mtu ana Ma experience yake tupa kule
 
ukiondoa rushwa GPA ni kipimo kizuri Cha competency ya mwanafunzi ..hasa vyuo vinavyotumia mfumo CBET (competency based education & training) .....
 
Kweli nchi inaenda kubaya sana. Kwa hiyo wakifanyiwa usaili ndio elimu inakua bora. [emoji3][emoji3][emoji3][emoji3][emoji3].
Mtu mwenye GPA kubwa kwa vyuo kama SUA, MZUMBE na UDSM huyo anauwezo mkubwa, haina haja ya kujiuliza mara mbili.

Nenda uendako, kwenye usaili watu wanakalili na kufaulu baada ya hapo wanasahau. Ila mwenye GPA kubwa ni mtu mwenye uwezo.

Haiwezekani mtu kidato cha Nne abamize one ya saba, kidato cha sita one ya nne na chuo GPA ya 4.6. Useme hana uwezo badala yake utegemee kumpima kwenye usaili Ili kupima uwezo wake.

Tuwekeze kwenye practical zaidi
Sasa hapo tatizo liko wapi? Una GPA yako kubwa unakataa nini kufanyiwa usaili kujua upande mwingine ukiachilia mbali hayo katokeo yako ya darasani.
Ikumbukwe hawajasema wanaondoa GPA, ila kuna vipaji vya kufundisha tofauti na matokeo uliyonayo na kwa wale waliosoma wanajua kasumba ya GPA.
 
Jee pia ni kipimo cha mtu kuwa mhadhiri bora??
Ndio ,,Kwa mfumo wa CBET huwezi pata GPA nzuri kama practical module umevurunda .... tatizo la vyuo vyetu ni rushwa ya ngono ,pesa ,au kubebana ..
Ukiona mtu ana GPA ya 3.5 kwenye vyuo vya CBET mheshimu sana
 
Ni habari njema na hatua nzuri...
Ingawa ufaulu unatakiwa kuwa kigezo cha kwanza then uwezo wa mtu uwe kigezo kinachofuata..........
 
Tatizo la mkenda huwa anajiona yeye anaakili sana
Hata hivo ana akili mkuu... mtu uwe profesa na undergraduate ulitoka na First class halafu useme eti hana akili?

Haumtendei haki...

Ki chuo chuo mtu akikupita GPA amekuzidi kwenye shule.. achana na mambo ya kutafuta hela.

Utashangaa hata kwenye ma group ya chuo ya whatsapp. wenye gpa ndogo always wanatoaga pumba points nyingi sana.. ata kwenye kudiscuss mambo ya kawaida
 
Naona kama vile wengi mnachanganya. Chuo Kikuu ni mahali pa academicians ambao kazi yao kubwa ni kukupa nyenzo za kuweza kufikiria mwenyewe. Chuo Kikuu kinakupa knowledge na sio ufundi. Tatizo la vyuo vyetu ( na shule zetu) ni kuwa zinakazania kukariri badala ya kuwafundisha wanafunzi udadisi. Chuo Kikuu hakiwezi kumfundisha mwanafunzi namna ya kukabiliana na kila hali atakyoikuta lakini akizitumia nyenzo alizofundishwa anaweza kukabiliana na hali tofauti atakazo zikuta uraiani. Na pale ambapo atashindwa ataomba msaada kwa sababu amefunzwa kutambua udhaifu wake. Mafundi mchundo mara nyingi tunakuwa na ujuzi mkubwa wa utendaji kazi kuliko wahandisi wapya lakini kwa wale wenye uelewa haichukuwi muda kutuzidi maana sisi tunafanya kwa mazoea lakini yeye ana uwezo wa kudadisi na kujua kwa nini tunapata matokeo tunayopata.

Kwa sababu hiyo, tusiwabeze wahitimu wa chuo kikuu kwa sababu kuna vitu hawavielewi. Tuwape muda na ushirikiano na wote tutafaidika.

Amandla...
 
Waziri anachosema ni ujinga mtupu

Mfano huajiri mtu kwa GPA unaajiri Tutorial Assistant umempata mmoja mzuri sana kwenye presentation lakini ana GpA ya chini sana ambayo haimuwezeshi hata kujiunga kwenda kusoma Masters degree sababu hakidhi vigezo anataka huyo aje kufia rank ya tutorial assistant atapandaje juu kuwa mhadhiri bila kuwa na Masters ?

OK fine anachukua hata mwenye Masters pass za chini sana kuwa mhadhiri PhD akitaka kusoma ataendaje wakati pass hana za kutosheleza?

Tatu GPA kubwa maana yake nini ni kuwa mwanafunxi hadi anamaliza degree aweza.kuwa kasoma mathalani masomo 30.ambayo yote kafundishwa na wahadhiri tofauti tofauti na kote akapasua masomo yao yote kwa ufaulu mkubwa kila somo.la kila mmoja kwa miaka yote.Maana yake yuko bright kila eneo sio evarage.Sasa kufundisha anatakiwa mtu bright

Anachofanya waziri ni kuua elimu ya vyuo vikuu kama walivyoua primary kuwa mtu kusomea ualimu anapelekwa amiyefeli aliyepata division three na four ndio anapelekwa chuo cha ualimu akasomee kufundisha shule za msingi

Matokeo yake wanazalishwa watoto hawajui kusoma wala kuandika.Primary watu wameshauri kuwa ualimu wakasomee division one na two kama njia ya kuongeza uwezo wa kufundisha shule serikali haisiki
Sasa wameozesha elimu ya msingi wanataka kupeleka wahadhiri wa UPE low class wakafundishe chuo kikuu
Hata kama ni sjira wanawatafutia watoto wao wenye GPA ndogo waone aibu wakawatafutie kwingine sio uhadhiri vyuo vikuu
 
mjadala sasa umenoga... Asante sana Fundi Mchundo maana unaandika mantiki sana kwenye kona mbali mbali za mjadala huu.

Ni kweli kwamba Chuo kikuu hufundishwa ni kwa nini matokeo fulani yanatokea wakati vyuo vingine wanafundishwa kufanya kitu ili kitokee kitu kingine. Lakini hoja yenyewe ni kweli hali iko ivo??

Maana kama Profesa aliyehudumu chuo Kikuu baada ya kupata alama za juu sana chuoni hapo akiwa mwanafunzi, (kwa maelezo ya Naantombe Mushi, )anaona kuna upungufu kwenye kusaili wahadhiri vyuoni, hiyo nadharia ya vyuo vikuu kutoa watu hao wenye kujua ni kwa nini matokeo fulani hutokea, inafikiwa kweli??
 
Waziri anachosema ni ujinga mtupu

Mfano huajiri mtu kwa GPA unaajiri Tutorial Assistant umempata mmoja mzuri sana kwenye presentation lakini ana GpA ya chini sana ambayo haimuwezeshi hata kujiunga kwenda kusoma Masters degree sababu hakidhi vigezo anataka huyo aje kufia rank ya tutorial assistant atapandaje juu kuwa mhadhiri bila kuwa na Masters ?
Umejipotosha bwana Mzee. Waziri hajasema wenye GPA ndogo watachukuliwa. Kasema hao hao wenye GPA kubwa watasailiwa kwa kina kwanza kabla ya kupewa kazi ya kuwa waadhiri ama wakufunzi wasaidizi. Tatizo liko wapi??
 
mjadala sasa umenoga... Asante sana Fundi Mchundo maana unaandika mantiki sana kwenye kona mbali mbali za mjadala huu.

Ni kweli kwamba Chuo kikuu hufundishwa ni kwa nini matokeo fulani yanatokea wakati vyuo vingine wanafundishwa kufanya kitu ili kitokee kitu kingine. Lakini hoja yenyewe ni kweli hali iko ivo??

Maana kama Profesa aliyehudumu chuo Kikuu baada ya kupata alama za juu sana chuoni hapo akiwa mwanafunzi, (kwa maelezo ya Naantombe Mushi, )anaona kuna upungufu kwenye kusaili wahadhiri vyuoni, hiyo nadharia ya vyuo vikuu kutoa watu hao wenye kujua ni kwa nini matokeo fulani hutokea, inafikiwa kweli??
Kwanza kabisa u Profesa ni ualimu. Pili, hawa jamaa wakiingia kwenye siasa kwa kiasi fulani wanapoteza dira zao. Kama academician alitakiwa ajiulize kwa undani kiini cha matatizo anayozungumzia. Kwa kukimbilia kwenye usaili ni kutafuta majawabu mepesi kwa maswali magumu, kitu ambacho wanasiasa wanafanya. Kwa mtazamo wangu tatizo sio walimu wapya bali ni wale waliopo ( pamoja na yeye) na tamaduni za ufundishaji katika vyuo vyetu. Mtu akiwa Profesa au akiwa na Ph.D anaona amemaliza na anajua kila kitu. Hataki kuwa challenged na vijana anaowafundisha akisahau kuwa mazingira wanayokulia ni tofauti kabisa na ambayo wao walikulia.

U profesa kwa wengi wao ni daraja la kufikia tamati ya safari yake. Wakati kwa wenzetu, uprofesa ni nafasi adimu ya kujifunza kila siku maana unazungukwa na vichwa vinavyokufanya ujitume zaidi katika kufikiria. Ndio maana Profesa Biden amekataa kuacha kufundisha hata baada ya kuwa First Lady kwa sababu hataki kuacha changamoto za ualimu. Ndio maana ma Profesa walioingia kwenye taaluma nyingine kama siasa au ujaji kila mara wanarudi vyuoni kuwa challenged na wanafunzi wao. Ni wangapi katika hawa maprofesa wetu wanafanya hivyo?

Haya majibu mepesi wanayotupa yatatufurahisha lakini hayatatupa permanent solution. Tukitaka permanent solution inatubidi tuangalie bila kupepesa macho dhana nzima ya elimu yetu. Kwa ujumla hatuheshimu elimu ndio maana hatuoni taabu kukatiza masomo ya wanafunzi wetu ili tuwapeleke kwenda kusikiliza hotuba za wanasiasa. Safari bado ni ndefu sana.

Amandla...
 
GPA itaendela kuwa kigezo cha kuita watu kwenye usaili na kuajirii Hilo halipingiki ....

Siwezi kuita mjinga mwenye gpa ya 2.0 wakati mezani nina CV ya watu wenye gpa za 4.0 and above et Kwa kujipa Moyo anaweza kuwa na akili ...

Kama ameshindwa kuwa na kumbukumbu za alichokuwa anafundishwa shuleni na kujibu mtihani na kufaulu ataweza nin kazin ..


Harafu fuatili watu wengi wenye gpa za 2.0 ni weupe vichwani kama ilivyo kwenye karatasi ,gpa ya chuo ,matokeo ya form six ,matokeo ya form four havijawahi kudanganya [emoji3][emoji3][emoji3]...

Nioneshe vyetu vyako vyote hivyo nikuambie uwezo wako wa kufikili na kuchambua Mambo ....
Nenda katafte historia ya Gregor Mendel father of genetics.. sio tuu gpa mwamba alifeli na kufeli lkn leo mchango wake unatambulika worldwide
 
Ninachokueleza ni kwamba graduates, matokeo yao ya makaratasi hayafanani na kilichomo kichwani, Nawapokea sana, nawapa nafasi sana, field wanaziomba sana, kujitolea na ajira wanaomba hivyo nakutana nao mara nyingi tu na wakati mwingine yule ambaye kwenye makaratasi wala haonekani mwenye elimu kubwa na diploma ya vyuo visivyo rasmi anafanya vizuri tu kuzidi vijana wa IAA, Mzumbe, UD, UDOM SAUT n.k.

Mfano wa swali jepesi katika field ya biashara ambalo mwanachuo yoyote esp mwenye GPA kubwa hakupaswa kushindwa kulijibu: Ni nyaraka zipi zinatumika kufanya miamala baina ya raia wawili walio nchi tofauti wakati wanafanya biashara?

Hii ni international trade, Mtu ana BBA na GPA fiirst class lakini anajibu mpaka unaona huruma, wakati mwingine unadhani ni panic unamwambia relax, kunywa maji unampigisha hadithi nyingine ili asiumie kisha ukishaona karudi normal unaruhusu panel iendelee ila still wengi wanashindwa na hapo swali limeulizwa kwa kiswahili.

BOSS NAKUELEZA, TUNA TATIZO LINALOPASWA KUFANYIWA KAZI. TUNAPOELEKEA IKITOKEA PAKAWA NA UHURU WA KUAJIRI BAINA YA EA VIJANA WETU WATAUMIA SANA.
Wameruhusu kuichezeq elimu ya o level na a level kwa kigezo cha kuongeza ufaulu.. leo hii mtihan wa kidato cha nne watoto wanafaulu tuu.. kuna mjomba wang kapiga form 4 one ya 10 mwaka jana ila ukikaa nae ukimpa maswali tuu ya kawaida hola, plus kumfundisha tuu mdogo wake changamoto shule ndogo.. unategemea dogo km huyo akifka chuo atakuaje??

Tumerahisisha sn elimu yetu
 
Serikali irud kwenye basics elimu ya msingi la kwanza mpk la saba iambatanishwe pmj na ufundi,sanaa na stadi za kilimo..

Mchujo uwepo wa uhakika wanaofaulu hata kama ni wawili nchi nzma waende sekondari, wanaofeli wakajiendeleze na hzo fani zingne

Nchi haiwez kujengwa na madaktari,mainjinia na wanasheria tunaitaji pia maseremala,makuli,wasanii, wanamichezo n.k

Huku kubebana bebana ili kila mtu awe na cheti cha form 4 au degree tualiangamiza taifa
 
shida ya hii nchi uhuni mwingi , ivyo ivyo wanavyotaka wao bado kuna wahuni watawapitisha wasiostahili
Upo sahihi sana Jombaa. Huyo huyo Mkenda akiwa mwalimu na mkuu wa idara ya uchumi chuo kikuu cha Dar es Salaam walikuwa wanalazima aajiriwe mwanamke kisa idara ilikuwa na wanawake wawili tu mke wake na aliyekuwa naibu gavana wa benki kuu kipindi hicho. Maanake hapo una-risk kuweka mtu hata mwenye uwezo mdogo kwa ubaguzi wa kijinsia.
 
Unajiliwaza tu mkuu. Kigezo ndio hicho. Minimum GPA ni 3.8. Hapo ndio unqualify walau kuwa shortlisted kwa ajili ya interview. Na hizo ni guidelines za TCU. Hata kama unahisi una uwezo wa kufundisha, maadam hujakidhi hicho kigezo kimojawapo, sahau kuitwa kwny interview. Halafu tuache excuses za kufeli kwetu kwa kubeza waliofaulu kutuzidi. Mnatumia kigezo gani kuwa mwenye GPA kubwa kafake na mwenye GPA ndogo ni genuine? Nani aliyeingiza hii mentality kwa jamii?
Kiukweli nakuunga mkono, wacha iendelee hivyo hivyo! Pengine hii mentality imeenea kutokana na ushenzi unaoendelea vyuoni.

Unakuta vyuo binafsi haviko serious kwenye suala la GPA, kwakuwa muamuzi wa GPA ni mwalimu mwenyewe yaani personal ndipo tatizo linaanzia.

Kama pangekuwepo na mtihani wa aina moja nchi nzima na uko chini ya usimamizi mmoja nankusahihishwa na usimamizi husika ingeleta mantiki...mfano tunaona kwa NECTA.

Ushawahi kujiuliza kama form four au six wangekuwa na mamlaka walimu binafsi kujipangia matokeo kuna shule wanafunzi wangekuwa wanapata 100 wote na kwa masomo yote?
 
Wameruhusu kuichezeq elimu ya o level na a level kwa kigezo cha kuongeza ufaulu.. leo hii mtihan wa kidato cha nne watoto wanafaulu tuu.. kuna mjomba wang kapiga form 4 one ya 10 mwaka jana ila ukikaa nae ukimpa maswali tuu ya kawaida hola, plus kumfundisha tuu mdogo wake changamoto shule ndogo.. unategemea dogo km huyo akifka chuo atakuaje??

Tumerahisisha sn elimu yetu
Daaa. Tuna tatizo sana mkuu.
 
Back
Top Bottom