Habari ya upande mmoja hii itawachanganya sana katika kutoa maoni!
Mleta mada hajaeleza nini kilisababisha kunyang'anywa viti na meza walizokuwa wakitumia na wakaridhika.
Waweza kuta walikula hela ya kununulia samani za shule na hapo wamewajibishwa.
Kusikiliza maneno ya upande mmoja huleta taharuki sana.
Niliwahi shuhudia ofisini mtu mzima akilambwa mboko za nguvu na akanyanyuka hapo na kushukuru huku akisema "ahsante mkuu"!
Ilikuwa hivi: kazini kwetu kosa la "utoro" linachukuliwa kwa uzito mkubwa sana.
Utoro wa siku3 usijulikane ulipo, adhabu ya chini ni kunyang'anywa cheo na adhabu ya juu ni kifungo ama kufukuzwa kazi kwa aibu.
Jamaa alihuni kazi zaidi ya miezi6 asijulikane alipo, yalipomshinda maisha alikokwenda, akaamua kurudi ili liwalo na liwe.
Alivorejea, akakutana na kiongozi mbabe.
Katika kuhojiwa akawa anakiri na kuomba msamaha.
Huyo kiongozi akasema hapana, jambo kubwa kama hilo haliwezi likaisha kwa "samahani", akampatia option achague, amshitaki ili akumbane na lango la jela au amrarue mboko, tena zile hamsa ishirini ili wayamalize😀😀!
Jamaa akachagua mboko ili yaishe.
Lambwa mboko sana humo ofisini jamaa kugaragara vibaya na hadi chozi la mtu mzima juu, yakaisha kwa njia hiyo.
Sasa kama mtu siku hiyo alichungulia dirishani na kuangalia huo udhalilishaji bila kusikiliza maelezo ya pande zote, lazima angelimtetea huyo mtoro, wakati huo kumbe mboko hizo zilikuwa ni za ridhaa ili kulinda utu na heshima ya mpigwaji.
Sasa na hao walimu usikute picha imechukuliwa wakati wa muwambo, wakisubiri mishahara itoke ili kwenda kununua madawati yaliyostahili kununuliwa zamani, wao wakazilamba fedha hizo.
Haiwezekani mwalimu akakalishwa chini mavumbini bila sababu na akaridhika, wakati jukumu la kununua samani za shule na vitendea kazi si la walimu ni jukumu la ofisi.