Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza zawadi ya cheni aliyopewa mkewe iuzwe ili kujenga bweni la Wanafunzi Simanjiro

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa aagiza zawadi ya cheni aliyopewa mkewe iuzwe ili kujenga bweni la Wanafunzi Simanjiro

Atamnunulia kwa mshahara wake ambayo itakuwa na thamani zaidi ya hiyo zawadi.
Kama hivyo sawa.

Ila wengine wetu wangetaka ile ile na ingine juu ya mume.

Yaani tungesema kabisa tunanunuliwaje na watu wa nje. Na wewe tununulie.
 
Huyo ni mke wa Waziri wa nchi, hana sifa za nyie wanawake njaa kali! Ukiwa mkubwa lazima uchague bhana, unafikiri hao wakuu wanaoa oa tu kwa kuokoteza vitu vya ajabu ajabu kama nyie[emoji23][emoji23][emoji23]
Hujui unachokiandika wewe.

Kisirani tu kama mshahara wako nalipa mie.

Kibwengo weye.
 
Kwani inawezekana kweli mama PM hakuwa na mkufu wa dhahabu au tanzanite? Au ina maana PM hawezi kumnunulia my wife wake mkufu wa tanzanite? Ni vizuri viongozi wa wananchi wanapoepuka mitego ya wazi ya wafanyabiashara.
Women never get enough of jewellery, shoes or clothes my dear friend.
 
Kipindi cha Mzee Mkapa, Mkapa akiwa Rais na Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi waliwahi kupewa dhahabu na GGM! Mkapa alipewa tofali na Magufuli koreo,sasa sijui waliyapeleka wapi hawa watu
wadau walipiga kelele sana lakin yule Mzee alikuwa jeuri
 
Hivi kweli tanzanite moja inajenga bweni moja?aise nmeogopa
 
Ila hakupewa yeye Ile ni zawadi binafsi

Aache wivuuuu
 
Kipindi cha Mzee Mkapa, Mkapa akiwa Rais na Magufuli akiwa Waziri wa Ujenzi waliwahi kupewa dhahabu na GGM! Mkapa alipewa tofali na Magufuli koreo,sasa sijui waliyapeleka wapi hawa watu
Tutawaulizaje wakati hawapo tena?
 
Tungeliweza kumpima vizuri integrity yake, kama angalipewa kisirisiri halafu yeye akaamua kufanya kama alivyofanya.
 
Hii serikali imejikita katika elimu kwa sasa kila mtu ni msomi ila hajira hakuna..hili ni bomu
 
Kwa ufahamu wangu mimi kwa mujibu wa sheria na kununi za utumishi wa umma, ukipewa zawadi kwaajili ya cheo chako au nafasi yako katika Serikali, Hiyo zawadi inakuwa sio yako, inatakiwa kuwasilishwa Serikalini, ni mali ya Serikali. Majaliwa amefanya kwa mujibu wa sheria na kanuni. By the way ameepuka mtego mkubwa sana ambao ungekuja kumsumbua baadaye.
 

MAJALIWA AAGIZA CHENI YA MKE WAKE IUZWE.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ameishukuru kampuni ya Tanzanite Forever Lapidary (T) LTD ya mkoani Manyara,kwa kumzawadia mkewe, Mama Mary Majaliwa mkufu wa Tanzanite.

Hata hivyo,Waziri Mkuu ameagiza mkufu huo uuzwe, ili ipatikane fedha,itakayosaidia kujenga bweni la wanafunzi katika moja ya shule zilizopo wilayani Simanjiro.

Waziri Mkuu amehitimisha Ziara yake ya Siku nne, Mkoani Manyara.

Source: Watetezi TV
Amekwepa mtego mkubwa sana. Naona Majaliwa ni Smart sana upstairs!
 
Back
Top Bottom