Waziri Mkuu Kassim Majaliwa acha siasa za ujanja ujanja

Tangu alipotupiga kamba kuwa Magufuli yuko vyema na anaendelea na majukumu yake ya kiofisi (ikulu) kumbe mzee wetu anapigania maisha yake ..kwanzia hapo huyu Ca-phone sijawahi mkubali.
Majaliwa kwa sasa ana credibility crisis!
 
Unapokuwa na viongozi wa aina hiyo huko juu kabisa serikalini, urategemea vipi hawa wa chini wafanye kazi kwa ufanisi?

Maana yake ni kwamba uozo utaendelea kuwepo ndani ya serikali yote hata kama hao hao wakubwa watakuwa wanajinadi kuwa wasimamizi wa walio chini yao.

Wao hawatumbuliwi wakati ndio wanaolea uozo; badala yake wanawatumbua wanaotafuta kufanya kazi kwa njia nyoofu.
 
Kaka Kassim anayo vita pevu na Kaka Kakoko aliyekuwa Bandarini. Tatizo ni kwamba Kassim kashika mpini na walalamikaji wengine wameshika makali.

Jingine ni ukweli kuwa Kaka Kassim akiwa kando na Mama Samia wanayo sababu ya pamoja ya kubakia team moja (common cause). Mama anamhurumia Kassim akikumbuka mateso waliyoyapata chini ya JPM, Hivyo huruma ya Mama ipo kazini.
 
Kumekucha , Majaliwa Kuna ujumbe wako huku , chunguli kidogo
 
Yaani huyu nikikumbuka ile hotuba yake ya Njombe kuhusu afya ya JPM huwa simwamnini tena. Mwongo sana!
 

Thank you

Mi nilimshtukia siku nyingi sana…

Na kama unaongelea UDART ina maana hujamshtukia leo… siku nyingi nyuma

Majaliwa huyu hafai kabisa, huwa hamwachii ofisa amalize kujibu swali, anagomba kwa ku feki feki tu..

Tuna bahati mbaya sana ya viongozi wabovu
 
Ngoja waje bavicha!
Mwaka mmoja wakati wazir wa TAMISEMI ni naibu wazir wizara fulani. Alitembelea nilipokuwa nafanyia kazi. Wananchi walikuwa wanalalamikia . Nikaanza kutiririka kadir nilivyolijua. Ile naanza tu akanikatisha na kusema ccm oyeeeeeeeee!
Mummy mwalimu namdharau hadi leo.
Pmv
 
Boka ww ni mmoja wao nini, inawezekana vipi umkabidhi mtu akujengee nyumba hajakamilisha vipengele vya ujenzi kama mlivyokubaliana, aje akukabidhi upoke… simpo logic tu… acha ubabaishaji wananchi wanahitaji huduma bora zenye viwango… tusiwafanye viongozi wetu wawe chanzo kupokea miradi isiyo na viwango… halafu kwa waliofuatilia TBC waliona Naibu Waziri alikiri mapungufu na kuahidi kufanyia kazi. Tuwaacheni viongozi wetu wafanye kazi jamani tunaongea sana kama vichaa
 

Boka ww ni mmoja wao nini, inawezekana vipi umkabidhi mtu akujengee nyumba hajakamilisha vipengele vya ujenzi kama mlivyokubaliana, aje akukabidhi upoke… simpo logic tu… acha ubabaishaji wananchi wanahitaji huduma bora zenye viwango… tusiwafanye viongozi wetu wawe chanzo kupokea miradi isiyo na viwango… halafu kwa waliofuatilia TBC waliona Naibu Waziri alikiri mapungufu na kuahidi kufanyia kazi. Tuwaacheni viongozi wetu wafanye kazi jamani tunaongea sana kama vichaa
 

Jamani huo ni upotoshaji tuliokuwa live tuliona PM akimhoji Naibu Waziri na alitoa majibu pia alimhoji meneja tanroads mkataba ulikuwa na taa au haukuwa na taa na alijibu ..hiyo ya kukatisha yatoka wapi..Samia, Mpango Majaliwa tuna imani nanyi KAZI IENDELEE MPAKA KIELEKEWEKE
 
Mbona hakumpa nafasi ajieleze? Kilichomfanya amkatishe ni nini? Hizo ni siasa za kise.nge sana. Unamshusha mwenzio ili wewe upande kisiasa. Udhalilishaji usiwe ngazi ya kupanda kisiasa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…