Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Mwongo mkubwa!

UDART haijawahi kuwa na konda wa kuuza ticket kama daladala

Unabishana na uhalisia?

Wangeacha tuendelee kulipa nauli Kwa card
Na machine za kukagua ticket ziendelee kuwepo

Ila wangepiga vipi?
 
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu.

Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
Bado ombwe la u JPM linawausumbua
 
Vivuko ndio kabisaa
Hayo mabasi 100 yanafanya kazi barabara zipi aisee?? Abiria wanajazana kituoni mabasi hayaji halafu mnasema mabasi yaliyo barabarani ni 100,aah wapi?

Mwendokasi ubabaishaji ni mkubwa sana, mfumo wa kuonesha tiketi kwenye mashine umekufa zaidi ya miaka 2 sasa na hakuna hatua zinazochukuliwa.

Mabasi yanayofanya kazi ni machache na hayo machache madereva wanapaki wanavyotaka..utasikia derava anakunywa chai, mara anapumzika nk
 
Hiii kitu kwa kuitafakari nje ya box sahii ndio wakati wa kaz kabla ya mwendazake,,,, mean Kuna mengi yalikuwa nyumba yaliyo ficha madubwasha.
Mama suruhu anafanya suruhisho.
 
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu.

Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
Wanacheza na akili za watanzani. But wacha mwendo tuone itakuaje after 3 yrs
 
Ooh okay
Na lilikuwa linanuka harufu ya plastic inayoungua
Ukipanda zile gari unatakiwa mguu moja ndani mwingine nje.

Unategemea nini toka mwanzo wa safari unasikia harufu ya kitu kama kinaungua.
 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa leo amefanya ziara ya kushtukiza kituo cha mwendokasi eneo la gerezani na kukuta mfumo wa kusoma tiketi haufanyi kazi, mtendaji mkuu alisema mfumo haufanyi kazi baada ya kutokea mgogoro kati ya supplier na alieununua. Meneja huyo amesema mfumo mpya unajengwa na waziri mkuu kumuhoji inatumia miaka mingapi kukamilika?

Majaliwa amesema wanaibiwa mapato kwani wao wanatumia mtambo na wengine wanatumia mtambo mwingine na hawana namna ya ku-check.

Pia Meneja amehojiwa tangu aingie amenunua mabasi mangapi baada ya serikali kununua mabasi 140 huku mabasi yanayokadiriwa kuwa barabarani ni wastani wa 100.

Mtoa huduma ya mwendokasi aliagiza mabasi 70 ambayo yamekwama kuingia barabarani kutokana na mgogoro na waziri mkuu akasema anaenda kuyaona. Majaliwa amesema wananchi wanalalamika mabasi hayatoshi akitolea mfano Kimara watu wanaingilia dirishani na kuhoji mapato wanayokusanya wanapeleka wapi kama wanashindwa kununua mabasi.

Pia waziri mkuu amepita karakana ya Jangwani na sasa anaelekea Ubungo kuangalia mabasi yenye mgogoro

==========

UBUNGO: Kinachoendelea waziri mkuu anauliza hatua zinazoweza kuchukuliwa kwa mabasi yaliyokwama ambapo mtu TRA anasema sheria inamruhusu kamishna kuya-donate au kuyaharibu na waziri mkuu amesema hawezi kupewa Shabiby kwasababu hayamfai kwenda Dodoma kwani ni kwaajili ya barabara za mwendokasi na sasa anauliziwa mwanasheria

Pia waziri mkuu anawaambia forodha waendelee kufanya minada ya mizigo iliyokaa kupita kiasi mara kwa mara ili kusafisha nafasi ya kuagiza mizigo mingine na kuwataka wabadilike kwani baadhi ya wateja wanalalamika process zinachukua muda mrefu

Kassim Majaliwa anasema pesa zilizotumika zimekopwa world bank na zinalipwa na mabasi yameletwa na mjasiriamali laiki ameshindwa ku-comply na sheria na sheria zimechukua mkondo wake tangu 2018 na kutaka kesho wakae waamue

Majaliwa amesema serikali inao uwezo wa kununua mabasi lakini tatizo ni usimamizi na hawawezi kumsimamia msimamizi ambae hawezi na leo amemuweka pembeni mkurugenzi wa fedha na mwingine anamuachia Rais kwani yuko kwenye mamlaka yake.
1. Mzabuni wa kuendesha mradi alipatikanaje (taratibu)?

2. Contract term and conditions zilikuwaje?

3. Kama ameenda kinyume mkataba, taratibu zinataka hatua gani zichukuliwe?
 
Nilikuwa siamini kwamba kwenye kila analogusa Magufuli huwa ana haribu Ila kwenye Mwendokasi ndo sehemu niliyokuja kuamini kwa Mara ya kwanza!

Kwanza inabidi wote tujiulize mwendokasi ilianzia wapi?

Mradi wa mabasi ya mwendokasi ukianzishwa na kuasisiwa na Rais wa Awamu ya nne. Kwa Jinsi mradi ulivyokuwa umeandaliwa ulitakiwa kusimamiwa na kampuni binafsi na tangu mwanzo ulisimamiwa kwenye mfumo huo. Mradi huu ulikuwa chini ya Kampuni na Kisena na wakati unaanza kila kitu kilikuwa kinaendeshwa katika dunia ya kisasa. Ticket zilikatwa kielectronic na watu waliweka hadi kuwa na kadi ya kutumia mwezi mzima.

Alipokuja Magufuli kwanza alianza ku deal na kisena kwa sababu kisena hakuwa kwenye kundi la watu waliomuunga mkono kwenye uchaguzi wa mwaka 2015. Alimtesa kisena kumpa kesi za uhujumu uchumi na mkewe na baadae kumnyang’anya mradi na hatimaye akaondoa utaratibu wote mzuri uliokuwa umewekwa kwa ajiri ya kuendesha mradi.

Matokeo yake akawapa wanajeshi, na hapo ndo Tatizo lilipoanza. Mradi ulianza kuendeshwa kwa tabia za kiswahili na watu wakaanza kukata ticket kama daladala.

Mradi huu hadi kufikia sasa ulitakiwa uwe umeshaanza kujiendesha kwa faida Ila kwa roho mbaya ya magufuli na tabia zake za kuchukia matajiri ndo amefanya mradi ule uwe kituko na usifike popote.

Polee kisena. Buriani Mwendokasi.
Haya unayatoa wapi!? Seriously...

Sent from my Infinix X650 using JamiiForums mobile app
 
Kama tunashindwa kuendesha mradi mdogo huu wa mabasi na kila siku inakuwa shida mpaka PM anakuja site tutayaweza kweli haya madubwana kama SGR, Stieggler, ATCL nk?
 
Hayo mabasi 100 yanafanya kazi barabara zipi aisee?? Abiria wanajazana kituoni mabasi hayaji halafu mnasema mabasi yaliyo barabarani ni 100,aah wapi?

Mwendokasi ubabaishaji ni mkubwa sana, mfumo wa kuonesha tiketi kwenye mashine umekufa zaidi ya miaka 2 sasa na hakuna hatua zinazochukuliwa.

Mabasi yanayofanya kazi ni machache na hayo machache madereva wanapaki wanavyotaka..utasikia derava anakunywa chai, mara anapumzika nk
John aliuharibu mfumo wa mashine kwa kutoa tiketi akawapa TTCL nao wakafanya yao naona wakachemsha pale UDART na DART ni wizi mkubwa sana
 
Yaani, daah mradi kama wa kawaida tu kama huu, unatusumbua kiasi hiki? Sasa ATCL business ya ndege itakuwaje?
 
Hongera sana waziri mkuu kwa kuliona Hilo , maana abiria wanateseka sana , zichukuliwe hatua haraka
 
Waziri Mkuu hapo anaenda hii sijui mara ya tatu kila siku changamoto haziishi na anataka kutatua kwa makamera kazi ipo...Kuna kitu kimejificha hapo apeleke Timu ya ukaguzi tupate majibu ya kitaalamu sio haya ya kisiasa...
 
Waziri Mkuu hapo anaenda hii sijui mara ya tatu kila siku changamoto haziishi na anataka kutatua kwa makamera kazi ipo. Kuna kitu kimejificha hapo apeleke Timu ya ukaguzi tupate majibu ya kitaalamu sio haya ya kisiasa.
Huyu PM kwa makamera hadi anakera.
 
Back
Top Bottom