Executivesister
JF-Expert Member
- Aug 7, 2012
- 514
- 595
Aisee upo vizuri mkuu, umefanya justification hadi nimejiskia vizuri moyoni,... CCM hawawezi kuwa wakweli hata jiwe akifufuka Leo watasema ni kivuli chake.
Nikufahamishe kuwa hao bil. 3.9 hakuwahesabu yeye, yeye ameitumia idadi hiyo kumkweza marehemu na CCM tu hivyo hakuna cha kumuamini au kutomuamini.Kwani wewe mwenzetu bado unamwamini huyo jamaa? Haya huyu wanayezurula naye alikwambia yuko wapi? Si alikwambia huyu ndugu yetu ni mzima wa afya na anachapa kazi kulingana na mpango wake na hawezi kuzurula kariakoo wala magomeni. Ila sasa naona anazurula kwenye hayo maeneo bila kupenda.
Ha ha hahaaaa!!!!! Kazi kweli kweli.Maziko yanahusiana vipi na sheria ya takwimu, sheria husimama kama ilivyo haifuati jua au mvua, giza au mbaramwezi, msiba au harusi, sheria ni sheria.
Tujadili kuhusu sheria ya takwimu tu.
Tuliambiwa na huyu huyu kwamba huyu wanayezurula naye vichochoroni ni mzima wa afya. Kumbe ni uongo na uzandiki. Huyu ni mwongo na mzandiki, basi! Hatuwezi kumwamini huyu.
Acha porojo zisizokuwa na maana, zungumzia hoja iliyoko mezani.
Hebu tuambie, Je, huyo Waziri Mkuu hakusema uongo wa wazi wazi, tena akiwa ndani Msikitini??
Je, huyo Waziri Mkuu, hajavunja sheria ya takwimu kwa kutoa takwimu zisizo rasmi?
Huna hoja wewe, umejawa na mahaba na mihemko kwa huyo Waziri Mkuu.Acha chuki kwa Waziri Mkuu Majaliwa. Katika kuongoza nchi Hekima inahitajika si sheria tu. Jua hilo. Daudi kwa mfano wakati anamkimbia Sauli asimuue alisema Uongo kwa kutumia Hekima pale alipoulizwa na mmoja wa Makuhani mbona uko mwenyewe na wala hujabeba silaha yako?
Hakusema na mkimbia mfalme Sauli anataka kuondoa uhai wsngu. Bali alisema niko katika mission muhimu sana ya mfalme Sauli ambayo ilikuwa na uharaka kiasi ambacho sikutakiwa kujiandaa kwa lolote lile katika hii safari. Unamshangaa PM Majaliwa Majaliwa leo.
Nyie wa pambe nuksi mtamharibia sana huyu Mama tena vibayo mno. Dalili za mvua ni mawingu na manyunyu wakati jua bado linawaka.
Huna hoja wewe, umejawa na mahaba na mihemko kwa huyo Waziri Mkuu.
Wacha tukuache kama ulivyo.
Kwa sababu ya "chama chenye kuamini na kuabudu katika uongo"Yaani uongo umetamalaki utafikiri nchi inaongozwa na baba wa uongo!!!
Mkubwa muongo.
Mdogo muongo.
Mwanasiasa muongo.
Raia muongo.
Mtumishi wa Mungu muongo.
Muumini muongo.
Kiongozi muongo.
Anayeongozwa muongo.
Tumefikaje hapa!???
Amesha "cukondukii" wala usiwe na presha Mkuu.Mjinga wewe hebu ni ondikee hapa kwani umeamua kujitoa ufahamu na akili hadi kutumika na Mafisadi na Majizi ya Taifa hili kama taulo za usafi kwa wa Mama.
Sema ukweli basi. Huyu Majaliwa hakutudanganya watanzania kuhusu huyu marehemu?Wako watu wanamchukia PM tangu zamani na sababu moja wapo walimuona kaacha kuwa Muumini wa ile sera isiyokuwa rasm yai "Ni wa dini yetu."
Chuki hii inayoendelezwa kwake ni kwasababu yenye ndiye mwenyekiti wa kamati ya mazishi ya hayati JPM. Na kaongoza kamati hii kufanikiwa kufanya utaratibu wa Mazishi ya JPM ambayo yamemuheshimisha na kumpa umaarufu kuliko wakati wa uhai wake.
Kingine kinachowauzi hawa watu wa Mfumo ni wa dini yetu utaratibu ulioandaliwa na PM na timu yake ya mazishi umevifanya vyombo vya ulinzi na usalama hasa Jewii vipendwe na kuaminika zaidi na walalahoi. Na kusema kweli wanaona kuwa hata kama JPM katwaliwa matumaini yao yako kwa Majeshi. Ndio hiko kibwagizo maarufu zaidi sasa "Magu -Jeshi"
PM majaliwa, Mwigulu, Waziri wa Afya Mama Gwajima, Chalamila, Sabaya nk ni baadhi ya watu wanaopigwa vita kuwa hawafai na Rais wa awamu ya 6 anahimizwa aachane nao. Sasa tunajiuliza kwa nini? Hawa wanao wapiga vita ni wenye chuki binafsi au wametumwa na Rais wapige propoganda ili kumrahisishia kuwala vichwa.
Nikiangalia jina la mama PM ni kiangalia majina mengi wasio takiwa na misimamo yao katika kumcha Mungu napata mashaka makubwa. Mh Kabudi uliyekuwa unapenda kunukuu maneno ya Mungu ya Biblia jiaandae kisaikologia fitina ndio zimeanza kushika kasi.
Unamchukia PM kwa kumuambia Rais Mwinyi jr ukweli wa kwamba asisahau fadhila za Marehemu JPM. Kuna Mtanzania hajui kwamba huyu kufikia hicho cheo uko mkono wa JPM pia.
Wako watu sijui ni kwa kutumwa au kwa kujituma wenyewe kwa matakwa yao na chuki zao wanamfitinisha kwa Watanzania huyu Malkia bado kukiwa asubuhi na mapèma kabisa.
Ufalme ulio fitinika utaishi kwa mashaka na taabu hasa kama si kuanguka kabisa.
Sema ukweli basi. Huyu Majaliwa hakutudanganya watanzania kuhusu huyu marehemu?
Tangulia kunijibu ili na mimi nikujibu ndugu yangu. Tabu ya nini kusita kujibu wakati jibu ni Ndiyo au HapanaNa wewe sema ukweli hamumpigi vita PM kwa vile hakutimiza matarajio yenu ya kuendeleza mfumo wa ni wa dini yetu na mke wake anajina lenye ukakasi kwenu kwa mitazamo yenu ya wahafifhina wa kiimani.
Tangulia kunijibu ili na mimi nikujibu ndugu yangu. Tabu ya nini kusita kujibu wakati jibu ni Ndiyo au Hapana
Kumbuka ni mwanaccm na mwanaccm hatakiwi kubughudhiwa na sheria.Sheria ni msumeno hukata mbele na nyuma, TCRA inapaswa kumchukulia hatua kali ili liwe fundisho kwa viongozi wengine!