Waziri Mkenda hawa walimu walikosea nini hadi wapewe hii adhabu ya kuporwa madawati ya kukalia?

Waziri Mkenda hawa walimu walikosea nini hadi wapewe hii adhabu ya kuporwa madawati ya kukalia?

tapatalk_1706177375150.jpg
 
Inaingizwa kwenye AC ya shule, Mwalimu mkuu, mhasibu na mwenyekiti wa kamati ya shule ndio wanaweza kuiaccess....
Matumizi yanapitishwa na kamati ya shule na vikao vya walimu.
Sasa hapa, unadhani kweli walimu hawakuripoti ugumu wanaopitia? Hio kamati,haijui! Sema tu pesa za serikali zilishapigwa mnada,kila kona ikifika watu wana chao,walimu labda ukute siku moja wanatengewa chai na mandazi,hafu ripoti inaandikwa wametumia milioni 10 kuwasaidia chai walimu.
Binafsi naona hao walimu wa kawaida hawana kosa lolote,wamedhalilishwa na uongozi wao.
Ila kama alivyosema mtu mmoja kapa,maboss kama ni wengi,hawajui wamlilie nani.
Wangemuandikia barua Waziri mkuu Kassim tuone kama pesa zilizoliwa hazijarudishwa na meza na viti wakanunuliwa.
 
Mapoyoyo hai walimu. Wanashindwa kuwatafutia madawati wanafunzi qanajitafutia wao?

Hao wangechapwa na fimbo juu.

Hao ndiyo walimu wanaofundisha wanafunzi ujinga.

Kwa hivyo ni kazi ya mwalimu kutafuta madawati?. Acheni kiwaangushia waalimu mizigo isiyokuwa yao. Mnachanga bilioni tatu AFCON halafu madawati atafute mwalimu.
 
Sasa hapa, unadhani kweli walimu hawakuripoti ugumu wanaopitia? Hio kamati,haijui! Sema tu pesa za serikali zilishapigwa mnada,kila kona ikifika watu wana chao,walimu labda ukute siku moja wanatengewa chai na mandazi,hafu ripoti inaandikwa wametumia milioni 10 kuwasaidia chai walimu.
Binafsi naona hao walimu wa kawaida hawana kosa lolote,wamedhalilishwa na uongozi wao.
Ila kama alivyosema mtu mmoja kapa,maboss kama ni wengi,hawajui wamlilie nani.
Wangemuandikia barua Waziri mkuu Kassim tuone kama pesa zilizoliwa hazijarudishwa na meza na viti wakanunuliwa.
Hamna wa kumlalamikia, pesa ukute imeliwa na Mwalimu mkuu Kwa kushirikiana na maafisa wilayani.....huwa wanaimpose vimichango vya ajabu ajabu kutoka kwenye hiyo capitation.

Ukiona mwenyekiti wa kamati ya shule kahusika kupora madawati ujue anajua kuna mvujo wa pesa na hajapewa mgao.
 
Ila hii Nchi hatujaliani sana ...

Yaani wote ni Watumishi wa Serikali, Tena unaweza Kuta mmesoma wote Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ila mmoja Mwalimu mwingine ni Mwanasheria.

Mmoja anaajiriwa Wizara ya Fedha kama Mwanasheria ila mwingine anaajiriwa kuwa Mwalimu.

Huyu mwingine anakuta ofisini kwake Kuna Meza na Kiti kizuri cha Kuzunguka pamoja na Chai ya Ofisini

Huyu Mwingine anaingia Darasani ambapo hakuna Kiti Wala Meza

It's unfair Wakuu

Hebu Viongozi waangalie hili suala
 
View attachment 2882428

My Take
Sitaki kuzungumzia uhaba wa samani kwa sababu ni jambo linalojulikana.

Najiuliza Ilikuwaje walimu wakakubali na kuruhusu kunyang'anywa madawati? Mbona walimu inakuwa kada ya kinyonge sana? Nini kinafanya muwe na unyonge wa kijinga
Tatizo la walimu wetu hapa nchini walisha ambiwa kuwa mtaaani Kuna walimu wengi kwamba ukidai haki zako unaweza poteza kazi,na walimu wetu walio wengi wanaamini kuwa hawawezi ishi bila kazi ya ualimu, sasa unakuta walimu wengi wanadhalilishwa , Kila mtu anajidai boss anatoa maagizo ambayo hayana miguu Kwa mwalimu wa Tanzania,na wenyewe wako kama mazombi tu Kila kitu kwao ni YES papaaa[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].
 
Na muda mwingine walimu nao wanazingua, kila mwezi shule zinapelekewa capitation, kuna fungu la ukarabati na fungu la manunuzi ya vifaa....wangeweza kutengeneza samani za ofisi ya walimu.....Ila ukute Mwalimu mkuu kageuza hayo mafungu posho yake binafsi.

Hii Kada acha idharauliwe, kuna watu wabinafsi na wenye roho mbaya wamejazana humo
Nakazia,na wachawi wamejazana kwenye hii kada ya ualimu
 
View attachment 2882428

My Take
Sitaki kuzungumzia uhaba wa samani kwa sababu ni jambo linalojulikana.

Najiuliza Ilikuwaje walimu wakakubali na kuruhusu kunyang'anywa madawati? Mbona walimu inakuwa kada ya kinyonge sana? Nini kinafanya muwe na unyonge wa kijinga
Habari ya upande mmoja hii itawachanganya sana katika kutoa maoni!

Mleta mada hajaeleza nini kilisababisha kunyang'anywa viti na meza walizokuwa wakitumia na wakaridhika.

Waweza kuta walikula hela ya kununulia samani za shule na hapo wamewajibishwa.

Kusikiliza maneno ya upande mmoja huleta taharuki sana.

Niliwahi shuhudia ofisini mtu mzima akilambwa mboko za nguvu na akanyanyuka hapo na kushukuru huku akisema "ahsante mkuu"!

Ilikuwa hivi: kazini kwetu kosa la "utoro" linachukuliwa kwa uzito mkubwa sana.

Utoro wa siku3 usijulikane ulipo, adhabu ya chini ni kunyang'anywa cheo na adhabu ya juu ni kifungo ama kufukuzwa kazi kwa aibu.

Jamaa alihuni kazi zaidi ya miezi6 asijulikane alipo, yalipomshinda maisha alikokwenda, akaamua kurudi ili liwalo na liwe.

Alivorejea, akakutana na kiongozi mbabe.

Katika kuhojiwa akawa anakiri na kuomba msamaha.

Huyo kiongozi akasema hapana, jambo kubwa kama hilo haliwezi likaisha kwa "samahani", akampatia option achague, amshitaki ili akumbane na lango la jela au amrarue mboko, tena zile hamsa ishirini ili wayamalize😀😀!

Jamaa akachagua mboko ili yaishe.

Lambwa mboko sana humo ofisini jamaa kugaragara vibaya na hadi chozi la mtu mzima juu, yakaisha kwa njia hiyo.

Sasa kama mtu siku hiyo alichungulia dirishani na kuangalia huo udhalilishaji bila kusikiliza maelezo ya pande zote, lazima angelimtetea huyo mtoro, wakati huo kumbe mboko hizo zilikuwa ni za ridhaa ili kulinda utu na heshima ya mpigwaji.

Sasa na hao walimu usikute picha imechukuliwa wakati wa muwambo, wakisubiri mishahara itoke ili kwenda kununua madawati yaliyostahili kununuliwa zamani, wao wakazilamba fedha hizo.

Haiwezekani mwalimu akakalishwa chini mavumbini bila sababu na akaridhika, wakati jukumu la kununua samani za shule na vitendea kazi si la walimu ni jukumu la ofisi.
 
Back
Top Bottom