DOKEZO Waziri Mkenda, tuondolee huyu Mwalimu mlawiti hapa Mbeya, sasa inatosha!

DOKEZO Waziri Mkenda, tuondolee huyu Mwalimu mlawiti hapa Mbeya, sasa inatosha!

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Salaam Wakuu,

Mbeya kuna mwalimu ambaye sina haja ya kumtaja sababu serikali inamjua. Yeye kazi yake ni kutembea na watoto wa kiume kinyume na maumbile. Taarifa zilishatolewa kila sehemu ila hatua hazichukuliwi pamoja na ushahidi.

Natumia nafasi hii kumuomba waziri wetu msikivu Prof. Mkenda, kwake ni jambo dogo.

Huyu mwalimu mwaka 2013 alibaka akalindwa.

Kwa sasa analawiti watoto wa shule na kesi ipo polisi lakini wakubwa zake wanamlinda na kesi haiendi mahakamani. Badala yake wamemuhamisha na kumshusha cheo hapa Mbeya DC.

Mimi huwa siongelei haya mambo JamiiForums ila imenilazimu. Watoto wetu tuwafiche wapi. Muondoeni serikalini, anatia aibu. Mlawiti huyu kila mtu serikalini anamjua.

Asante Mkenda.
View attachment 2348182
Vitu vingine muwe mnahukumu wananchi tu Hapo. Hapo Bila Kujali..
 
Tulitegemea uje ulete habar amekamatwa amefikishwa mahakaman na amehukumiwa... Ila sio kutuletea upuuzi huu, haiwezekani mamlaka zote zimshindwe huyo mtu ni wew au na wenzako ndio mnamlinda mnamuogopa...
Nenda ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule (almaarufu Wakaguz wa shule) hawa wapo chini ya Wizara ya Elimu wanapokea taarifa kwa siri kubwa iwe ya kweli au ya uongo huanza kuifanyia kazi mapema wanaenda kuanza uchunguz na kufanya mahojiano ya siri kwa watu mbalimbali ktk mazingira tofaut tofaut na wakat tofaut, ofisi zao zipo kila Wilaya mara nyingi wapo jirani na ofisi za halmashauri... hawa wakisema mwl fulani au mratibu elimu kata fulani hafai hapohapo mkurugenz anamuondoa huyo mtu na taasisi ya nidham ya walimu (TSC) wanamfuta kazi huyo mwl bila hata ya kwenda nae mahakaman, Nasema tena nenda ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule...
 
Kama itamlazimu Mkenda kufanya hayo maamuzi, na kama tuhuma zikithibitishwa basi wawajibishwe kuanzia afisa elimu wilaya, kata na mkuu wa shule husika, na yeyote alipokea hizo taarifa akazificha uvunguni. Ndiposa asulubiwe huyo bazazi.
 
Najua Mkuu, ila nataka RPC ndo amtaje. Sababu taarifa anayo na ndo mwalimu pekee ana kezi ya Ulawiti kwa wanafunzi. Anajulikana. Kama hatua isipochukuliwa nitamtaja. Tuwapime kwa mara ya mwisho watendaji wa Raisi Samia
RPC anaanzaje sasa kumtaja wakati umesema wanamlinda??
 
Sasa Kama vielelezo vipo huyo mlawiti anafanya Nini mtaani . So apelekwe tu jela akakutane na mabingwa wenzie huko.
 
Hiyo picha ya mkono wa mwanaume kuushika mkono wa mwanamke ndio ushahidi! Acha kutafsiri ndoto zako hapa.
 
Unakwama wapi mwalimu ebu mtaje kwa kina kuwa mwalimu furani wa shule furani ili watu watule kuanzia afisa elimu wake,mratibu elimu kata wake mpaka bosi wake kumbuka jumaa watu wanamaamuzi kabla hata mlenda ajafika washaruka naye
 
Tulitegemea uje ulete habar amekamatwa amefikishwa mahakaman na amehukumiwa... Ila sio kutuletea upuuzi huu, haiwezekani mamlaka zote zimshindwe huyo mtu ni wew au na wenzako ndio mnamlinda mnamuogopa...
Nenda ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule (almaarufu Wakaguz wa shule) hawa wapo chini ya Wizara ya Elimu wanapokea taarifa kwa siri kubwa iwe ya kweli au ya uongo huanza kuifanyia kazi mapema wanaenda kuanza uchunguz na kufanya mahojiano ya siri kwa watu mbalimbali ktk mazingira tofaut tofaut na wakat tofaut, ofisi zao zipo kila Wilaya mara nyingi wapo jirani na ofisi za halmashauri... hawa wakisema mwl fulani au mratibu elimu kata fulani hafai hapohapo mkurugenz anamuondoa huyo mtu na taasisi ya nidham ya walimu (TSC) wanamfuta kazi huyo mwl bila hata ya kwenda nae mahakaman, Nasema tena nenda ofisi za Uthibiti Ubora wa Shule...
Kwa hiyo wamhamishie wapi?

Sent from my SM-T555 using JamiiForums mobile app
 
Kwa sasa analawiti watoto wa shule na kesi ipo polisi lakini wakubwa zake wanamlinda na kesi haiendi mahakamani. Badala yake wamemuhamisha na kumshusha cheo hapa Mbeya DC.
Labda na wao hupewa dose
 
Usipomtaja jina na shule anayofundisha hapo Mbeya DC hii taarifa yako inakuwa Ni umbeya tuu, nakuomba mtaje jina na shule anayofundisha ili tukampe somo, pumbavu kabisa Ticha huyo😞😞😞
 
Hapo hata haujafanya chochote Huyo wazuri mkenda atasgughulikaje na mtu hamfahamu, taja jina, na shule anayofundisha waziri atalala na mbele kama tuhuma zikithibitishwa kwani ID Yako wanaifahamu
 
Usipomtaja jina na shule anayofundisha hapo Mbeya DC hii taarifa yako inakuwa Ni umbeya tuu,nakuomba mtaje jina na shule anayofundisha ili tukampe somo,pumbavu kabisa Ticha huyo[emoji20][emoji20][emoji20]
Anatumia id fake na anakuwa muoga

Na cha kusikitisha kesi bado ipo

Kwa uoga huu wacha wana mbeya waendelee kulizwa mpka akili itakapo wakaa sawa
 
We jamaa bhana...eti eti DC anamfahamu sijui Police wanamfahamu...sasa hapa JF inatuhusu nini kama hata wewe huna mbavu za kumtaja.
Endeleeni kumlea hadi akili iwakae sawa
 
Back
Top Bottom