Waziri Mkuu aongoza msafara wa kupokea mwili wa Balozi Kijazi

Waziri Mkuu aongoza msafara wa kupokea mwili wa Balozi Kijazi

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Februari 18, 2021 ameongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Pichani, Mheshimiwa Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wailoshiriki katika kuupokea mwili huo wakimpa pole, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi ambaye alikuwa ni mmoja wa Wanafamilia na viongozi wa serikali waliosafiri pamoja na mwili wa marehemu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

...Naona Kuvaaa Barakoa bado ni Anasa kwa Mujibu wa hao Wapokeaji hapo...![emoji848]
 
Huyo anaewasalimia kafanana na marehemu jamani. Kidogo nisema marehemu kafufuka.
..Nahisi ndio anayetajwa hapo kuwa Allan Kijazi.
Kwa mfanano huko nafhani ni Mdogo wake Marhum.

Kaka Katibu Mkuu Kiongozi, mdogo Mtu Naibu Karibu Mkuu? Ama Sijaelewa?
 
Wamejua kubebana. Nimeangalia CV ya dada yao(mdogo wao)kumbe alianzia vi certificates. Degree ya kwanza kapata akiwa na miaka 37 tena Nairobi huko,masters kasomea South Africa.

Itakuwa Kaka yake alimbeba sana aisee. Kaanzia vi certificate mpaka PhD.Hongera kwao itakuwa wazazi wao waliwalea kwa Upendo na wakawafundisha umoja.

Dada yao ndo yule Agnes Kijazi wa hali ya hewa
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo Februari 18, 2021 ameongoza mapokezi ya mwili wa aliyekuwa Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi kwenye Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Pichani, Mheshimiwa Majaliwa pamoja na viongozi mbalimbali wa serikali wailoshiriki katika kuupokea mwili huo wakimpa pole, Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Allan Kijazi ambaye alikuwa ni mmoja wa Wanafamilia na viongozi wa serikali waliosafiri pamoja na mwili wa marehemu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

RIP
 
Back
Top Bottom