Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

msovero

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2019
Posts
929
Reaction score
1,764
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
 
Matamko mengi ya hawa viongozi wa serikalini yanawalenga watoto wa masikini, wale wanaopewa mikopo ya chuo halafu wanatakiwa kulipa na riba juu, tena bila kujua lini watapata ajira, hizo ajira chache anazosema zipo kwa ajili ya watoto wao na wale wengine wenye connection nao.

Wengine tutaishia kutukana humu kila siku lakini ukweli ndio huo, ajira kwa ajili ya watoto wa masikini Tanzania hii hakuna, kama mzazi anauwezo akupe mtaji wa biashara hata ikiwa ndogo sio mbaya kuanzia, au kuungana vikundi kupewa mikopo, hii serikali imefikia mwisho wa kufikiri kwenye suala la ajira kuendelea kuilaumu ni kujipotezea muda.
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Kwani zile ajira milioni 8 zimeshapata watu zote?
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Kuna mambo hawa wanasiasa sijui wanatuchukuliaje vijana coz ni aibu mtu ambaye anapambana kwa namna yeyote ile kupata nafasi kisiasa then anasahau kuwa mfumo wezeshi kwa vijana kujifanyia shughuli zao za kujiingizia kipato ndo sababu ya yeye kukimbia taaluma yake.... Waziri mkuu anawezaje kupangia vijana cha kufanya ilhali yeye kakimbilia kwenye kula mema ya nchi kupitia njia kandamizi kwa wenzie.... Watuache na maisha yetu tunajua tunaishi vipi so hizo propaganda zao km ni itampendeza ajiuzuru nafasi yake ili akajiajili
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Hawa wazee bwana, wako serikaini miaka zaidi ya 20 wanakula mishahara mirefu na hawataki kutoka japo mitaji wanayo lakini utawasikia wanawambia vijana ambao hawana hata mitaji wajiajiri. Hapo hapo watoto wao wanapitia milango ya nyuma kuwachomeka kwenye ajira hawawambii wajiajiri.
 
Nimebrashi Viatu, Nimekata Nywele..., Nikaziba pancha.....

Ila nilichogundua...., bila buying power / watu kuwa na kipato cha kueleweka; wana wanaziba pancha wenyewe, wanajinyoa na viatu wanabrush wenyewe....

Hivi kweli li nchi hili lenye madini, maziwa, watalii na bandari na makusanyo ya kutosha wanashindwa ku-create system ya kupunguza wabangaizaji mitaani kwa kupata ajira ? Basi kama ni hivyo wana kazi gani huko walipo ? wote waje kitaa tubrashi viatu, tukate nywele na kuziba pancha...
 
Katika suala la ajira ( iwe ni kuajiriwa au kujiajiri) viongozi wengi wa Tanzania hawana ubunifu! Wanapiga blah blah tu!

Ukweli ni kwamba nafasi za hao viongozi madarakani ni suala la muda tu kwani wakosa ajira ( vipato) ndo watakao watoa madarakani.

Unatoa bilioni 700 kujenga daraja ( Busisi) wakati alternative ipo ( Panton) badala kuingiza fedha hiyo kwenye uzalishaji kilimo na viwanda .

Hatujitoshelezi kwa mafuta ya kula kwa 55% kwa mfano! Hizo ni ajira ngapi direct na indirect tukiwekeza hapo fedha kwenye kilimo na viwanda tukajitosheleza kwa angalau 85% ?! Bado kwenye sukari na simenti!

Acha watu wajiajiri kwenye kuwanyoa nywele ( salon) na kuwabrashia viatu ( shoe shiners) kwani ndiko uwezo wa viongozi wetu kufikiri ulipo!
 
Serikali imeshindwa ku create ajira, uwasumbue wawekezaji, uharibu sekta ya kilimo, sekta ya uvuvi, mfumo mzima wa biashara umeuua halafu utegemee watu wataajiriwa. Lazima uwe na akili za zezeta
Mkuu Tatizo Watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
Utafaidi matunda ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Hilo swala la ajira ni rahisi sana kujiajiri kuliko kusubiri serikali ikuajiri
Hayo Makampuni ya sekta binafsi walikua hawalipi kodi Ndio maana kazi imewashinda
Yaani wapiga dili lazima muumie maana mianya imeziba kabisa
 
W
Nimebrashi Viatu, Nimekata Nywele..., Nikaziba pancha.....

Ila nilichogundua...., bila buying power / watu kuwa na kipato cha kueleweka; wana wanaziba pancha wenyewe, wanajinyoa na viatu wanabrush wenyewe....

Hivi kweli li nchi hili lenye madini, maziwa, watalii na bandari na makusanyo ya kutosha wanashindwa ku-create system ya kupunguza wabangaizaji mitaani kwa kupata ajira ? Basi kama ni hivyo wana kazi gani huko walipo ? wote waje kitaa tubrashi viatu, tukate nywele na kuziba pancha...
Watanzania tunapenda kudeka kama mtoto wa mwisho
Mnatakiwa mjiongeze ajira chache
 
Mkuu Tatizo Watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
Utafaidi matunda ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Hilo swala la ajira ni rahisi sana kujiajiri kuliko kusubiri serikali ikuajiri
Hayo Makampuni ya sekta binafsi walikua hawalipi kodi Ndio maana kazi imewashinda
Yaani wapiga dili lazima muumie maana mianya imeziba kabisa
Watu mliopo kwenye mfumo hili swala mnalichukuliaga poa sana.... Hoja hapa sio kulipa kodi au kutii sheria bila shuruti..... Tupunguze siasa twende kwenye utekelezaji wa mazingira wezeshi kwa hawa tunaotaka wajiari
 
Takwimu za idadi ya watu Tanzania hadi mwaka 2020 58.5M na Kati ya hao watu, zaidi ya watu 30M wako kwenye kundi la wazalishaji mali.

0-14 years: 42.7% (male 12,632,772/female 12,369,115)
15-24 years: 20.39% (male 5,988,208/female 5,948,134)
25-54 years: 30.31% (male 8,903,629/female 8,844,180)
55-64 years: 3.52% (male 954,251/female 1,107,717)
65 years and over: 3.08% (male 747,934/female 1,056,905) (2020 est.)

Kwenye 30M people serikali imeajiri watu watu wasiozidi 1M ikiwa ni pamoja na serikali kuu, serikali za mitaa na agency za serikali.
Waliobaki wako kwenye ajira za sekta binafsi ikiwa ni pamoja na ajira za moja kwa moja toka kwa wawekezaji wazawa na wageni, kilimo na ufugaji kazi ambazo wengi wetu tunazidharau

Kuongeza mshahara ni jambo jema kwa ustawi wa wafanyakazi japo hakuna mshahara uliwahi mtosha mtu.
Nyongeza ya mshahara inategemea sana na uzalishaji mali, ongezeko la kudumu la mapato na vipaumbele katika uzalishaji mali.

Ofisi nyingi za serikali zinahusika na kutoa huduma zaidi ya kuzalisha mali na kutengeneza faida inayoonekana, kwa hiyo kuongeza mshahara sio zoezi la kuamka na kutamka tuu. Usishangae nyongeza ya mshahara kwa hawa watumishi wa umma ikailazimu serikali kutafta trilion2 au zaidi juu ya kile wanacholipwa sasa kila mwezi. Lazima kuwe na uhakika kwamba vyanzo vya mapato vya serikali vitaweza kulipa kiasi cha mshahara kwa wakati.

Serikali yetu ni serikali sikivu, sisi milioni moja tunaosupport wazalishaji mali tuendelee kupambana kwenye maofisi yetu katika kutoa huduma nzuri ili wateja wetu ambao wengi wao ndio wazalishaji mali waweze kuongeza
 
Sio kila kitu serikali ikufanyie
 
Kumbe wavulana tupo wengi hivoooo. Kale kamsemo ka wanawake ni wachache kumbe kauongo? Au data zako ndo za uongo😁

Back
Top Bottom