Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutumia takwimu ambazo siyo rasmi hajavunja Sheria?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kutumia takwimu ambazo siyo rasmi hajavunja Sheria?

Wewe umejuaje takwimu hizo alizotumia sio rasmi?

Kumsemea Kassim Majaliwa bila kuwa na uthibitisho wa unachokisema ni kosa kisheria
 
Huyu tumesha mzowea.

Kama aliweza kusema mgonjwa mahututi yuko ofisini ana chapa kazi, anashindwa nini kusema hayo aliyo sema?
 
Msiba wa kwanza wa kitaifa kwako ni wa Mkapa? Unakuja na porojo za kuvunja rekodi ya maombolezo uliishuhudia misiba ya Karume, Sokoine na Nyerere?
 
Msiba wa kwanza wa kitaifa kwako ni wa Mkapa? Unakuja na porojo za kuvunja rekodi ya maombolezo uliishuhudia misiba ya Karume, Sokoine na Nyerere?

Hutaki sasa?! Na mtakoma JPM hata akiwa amekufa bado anaishi katika mioyo ya Watanzania.
#tag JPM/Magufuli-Jeeeshiii! Uko hapo!!!
 
Wakuu,

Niwe mkweli, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa mmoja kati ya Wanasiasa waliokuwa wananivutia sana. Nilimuona mtu smart, asiyeweka mbele sana siasa za ujanja ujanja kama wale mawaziri Kangi Lugola na wengine wa aina hiyo. Lakini katika muda mfupi, kwangu amepoteza ile hali. Na hii yote ni kusema uongo.

Kwanza aliudanganya umma wa Watanzania kuwa kipenzi Rais wao, aliyekuwa akiuliziwa alipo alipodai ni mzima bukheri wa afya akifanya kazi zake ofisini. Siku chache baadaye iktangazwa kuwa kipenzi cha watu kimefariki, ikiwa ni siku chache tu baada ya tamko lake.

Ilipotangazwa kifo chake tuliambiwa alianza kuumwa tangu Machi 6! Jana Waziri Mkuu kadanganya tena. Ili kuonyesha kuwa msiba huu ni mkubwa duniani, eti watu bilioni 3.9 wameangalia shughuli zake duniani kote.

Wakuu, kwa mujibu wa vyanzo mbalimbali, hivi sasa dunia ina watu takribani bilioni 7.8. Bara la Afrika lina jumla ya watu bilioni 1.341, China ina watu bilioni 1.439, Ulaya nzima ina watu milioni 447.1 na Marekani ina watu milioni 331.

Ukipiga hesabu bila kuwa na Masters ya Chuo Kikuu, maana ya kauli ya Waziri Mkuu ni kuwa tukio la kuagwa kwa Rais Kipenzi cha Watanzania, kilitazamwa na watu wote wa Afrika, China, Ulaya na Marekani ukiwaweka pamoja!

Ha ha ha, sijui anachokitafuta Waziri Mkuu. Ingekuwa aliyesema ni Musiba, Makonda, Mashinji au Kafulila ningesema anatafuta teuzi.


~+Z�R
 
Kitu rasmi ndiyo kipi? Waziri Mkuu, kama ilivyo kwa Rais, ni kiongozi mwandamizi wa serikali. Kitu anachotamka ni rasmi na ye yote anaweza kukikariri kwamba Serikali imesema kadha wa kadha kutokana tu na matamshi hayo. Si hivyo kwa mtu baki tu kama wewe na mimi. Maadam kitu kimesemwa na Waziri Mkuu, basi hicho kitu ni rasmi kulingana na serikali ya Tanzania.
 
Hata kama amedanganya, tukiweka chuki pembeni ni kweli maziko ya jiwe yanafuatiliwa sana kwa sababu sio alikuwa anapendwa, ni kwamba watu hawakutegemea atakufa, alafu kwamba alikuwa mgonjwa wa moyo hilo limeniumiza hata mimi binafsi.
Mkuu, ni kweli watu wanafuatilia lakini siyo kwa kuangalia hivyo kwenye TV. Unajua hiyo idadi ni nusu ya popoulation ya dunia. Hivi kwa akili tu ya kawaida hiyo ni kweli. Hata Bongo tu sidhani kama nusu ya population (30 million) wanaaccess ya kufuatilia kwenye TV!!

I can imagine eti 150 million American, 40 million Germans, 07 Billion Chinese, 0.7 Billion Indians, 30 Million Britons ...... What a JOKE!!!

Anyway, tujaribu kucheck tu hizo statistics. TV zinazoonyesha mostly na ambazo ziko kwenye mtandao ni tatu, TBC, KTV na Azam. Hakuna major TV station kama CNN, Aljazeera, BBC, Sky News nk. zilizoonyesha zaidi ya kucover tu kama any news (about 5 min, maximum). Na hizo TV station 3 (TBC, KTV na Azam) ukiangalia sana sana waangaliaji kwa wakati moja live streaming ni 2 - 3K kwa kila channel. TV station probably zote za Southern Africa hazikuonyesha live zaidi ya SABC ambao walionyesha wakati tu Rais wao anaongea ..... Sasa kama Main stream TV hazikuonyesha hao viewers wanatok awapi ....!!?
 
Chadema wana wivu sana
IMG_20210324_095433.jpg
 
Back
Top Bottom