Waziri Mkuu aongoza msafara wa kupokea mwili wa Balozi Kijazi

Waziri Mkuu aongoza msafara wa kupokea mwili wa Balozi Kijazi

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Februari 18, 2021 ameongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Pichani, Mheshimiwa Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wailoshiriki katika kuupokea mwili huo wakimpa pole, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi ambaye alikuwa ni mmoja wa Wanafamilia na viongozi wa serikali waliosafiri pamoja na mwili wa marehemu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Kijazi.jpg
 
Brother Majaliwa akiendelea kuwa mkaidi wa kutokuvaa barakoa litamkuta jambo. Yetu macho 🤔
huenda anatamani sana kuvaa barakoa lakin anaogopa wanadamu...
any way wanapaswa kujiongeza mapema
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Februari 18, 2021 ameongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam....
Viongozi wa Tanzania; Tatizo nini!?

1) Social Distance haijazingatiwa.

2) Barakoa wengi wenu mmepuuza.

Namna hii kweli tutaweza kutokomeza hili janga la Coronavirus!
 
Sasa msafara umekuja Dar kufanya nini wakati anazikwa Tanga, au nilisikia vibaya?
 
Huenda kuna kundi la viongozi wa serikali walishajipatia chanjo, sasa wanatuzuga ili tuamini wanachosema wanakiqmini na kukisimamia.
 
huenda anatamani sana kuvaa barakoa lakin anaogopa wanadamu...
any way wanapaswa kujiongeza mapema
Very strange, unaogopa binadamu over your healthy? We live once....
 
Ni mdogo wa marehemu,alikuwa tanapa dada yao ni yule wa hali ya hewa,wasambaa hawa mama yao alizaa
Wamejua kubebana. Nimeangalia CV ya dada yao(mdogo wao)kumbe alianzia vi certificates. Degree ya kwanza kapata akiwa na miaka 37 tena Nairobi huko,masters kasomea South Africa.

Itakuwa Kaka yake alimbeba sana aisee. Kaanzia vi certificate mpaka PhD.Hongera kwao itakuwa wazazi wao waliwalea kwa Upendo na wakawafundisha umoja.
 
Back
Top Bottom