Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa: Rais Magufuli ni mzima na anachapa kazi. Wanataka atoke, atoke aende wapi? Kariakoo au Magomeni?

Naomba sana tena sana kwamba uvumi ulioenea kwamba Rais wetu, kioenzi cha watanzania ni mgonjwa usiwe kweli. Lakini ikidhihirika ni kweli na viongozi wakatuficha, na kwa kufanya hivyo tukakosa nafasi ya kumwombea Rais ili apone, tutawalumu sana viongozi hawa. Kwa kweli watakuwa hawajatutendea haki. Maana sasa tunashindwa kufanya maombi kwa kitu ambacho ni uvumi.
Kinachofanya ushindwe kufanya maombi ni nini? Kwani kama ukiomba tu hata bila kupewa taarifa kuna tatizo gani?
 
Kwani si unaruhusiwa kumuombea hata mtu mzima,sio lazima kumwombea mtu mpaka awe Mgonjwa.
 
Ajabu zaidi ni kwa nini mheshimiwa, anashindwa hata kupost clip kwa tv na mtandaoni kukanusha kuwa anaumwa. Ok yuko busy basi hata clip ya dakika 2 ya kukata mzizi wa fitna inamshinda?
Akiweka clip itazalisha maswali zaidi.Wanaona bora kupiga kimya hivihivi!
 
Hivi kuna anaemwombea kifo Rais Magufuli...?

Watu wanauliza tu aliko maana si kawaida yake na pia huyu ni Rais wa nchi kila kitu kumhusu (isipkuwa kuhusu mambo ya nyumba yake) is a public concern...
Mkuu, naona umegusia mambo mengi sana pamoja na lawama chungu mzima - kuwa muwazi unacho taka ni kipi hasa, je, hutaki Mzalendo JPM awe mzima wa afya au? Either way wewe binafsi na familia yako utafahidika nini? Labda tuanzie hapo.
 
Hata kama mtu unamchukia kikubwa lakini kumvumishia kifo ni ushetani kabisa. Tena Rais wa nchi? Tuwe waungwana.
 
Back
Top Bottom