Mkuu hebu twende taratibu. Mwanzoni umesema waziri arekebishe mitaala na tuwe na lugha moja ya kufundishia . Nataka tukikite hapo halafu ndipo tuangazie changamoto niyingine.Mapungufu ya elimu ya Tanzania
1. Language of instruction ni Tatizo la kwanza
2. Mtaala ni too theretical than practical
3. Kozi zinazotolewa vyuoni hazioni na soko la ajira, nyingi zimepitwa na wakati au Supply sio sawa na demand
4. Siasa pia inaharibu elimu eti ili kiongozi ajue kusoma na kuandika .
5. Hakuna vocational training za kutosha
7. Technical college ya Dar, mbeya naarusha zianze upya na masuala ya degree kwenye hivyo vyuo zifutwe.
8. Kuwepo na shule za sekondari za ufundi kuanzia msingi hadi sekondari
9. Azimio la musoma ni muhimu kupitiwa upya na liwepo
10. Serikali ianzishe vyuo vya ualimu vya kufundisha walimu wa ufundi
11. Mtaala wetu kwa ujumla umpepitwa na wakati
12. Tuwe na lugha moja ya kufundishia kuanzia awali hadi chuo kikuu
13. Kila shule iwe na mtaalamubwa maabara na kila shule iwe na vifaa vya sayansi vya kutosha
14. Tehama , hesabu na kiswahili iwe ni somo la kusomewa kuanzia darasa la kwanza hadi chuo kikuu.
15. Shule za msingi zote zisiwe za bweni ili kukuza maadili ya watoto,wazaxi wamekuwa wakikimbia watoto na kuachia walimu watoto
16. Wanasiasa wamekuwa wakinunua Degree ,sasa iundwe tume ya kupitia waliopata degree hizo na watakaondelea kuzipata.
Mitaala ya sasa Ina mapungufu yapi? Na waliosoma English medium toka chekechea mpk vyuo vikuu wameyaepuka mapungufu yanayosababishwa na kuchanganya lugha? Wameelimika vizuri kuliko waliopita st. Kayumba? Wana tija kwenye jamii kuliko wa st. Kayumba?