Waziri Mkenda, nakushauri ufumue mfumo wa elimu kuanzia Awali, Msingi, Sekondari ndipo uanze mambo ya ajira za GPA

peno hasegawa

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2016
Posts
14,255
Reaction score
23,949
Waziri mkenda, ninaomba nikupe ushauri wa bure kabisa kuhusu elimu.

Kwa sasa mambo ya ajira za GPA uko sawa ila anza kufumua mfumu, muundo na mitaala ya elimu nchini.

Prof, hakikisha kila shule ya msingi ina madarasa 2 ya awali na walimu wa awali wenye uwezo wa kufundisha wanafunzi kwa lugha ya Kiingireza.

Elimu kuanzia awali iwe kwa lugha ya kiingireza hadi chuo kikuu na kiswahili kiwe ni somo tu kama masomo mengine.

Somo la kiswahili na hesabu liwe compulsory kuanzia awali hadi chuo kikuu.

Awali mtoto asome miaka miwili tu na msingi mtoto asome miaka 6 na awali mtoto aanze akiwa na umri wa miaka 2-4 tayari kwa kuanza elimu ya msingi ya kuishia darasa la sita.

Mtihani wa la saba ufutwe ili mtoto akimaliza la sita walifanya vizuri kwa matendo na kwa masomo waingie kidato cha kwanza hadi cha nne wasio na uwezo kuanza kidato cha kwanza waingie vicational training school.

Walimu wote wajifunze kufundisha kwa lugha ya kiingireza na wapatikane walimu wa vocstional training soon.

Vyuo vikuu kuna kozi za kufutwa na kuondolewa kwenye mfumo na suala la kusahihisha mitihani ya university isahihishwe kwa Panel sio mtu anajificha na mitihani ya akina dada akisahihishaili akamvue nguo ampatie marks nzuri kiandaa GPA.

Sasa baada ya hapo anza kuongelea ajira kupitia GPA au la.
 
Ipitishwe sheria mitihani vyuo vyote nchini kuanzia ngazi ya cheti hadi Phd mitihani isahihishwe kwa PANEL.
Ni kweli tumeshuhudia watu kibao wamegraduate lakini uelewa wao wa mambo uko chini kuliko mtoto wa form iv aliyesoma shule za magari ya njano .Mpaka unajiuliza huko vyuoni wanaenda kusomea ujinga
 
Prof, hakikisha kila shule ya msingi ina madarasa 2 ya awali na walimu wa awali wenye uwezo wa kufundisha wanafunzi kwa lugha ya Kiingireza.
Ushauri wa hovyo kwa waziri wa elimu kuwahi kutolewa ktk jukwaa hili.

Nilipoona kichwa cha uzi wako nikadhani kuna cha maana Sana ulichotuletea. Kumbe kwako wewe maborsho ya elimu ni kufundiaha kwa lugha ya kiingereza!!!?
 
Labda tuue kizazi chote.

Serikali ilikosea kuchukua waliofeli kuwasomesha Ualimu.
Unamchuku mtu aliyefeli, afu unampa kazi ya kufundisha wasiojielewa ili wajielewe
 
Waziri mkenda, ninaomba nikupe ushauri wa bure kabisa kuhusu elimu.

Kwa sasa mambo ya ajira za GPA uko sawa ila anza kufumua mfumu, muundo na mitaala ya elimu nchin...
Umesema kweli na vyema kabisa.
 
Labda tuue kizazi chote.

Serikali ilikosea kuchukua waliofeli kuwasomesha Ualimu.
Unamchuku mtu aliyefeli, afu unampa kazi ya kufundisha wasiojielewa ili wajielewe
Hivi kwenye ualimu wanachukuliwa waliopata 0 ee?!!!
 
Ushauri wa hovyo kwa waziri wa elimu kuwahi kutolewa ktk jukwaa hili.

Nilipoona kichwa cha uzi wako nikadhani kuna cha maana Sana ulichotuletea. Kumbe kwako wewe maborsho ya elimu ni kufundiaha kwa lugha ya kiingereza!!!?
Mtoto anasoma masomo karibia yote kwa kiswahilu kwa miaka 7 , ghafla kidato cha kwanza hadi chuo kikuu. Masomo yote anafundishwa kwa kiingireza? Huoni kuna tatizo hapo?

Ni bora masono yote yafundishwe kwa kiswahili kuanzia awali hadi chuo kikuu kuliko kubadilishia gia ya lugha njiani.

Kinyume chake kwanini kuna shule za english medium?Zifutwe zianze kutumia kiswahili basi?

Interview zote ni kwa kiingireza mtu kupata kazi leo unafundisha kwa kiswahili?
Interview ziwe za kiswahili ili tufaidi badi na hicho kiswahili.

Ukienda mahakamani watanzanua ni bubu ukumbini hawasikii kinachoongelewa na jesi anayoisikiliza ni ya kuuzwa kwa nyumba yake au kuuwawa kwa ndugu yake.

Utambue mtu anajifunza lughaakiwa mdogo , unakuja kumfundisha mtu lugha akiwa kidato cha kwanza?

Kiswahili kifundishwe kama somo ila isiwe lugha ya kufundishia.

Masomo ya sanyansi unayasomaje kwa kiingireza wakati hukijui?

Sijawahi ona mtanzania wa hovyo kutoa maoni ya kielimu kama wewe.
 
Mi naunga mkono hilo la wasio na uwezo kwenda vocational lkn ningependa kuongeza yafuatayo;

1. Wale aanaofeli f2 pia wapelekwe huko badala ya kuwalazimisha warudie kidato......anayefeli f2 siku hizi (kutokana na maswali yenyewe) ni kwamba hajiwezi kabisa huyo kwa lolote lile. Apelekwe tu vocational.
2. Kuwe na mawasiliano jamani na uongozi wa hizi shule za sekondari miezi sita au mwaka baada ya watoto kujiunga kidato cha kwanza ili kujua ukweli ni yupi anafaa sekondari na yupi hafai. Kule primary, kutokana na mashindano ya kufaulisha, hata asiyejua A inaandikwaje anafaulu na kuja kuleta shida kubwa huku sekondari.....wako wengi balaa. Ufuatiliaji wa kina ufanyike ili majina ya hao yapatikane wakajiunge vocational huko kuliko kuwapotezea muda kuwakaririsha habari za sijui 'simile' mara 'metaphor' baadae sijui 'French revolution n.k

3. Na hawa wanaofaulu f2 kwa IV zenye 'c' moja tu za masomo ya Kiswshili au Islamic/Bible serikali iangalie tu namna ya kuwasaidia huko vocational......ukweli ni kuwa hawawezi.
 
Mtoto anasoma masomo karibia yote kwa kiswahilu kwa miaka 7 , ghafla kidato cha kwanza hadi chuo kikuu. Masomo yote anafundishwa kwa kiingireza? Huoni kuna tatizo hapo?

Ni bora masono yote yafundishwe kwa kiswahili kuanzia awali hadi chuo kikuu kuliko kubadilishia gia ya lugha njiani.

Kinyume chake kwanini kuna shule za english medium?Zifutwe zianze kutumia kiswahili basi?

Interview zote ni kwa kiingireza mtu kupata kazi leo unafundisha kwa kiswahili?
Interview ziwe za kiswahili ili tufaidi badi na hicho kiswahili.

Ukienda mahakamani watanzanua ni bubu ukumbini hawasikii kinachoongelewa na jesi anayoisikiliza ni ya kuuzwa kwa nyumba yake au kuuwawa kwa ndugu yake.

Utambue mtu anajifunza lughaakiwa mdogo , unakuja kumfundisha mtu lugha akiwa kidato cha kwanza?

Kiswahili kifundishwe kama somo ila isiwe lugha ya kufundishia.

Masomo ya sanyansi unayasomaje kwa kiingireza wakati hukijui?

Sijawahi ona mtanzania wa hovyo kutoa maoni ya kielimu kama wewe.
Hiyo sentensi ya mwisho🤣🤣🤣🤣🤣
 
Kizungu tunakipa kipaumbele sana, personal sidhani kama ndio tatizo la elimu yetu.

Mfano nchi kama U.K. Mwalimu anaweza vumilia broken English kwenye maandishi but not structure and arguments.

Watanzania awatambui ata umuhimu wa signposting, unaweza kutaka kusikiliza habari/mjadala fulani youtube, yaani ile introduction tu ina kufanya uachane nayo na pengine mbeleni kuna uchambuzi mzuri.

Same thing kwa wenzetu Mwalimu ambae ana kazi 300 za kusahihisha na report za 3000 words if you can’t signpost to engage him, elewa atotumia muda mwingi kuisoma hiyo kazi and most likely aitopata marks nyingi sasa aina maana kazi yote sio nzuri.

Graduates wengi Tanzania awawezi kuandika.
 
Labda tuue kizazi chote.

Serikali ilikosea kuchukua waliofeli kuwasomesha Ualimu.
Unamchuku mtu aliyefeli, afu unampa kazi ya kufundisha wasiojielewa ili wajielewe
Kufeli ni kupata zero nani ana zero na kaenda kusomea ualimu!?
 
Tunachokijua #[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kinyume chake kwanini kuna shule za english medium?Zifutwe zianze kutumia kiswahili basi?

Interview zote ni kwa kiingireza mtu kupata kazi leo unafundisha kwa kiswahili?
Interview ziwe za kiswahili ili tufaidi badi na hicho kiswahili.

Ukienda mahakamani watanzanua ni bubu ukumbini hawasikii kinachoongelewa na jesi anayoisikiliza ni ya kuuzwa kwa nyumba yake au kuuwawa kwa ndugu yake.
Sijaelewa lengo lako mkuu.
1. Unataka elimu iliyopo iboreshwe ? Umebaini mapungufu yapi ktk elimu ya Sasa? Hiyo kubadilika badilika kwa matumizi ya lugha ya kufundishia Kama hakuleti shida yoyote ktk kumpatia mtoto maarifa hakuna shida.

Wapo watoto wanaosoma English medium kuanzia chekechea na vuuo vikuu wanapelekwa nje. Unaridhishwa na ubora wa elimu waliyoipata? Kivipi......? ( Elezea).

2. Au kuna mambo yanafanyika ktk elimu huyapendi ndiyo unataka yaondooewe?
 
Waziri mkenda, ninaomba nikupe ushauri wa bure kabisa kuhusu elimu.

Kwa sasa mambo ya ajira za GPA uko sawa ila anza kufumua mfumu, muundo na mitaala ya elimu nchini.

Prof, hakikisha kila shule ya msingi ina madarasa 2 ya awali na walimu wa awali wenye uwezo wa kufundisha wanafunzi kwa lugha ya Kiingireza.

Elimu kuanzia awali iwe kwa lugha ya kiingireza hadi chuo kikuu na kiswahili kiwe ni somo tu kama masomo mengine.

Somo la kiswahili na hesabu liwe compulsory kuanzia awali hadi chuo kikuu.

Awali mtoto asome miaka miwili tu na msingi mtoto asome miaka 6 na awali mtoto aanze akiwa na umri wa miaka 2-4 tayari kwa kuanza elimu ya msingi ya kuishia darasa la sita.

Mtihani wa la saba ufutwe ili mtoto akimaliza la sita walifanya vizuri kwa matendo na kwa masomo waingie kidato cha kwanza hadi cha nne wasio na uwezo kuanza kidato cha kwanza waingie vicational training school.

Walimu wote wajifunze kufundisha kwa lugha ya kiingireza na wapatikane walimu wa vocstional training soon.

Vyuo vikuu kuna kozi za kufutwa na kuondolewa kwenye mfumo na suala la kusahihisha mitihani ya university isahihishwe kwa Panel sio mtu anajificha na mitihani ya akina dada akisahihishaili akamvue nguo ampatie marks nzuri kiandaa GPA.

Sasa baada ya hapo anza kuongelea ajira kupitia GPA au la.
Futa elimu ya kukaa darasani chekechea ndiyo wakae darasani kuanzia la kwanza ni field mpaka University
 
Mtoto anasoma masomo karibia yote kwa kiswahilu kwa miaka 7 , ghafla kidato cha kwanza hadi chuo kikuu. Masomo yote anafundishwa kwa kiingireza? Huoni kuna tatizo hapo?

Ni bora masono yote yafundishwe kwa kiswahili kuanzia awali hadi chuo kikuu kuliko kubadilishia gia ya lugha njiani.

Kinyume chake kwanini kuna shule za english medium?Zifutwe zianze kutumia kiswahili basi?

Interview zote ni kwa kiingireza mtu kupata kazi leo unafundisha kwa kiswahili?
Interview ziwe za kiswahili ili tufaidi badi na hicho kiswahili.

Ukienda mahakamani watanzanua ni bubu ukumbini hawasikii kinachoongelewa na jesi anayoisikiliza ni ya kuuzwa kwa nyumba yake au kuuwawa kwa ndugu yake.

Utambue mtu anajifunza lughaakiwa mdogo , unakuja kumfundisha mtu lugha akiwa kidato cha kwanza?

Kiswahili kifundishwe kama somo ila isiwe lugha ya kufundishia.

Masomo ya sanyansi unayasomaje kwa kiingireza wakati hukijui?

Sijawahi ona mtanzania wa hovyo kutoa maoni ya kielimu kama wewe.
Nakubaliana na wewe. Kama tuna nia ya dhati ya kufundisha kwa kiswahili basi tuwekeze katikakuhakikisha vitabu vyote vinavyotumika katika elimu vinatafsiriwa kwa kiswahili. Tufanye hivyo hadi chuo kikuu. Tunawezaje kusema kuwa tunakienzi kiswahili wakati hata vitabu vya Abdulrazak Gurnah tulishindwa kuvitafsiri kwa kiswahili? Kitabu chake "Paradise" kimetafsiriwa mwaka jana baada ya kushinda Nobel Prize. Hao wenzetu wanaofanya vizuri katika elimu wamewekeza katika tafsiri ya maandishi yote muhimu katika kila fani lugha zao.
Ukweli ni kuwa hata tukijitahidi vipi hatuna resources za kutafsiri kwa kiswahili vitabu vyote muhimu. Itachukua muda. Basi wakati tuko katika transition period tuwatendee haki watoto wetu kwa kuhakikisha wanapata elimu katika lugha watakayoitumia hadi chuo kikuu.

Amandla...
 
Sijaelewa lengo lako mkuu.
1. Unataka elimu iliyopo iboreshwe ? Umebaini mapungufu yapi ktk elimu ya Sasa? Hiyo kubadilika badilika kwa matumizi ya lugha ya kufundishia Kama hakuleti shida yoyote ktk kumpatia mtoto maarifa hakuna shida.

Wapo watoto wanaosoma English medium kuanzia chekechea na vuuo vikuu wanapelekwa nje. Unaridhishwa na ubora wa elimu waliyoipata? Kivipi......? ( Elezea).

2. Au kuna mambo yanafanyika ktk elimu huyapendi ndiyo unataka yaondooewe?
Mapungufu ya elimu ya Tanzania
1. Language of instruction ni Tatizo la kwanza
2. Mtaala ni too theretical than practical
3. Kozi zinazotolewa vyuoni hazioni na soko la ajira, nyingi zimepitwa na wakati au Supply sio sawa na demand
4. Siasa pia inaharibu elimu eti ili kiongozi ajue kusoma na kuandika .
5. Hakuna vocational training za kutosha
7. Technical college ya Dar, mbeya naarusha zianze upya na masuala ya degree kwenye hivyo vyuo zifutwe.
8. Kuwepo na shule za sekondari za ufundi kuanzia msingi hadi sekondari
9. Azimio la musoma ni muhimu kupitiwa upya na liwepo
10. Serikali ianzishe vyuo vya ualimu vya kufundisha walimu wa ufundi
11. Mtaala wetu kwa ujumla umpepitwa na wakati
12. Tuwe na lugha moja ya kufundishia kuanzia awali hadi chuo kikuu
13. Kila shule iwe na mtaalamubwa maabara na kila shule iwe na vifaa vya sayansi vya kutosha
14. Tehama , hesabu na kiswahili iwe ni somo la kusomewa kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.
15. Shule za msingi zote zisiwe za bweni ili kukuza maadili ya watoto,wazaxi wamekuwa wakikimbia watoto na kuachia walimu watoto
16. Wanasiasa wamekuwa wakinunua Degree ,sasa iundwe tume ya kupitia waliopata degree hizo na watakaondelea kuzipata.
 
Back
Top Bottom