Leo limetokea tukio la kustaajaabisha sana hapa katika shule ya msingi Tumaini iliyopo manispaa ya Bukoba, watoto wamerudishwa majumbani kwa kuwa wazazi hawajalipa mchango wa Tuition ya jioni.
Kinachoumiza ni kumrudisha mtoto asubuhi nyumbani, yaani akose vipindi vya msingi vya asubuhi kisa pesa ya tuition jion. Kwanini wasiwarudishe jioni kwenye darasa husika? Je, michango imeshakuwa lazima kinyumenyume?
Najua wanabodi wengine watanitukana nikalipe, mimi watoto wangu hawasomi hapo ila nimeumia kuona watoto wa wengine wakifanyiwa haya.
Ukweli ni kwamba elimu ni gharama, wanaotwambia tusilipe michango wala ada, ili watoto wetu wainjoi elimu, wao wanalipa mamilioni kwa ajili ya watoto wao, mf.Mwigulu, watoto wake wapo Feza huko analipia mamilioni, lakini utamkuta mishipa imemtoka akiihubiri elimu bure!
Nilienda shule moja huko mkoani Songwe,wilaya ya Mbozi, inaitwa Mlangali secondary school (anasoma mtoto wa shangazi yangu),waliagizwa kupeleka Ream papers kwa ajili ya mitihani, shangazi alilalamika kwanini wtnatozwa mchango wa Ream wakati serikali imesema wasitoe mchango!
Nilipofika shule kupeleka hiyo Ream nikapata wasaa wa kuongea na makamu Mkuu wa shule, kwamba shule ina mikakati ya kuwafanyisha mitihani ya kutosha wanafunzi wao ili kuwaandaa na mitihani ya taifa, na ili hilo lifanikiwe, waliwaomba wazazi kupeleka ream shule kwa sababu shule haina pesa...na pia wazazi wakaombwa kuchangia sh.1000 kila J.mosi ili kutoa copy hiyo mitihani, kulipa pesa ya maji kwa walimu kujitolea kufanya kazi J.mosi (kwani wangeweza kukaa nyumbani wapumzike) lakini wazazi HAWATAKI, kwa kuwa waliambiwa elimu ni BURE!
Niliiona nia njema ya walimu wa hiyo shule ya sekondari Mlangali, lakini jamii inayowazunguka inajijengea uzio mzito kuelekea mafanikio ya watoto wao kielimu, sasa hata kama hali ni ngumu, kweli kutoa sh. 1000 kwa wiki kumsaidia mtoto wako kielimu unaona shida????
Halafu ukiambiwa wachagga wamejazana maofisini mnakimbilia kusema ni ukabila? Mleta mada, nafikiri kabla hatujawalaumu walimu, tuanze na wazazi kwanza, kwanini hawatoi michango midogo midogo hiyo kusaidia elimu za watoto wao?
Sisi tulisoma private na bado unakutana na mchango wa "kuboresha elimu laki tatu (300,000) inalipwa, Mara pesa ya jengo 200,000, inalipwa na hizo zote zinakuwa nje ya ADA!
WATANZANIA TUKIENDELEA KUPUUZA ELIMU, NA KUIONA NI KITU CHEPESI NAMNA HII HAKIKA TUTAENDELEA KUKANDAMIZWA KWA MIAKA MINGI SANA IJAYO!