Mulhat Mpunga
JF-Expert Member
- Oct 28, 2010
- 27,256
- 16,317
ati niniWanabana matumizi alafu zilizo okolewa analipwa ProPesa afanye ziara mikoani kwangu hiki ni kichaa na kama kutembea mita 200 ni habari basi tuna safari ndefu na hawa bongo movie waliojificha kwenye uongozi wa serikali yetu.
Umeumbiwa roho ya upendo na uvumilivu
pata gari safi kabisa kwa 3 milioni tshs
Mita 200 hiyo inatofauti gani na kutoka ndani kwenda chooni kwa wale tunaokaa vijijini..Isichukuliwe kama dhihaka! Isichukuliwe kama maskhara na furahisha genge! Bali ikupe fikra fikirishi ya huko tunakoelekea na dhana nzima ya kubana matumizi.
Akiripoti kutoka Dodoma mwandishi wa kituo cha WAPO RADIO, amesema wananchi wa Dodoma Leo wamesifu kitendo cha Waziri Mkuu cha kutembea kwa miguu UMBALI WA MITA 200 kutoka makazi yake-Ikulu ndogo ya Dodoma hadi ofisini kwake (zingatia mita 200)akiwa na walinzi wachache.
Kitendo hicho kimetajwa kama kitendo cha aina yake chenye UADILIFU kilichookoa MAMILIONI YA PESA ambayo yangetumika kwenye msafara wa magari yasiyopungua sita.
Tuupinge kwa nguvu zote huu upuuzi, mwendo wa mita 200 katika uhalisia wake mtu anaweza kupanda gari na msafara?
Je kama Leo imeonekana ni ajabu ina maana siku zote ndivyo ilivyo?
Je kutembea mita 200 ni kubana matumizi?
Ni habari za namna gani hizi jamii inapewa?
Ina maana Dodoma leo kuanzia asubuhi hakukuwa na habari nyingine zaidi ya hii?
Hii breaking news imeniacha na maswali mengi.
Mita 200 ni sawa na viwanja viwili vya mpira, kabla hujabadili gia umeshafika mwisho!!Mita 200 hiyo inatofauti gani na kutoka ndani kwenda chooni kwa wale tunaokaa vijijini..
Hivi bado yupo dodoma!!Baada ya kurudia kusoma uzi nimejikuta nacheka tu !
Huwa anakuwa na msafara wa magari SITA kwa mwendo wa mita 200? Imagine ulinzi wote huu kwenye "kisiwa cha amani".
Japo Salva Kiir wa South Sudan yupo kwenye state of emergency na kule kula bullet ni suala la kawaida, protection detail yake haipo extravagant namna hii.
Swali lingine. Je Tanzania tuko vitani mpaka waziri mkuu asindikizwe na watu sita anapotembea mita 200 kwenda ofisini kwake kutoka ofisi nyingine????
Nchi yetu imegeuka kuwa nchi gani?