Waziri mkuu Dkt Mwigulu Lameck Nchemba awasili Ufaransa kumwakilisha Rais katika siku ya Kiswahili

USSR

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2015
Posts
12,213
Reaction score
28,916
WAZIRI MKUU AWASILI UFARANSA KUMWAKILISHA RAIS SAMIA KWENYE MAADHIMISHO YA SIKU YA KISWAHILI DUNIANI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mwigulu Nchemba, amewasili jijini Paris, Ufaransa leo, Julai 6, 2026, kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani yanayofanyika katika Makao Makuu ya UNESCO.

Mara baada ya kuwasili, Mheshimiwa Waziri Mkuu alipokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa Thabit Kombo, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Saidi Yakubu na maafisa wengine wa ubalozi.

Katika maadhimisho hayo, Tanzania itaendelea kuonesha nafasi yake ya kipekee katika kukuza, kuhifadhi na kuieneza lugha ya Kiswahili duniani, sambamba na kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kupitia lugha hiyo.
 
Guys guys
Anapokea rushwa cash kwenye sandarusi huyu mwizi tu
 
Taarifa Kwa Umma

Waziri Mkuu Kumwakilisha Rais Samia Ufaransa.
 

Attachments

  • IMG-20260706-WA0003.jpg
    262.1 KB · Views: 17
Naandika nikiwa na Masikitiko Makubwa sana Juu ya Taifa langu na Selikali hii ya Awamu ya sita.
Mimi ni Mtumishi wa Mungu nitaandika kwa Kifupi sana.

Mungu alimpa Musa Torati na ndani yake Kulikuwako Sheria Amri na Hukumu, kuwaongoza wama wa Islael.

Amri zake zilikuwa kumi ambazo nimeziona zote zikivunjwa na selikali ya Tanzania, Lakini zaidi naona nyingine zikivunjwa wazi wazi bila hofu wala Uoga.

1. UONGO.
Kila kitu kinachofanywa na hawa watu ni Uongo wa wazi kwa kisingizio cha Propaganda.
Mnawakwaza sana watu hata ambao hawana upande mnawapeleka upande wa haki, Mnajichimbia kaburi kwa Maneno ya Uongo.

2. USIUE.
Hii ni amri ya Mungu inayikataza kufanya Mauaji juu ya Binadamu mwenzio.
Selikali hii imekuwa Ikiua Raia, October 29, Ikiteka, Ikitesa nk

3. WIZI.
Hawa ni Majizi wa kura.
Wanaiba kura kwa kushirikiana na waalimu, polisi na wakurugenzi kuiba matokeo ambayo si halali.
Wanawanyima watanganyika Uhuru wa kuchagua kiongozi wanaye mtaka. Wanawaibia utajili Shahabu, Madini Gas nk
Mungu alikuwa na Makusudio yake vkuviweka hapa Tanzania.

MWIGULU ACHA DHAMBI, ACHA UONGO. MAGUFULI NILIMWAMBIA HIVI HIVI.

MENE MENE TEKELI NA PERESI
 
Waste of time and money ๐Ÿšฎ๐Ÿšฎ๐Ÿ—‘๏ธ๐Ÿ’ฉ
 
kila la kheri Dr Mwigulu Nchemba, waziri mkuu wa Tanzania.

Kiswahili hoyeee ๐Ÿ”ฅ๐Ÿ”ฅ
 
DKT. MWIGULU KUMWAKILISHA RAIS SAMIA MAADHIMISHO SIKU YA KISWAHILI DUNIANI, PARIS

Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba amewasili kwenye Makao Makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) jijini Paris Nchini Ufaransa na kupokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Profesa Khaled El-Enany, leo Julai 7, 2026.

Mheshimiwa Dkt. Mwigulu yupo nchini Ufaransa kumwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwenye Maadhimisho ya Tano ya Siku ya Kiswahili Duniani.
 

Attachments

  • IMG-20260707-WA0062.jpg
    485.2 KB · Views: 16
  • IMG-20260707-WA0061.jpg
    422.6 KB · Views: 14
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ