Waziri Mkuu aokoa mamilioni, atembea kwa miguu kwenda ofisini

Basi habari kama hiyo utakuta inapewa headline kuuuubwaaa na kusahau ile ya pesa ya msaada ya kagera iliyoruka viunzi
 
Mahaba niuwe....ukipenda chongo huona kengeza! Ukipenda pengo huona mwanya

Kila mtu yupo hivyo hivyo hata wewe unapopenda hata ukiambiwa huyu ni darasa la saba, wewe huyo huyo tu, kweli mapenzi upofu
 
Serikali ya ajabu sana hii jamani!
Imeshindwa kwenye kila kitu lkn sasa wanataka kuuvaa u Nyerereism kwa kutembea kwa miguu
Hivi akitembea kwa miguu ndiyo mwanangu atapata mkopo wa elimu ya juu?
 
siku zote anatumiaga magari kwa hizo mita 200?
 
Hii serikali ya muhula huu 'imewapumbaza' wengi sana, kiasi kwamba si ajabu mtu kuita tui la nazi maziwa...

Yaani vitu very ordinary vinabatilishwa na kupewa utukufu wa extra ordinary...
 
Mshana unashangaa kuwepo maamuma wa taarifa hiyo? hii hesabu rahisi kabisa huijui? Katika kila Watanzania wanne, mmoja ni kichaa. Tanzania ina watu takribani 50,000,000. Hivyo 1/4 ya 50,000,000 ni 12,500,000. Vichaa milioni kumi na mbili na nusuπŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€πŸ˜€...hawa ndio wanapigia vigelegele uchafu wowote ili mradi umefanywa na mabwana wakubwa
 
Kama ni mita 200 na ni msafara wenye magari 6 basi ya kijipanga tu kuaza msafara gari la kuongoza litakuwa lango kuu la kuingia ofisi ya pm

Asingetembea ingekuwa kashfa kwake.

Na washawasha!
 
Atafakari na kulinganisha umbali alotembea Nyerere akiunga mkono AZIMIO LA ARUSHA na 200m za kwake! Alikua mwalim wa sayansi kimu au hesabu!?
 
Hatari! 12,500,000 wote hao? Usikute hata wakina MOTOCHINI wapo kwenye kundi hilo ndio maana hawajamuelewa mshana jr anamaanishi nini kwenye hoja hii na wanaishia kumkejeli
 
Hyo aliyeripot habar hyo n boya m nlodhan katembea kilo mta tan kumbe mita mia mbili? Hapo ndo kaokoa mamilion? Mfyuuuuuu mijitu mingine bana tushawachoka na kiki zenu zisizo na tija
 
Labda tungejua kuwa kaokoa milioni ngapi kwa umbali huo.
 
Ndiomaana mimi wakati mwingine sitakagi kuongea.

Sasa mtu kama katembe kutoka mwisho wa uwanja wa mpira na katembea hadi kwenye gori lingine na kuludi ndio iwe gumzo!

Issue siyo gumzo tu mkuu, eti kaokoa mamilion ya pesa, jamani hivi hata angetumia V8 sita kwa msafara wa mita 200 zingetumia petrol hata ya laki kweli kwa zote 6 ??

Upuuzi mtupu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…