Waziri Mkuu auponda mpango wa kutumia viberenge kupanda Mlima Kilimanjaro

Waziri Mkuu auponda mpango wa kutumia viberenge kupanda Mlima Kilimanjaro

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewataka wadau wanaopendekeza matumizi ya viberenge katika kupanda Mlima Kilimanjaro kutathimini kwa kina mpango huo ambapo ameonyesha kutoridhia mikakati hiyo.

"Nasikia mnataka kuweka kiberenge cha kupanda Mlima Kilimanjaro, mnataka kuua mlima? Mkiweka machuma ya kupanda mlima mtaharibu, nataka mje mseme wapagazi mtawapeleka wapi na hizo ndiyo ajira zao, endeleeni kulijadili hilo mje na sababu zilizo tosha,” amesema Waziri Mkuu.

Ameyasema hayo katika hotuba yake aliyoitoa akiwa Chuo Cha Ushirika Moshi katika kilele cha mbio za Kilimanjaro Marathon mkoani Kilimanjaro, leo Jumapili Februari 27, 2022 alipokuwa mgeni rasmi.
 
Dah Hilo jina viberenge. Majina ya vitu na watu kwa kimatumbi yani Kero. Walibadilishe Bana.

Na hivyo viberenge vikiwekwa vitafankshen kwa umeme upi? Na msaada na mkopo kutoks wapi?

Penda sana vitu vikubwa vikubwa na uwezo hatuna.

Putin sucks!
 
Yuko sahihi kwani uharibifu mkubwa sana wa kukata miti utafanyika, ni wazi kutakuwa na barabara mbili ya kupanda na kushuka, pia muda wa watalii kukaa hotelini utakwisha na ajira za wapagazi zitakoma pamoja na wauza kahawa na vitu vya asili watakosa wanunuzi na mwisho watalii wa mazingira watasusa kuja kutokana na uharibifu utakaofanyika.
 
Kabisaa.
Yani safari ya siku 8 ifanyike kwa 1 hour mlima utachukuliwa poa kama kichuguu tu na hautakua na value tena coz safari ya usd 2500 itafanyika kwa usd 100.
Safari ambayo ingewahusisha wafanyakazi 12 itakua inachukua mfanyakazi 1 tu.
upo sahihi,lakini simuelewi PM hoja yake ya kwamba machuma yataharibu mlima
 
Mambo lazima ya badilike, watakao panda kwa miguu na wapande viberenge ndiyo mambo ya sasa.
Kabisa mkuu, surely WM kapotoshwa big time. Ukweli ni kwamba hivyo viberenge vitaleta new customers ambao hawapendi kupanda mlima kwa miguu kwa sababu mbalimbali, ikiwemo maradhi, ulemavu, afya, fedha etc... Ni makosa kudhani kwamba viberenge vitachukua nafasi ya wapandaji mlima kwa kutembea. Kumbuka Kuna kundi kubwa sana ambalo kwao adventure ni kutembea /hiking milimani na misituni. Hawa hata ulete viberenge huwezi kuwashawishi, hivi wale watu wanaofanya mazoezi kama jogging au kwenda gym hawana magari? Mwisho it seems watu hawazijui hizi cable cars/au viberenge na jinsi vinavyofanya kazi.
 
Kabisaa.
Yani safari ya siku 8 ifanyike kwa 1 hour mlima utachukuliwa poa kama kichuguu tu na hautakua na value tena coz safari ya usd 2500 itafanyika kwa usd 100.
Safari ambayo ingewahusisha wafanyakazi 12 itakua inachukua mfanyakazi 1 tu.
Sasa sie walemavu tunaotaka kufika kileleni mnatuangaliaje
 
huvi

johnthebaptist
ndege JOHN

na wewe mtoa mada ni mtu mmoja?

Yasemekana na TV online yake i mbioni kufunguliwa. Suala la muda tu sasa:

IMG_20220225_202247_875.jpg
 
"Mama" yeye anasemaje kuhusu hili suala ? Asije akashinikizwa ...
 
Kabisa mkuu, surely WM kapotoshwa big time. Ukweli ni kwamba hivyo viberenge vitaleta new customers ambao hawapendi kupanda mlima kwa miguu kwa sababu mbalimbali, ikiwemo maradhi, ulemavu, afya, fedha etc... Ni makosa kudhani kwamba viberenge vitachukua nafasi ya wapandaji mlima kwa kutembea. Kumbuka Kuna kundi kubwa sana ambalo kwao adventure ni kutembea /hiking milimani na misituni. Hawa hata ulete viberenge huwezi kuwashawishi, hivi wale watu wanaofanya mazoezi kama jogging au kwenda gym hawana magari? Mwisho it seems watu hawazijui hizi cable cars/au viberenge na jinsi vinavyofanya kazi.
Wewe umeshawahi kupanda mlima Kilimanjaro?
 
Kabisaa.
Yani safari ya siku 8 ifanyike kwa 1 hour mlima utachukuliwa poa kama kichuguu tu na hautakua na value tena coz safari ya usd 2500 itafanyika kwa usd 100.
Safari ambayo ingewahusisha wafanyakazi 12 itakua inachukua mfanyakazi 1 tu.
Mtalii ambaye ilibidi akae wiki mbili atakaa siku tatu tu amesepa,
 
Watu wanataka kufika kileleni bana namna gani kileleni ndio mpango mzima.kufika keleni raha
 
Back
Top Bottom