Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameviagiza vyuo vikuu vyote nchini, kufanya mapitio ya mitaala, ili iweze kuendana na mahitaji halisi ya sasa

Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa ameviagiza vyuo vikuu vyote nchini, kufanya mapitio ya mitaala yao, ili iweze kuendana na mahitaji halisi ya sasa ya soko la ajira.

View attachment 2296994
Yani anaviagiza vyuo badala ya serikali yake kutoa muongozo ni nini inataka vyuo vifanye!! Anazeeka huyuu!!?

Anaende akaongee na mama kwanza wapunguze kukopa
 
Hii kitu inatakiwa itokane na mpango mkakati wa muda mrefu na mfupi wa serikali. Kila shahada kabla ya kupitishwa lazima ieleze itafanyiwa mapitio baada ya muda gani. Mara nyingi ni kati ya miaka mitatu mpaka mitano.

Kwa hiyo, nadhani Mweshimiwa Waziri Mkuu anahimiza wahusika wafanye review kulingana na taratibu.
 
Mbatia aliwahi mwambia ndalichako kuhusu mitaala .. Mama etu akajibu pumba na akashindwa kufanya kitu kuhusu Hilo..
 
Nursing, Medicine, education, law, BBA, Accountant, civil engineer, electronics, mechanical.
Kwahy kwasababu hakuna ajira basi tufute kozi.

Kwanini solution isiwe kutengeneza ajira.??
 
Serikali haitakiwi kutoa muongozo vyuo vikuu vifanye nini katika masomo wanayofundisha.
Yani anaviagiza vyuo badala ya serikali yake kutoa muongozo ni nini inataka vyuo vifanye!! Anazeeka huyuu!!?

Anaende akaongee na mama kwanza wapunguze kukopa
 
Yani anaviagiza vyuo badala ya serikali yake kutoa muongozo ni nini inataka vyuo vifanye!! Anazeeka huyuu!!?

Anaende akaongee na mama kwanza wapunguze kukopa
Universities zina full autonomous kwenye masula ya nini kifundishwe na kipi kiachwe. Nafasi ya wadau ni kutoa maoni pekee.
 
Serikali haitakiwi kutoa muongozo vyuo vikuu vifanye nini katika masomo wanayofundisha.
Universities zina full autonomous kwenye masula ya nini kifundishwe na kipi kiachwe. Nafasi ya wadau ni kutoa maoni pekee.
Kila level ya elimu inaongozwa na mtaala.. haijalishi chuo au kindergatten.
 
Waziri Mkuu hii hoja angepeleka Bungeni wajadili kwa maslahi mapana ya Taifa kule walikua busy na Loliondo katoka Nje anatoa maagizo ya kisiasa tu ambayo hayabadili kitu chochote...
 
Hii kitu inatakiwa itokane na mpango mkakati wa muda mrefu na mfupi wa serikali. Kila shahada kabla ya kupitishwa lazima ieleze itafanyiwa mapitio baada ya muda gani. Mara nyingi ni kati ya miaka mitatu mpaka mitano.

Kwa hiyo, nadhani Mweshimiwa Waziri Mkuu anahimiza wahusika wafanye review kulingana na taratibu.
Kabisa..
Curriculum review nyingi zinafanyika after 5 years...ingawa zipo za miaka mitatu.
Na mara nyingi maboresho hayo yanafanyika yakitazama mambo mengi likiwemo suala la quality ya wahitimu na mazingira.
Sasa hili la Mkuu sijajua exactly anataka kitu gani?
 
Back
Top Bottom