Waziri Mkuu haondolewi kirahisi mnavyodhania. Akiondolewa Baraza la Mawaziri linavunjwa lote

Idugunde

JF-Expert Member
Joined
May 21, 2020
Posts
6,404
Reaction score
6,969
Mnapiga ramli juu ya PM Kassim kuondolewa mnadhania ni rahisi kama mnavyodhania?

Akiondolewa basi mtambue kuwa baraza zima linavunjwa na raisi anateua na kuapisha upya.

Someni ibara ya 57(2)(e) ya katiba ya JMT na muache kukurupuka kupiga ramli za kishamba.
 
Waziri mkuu anaondolewa na Rais kama waziri mwingine yeyote, acha kutishia watu wazima nyau.
Katiba ya JMT 1977
51.- (3) Bila ya kuathiri masharti mengineyo ya Katiba hii, Waziri Mkuu atashika kiti cha Waziri Mkuu hadi- (a) siku ambapo Rais mteule ataapa kushika kiti chake; au (b) siku ambapo atafariki dunia akiwa katika madaraka; au (c) siku atakapojiuzulu; au (d) siku Rais atakapomteua Mbunge mwingine kuwa Waziri Mkuu; au (e) atakapoacha kushika kiti cha Waziri Mkuu kwa mujibu wa masharti mengineyo ya Katiba hii.
 
Tuwekee na 57(2)(e), mnakurupuka kujadili mambo mazito wakati hamna akili.
 
Akiondolewa basi mtambue kuwa baraza zima linavunjwa na raisa anateua na kuapisha upya

Mabadiriko ya Baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais ni sawa na kulivunja Baraza na kuliunda upya hivyo baada ya Spika wa Bunge kupatikana litapelekwa jina la mtu atakayependekezwa kuwa Waziri Mkuu ili athibitishwe na bunge!
 
Mnapiga ramli juu ya PM Kassim kuondolewa mnadhania ni rahisi kama mnavyodhania?

Akiondolewa basi mtambue kuwa baraza zima linavunjwa na raisa anateua na kuapisha upya.

Someni ibara ya 57(2)(e) ya katiba ya JMT na muache kukurupuka kupiga ramli za kishamba.
You know nothing. Bera shut up
 
Mabadiriko ya Baraza la mawaziri yaliyofanywa na Rais ni sawa na kulivunja Baraza na kuliunda upya hivyo baada ya Spika wa Bunge kupatikana litapelekwa jina la mtu atakayependekezwa kuwa Waziri Mkuu ili athibitishwe na bunge!
Wewe unajua unachopost? Au unapost mradi kubisha?
 
Back
Top Bottom