Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

Duuh kumbe ni nani anawajibika kuandaa sera na mazingira ya hao mnaotaka wajiari??
Basi subiri serikali huku ukiendelea kuumia
Mkuu kua mbunifu
Mimi sijasoma lakini ninayoaarifa kuliko wasomi
Kwa sasa mimi nalima mboga mboga na mahindi ya kuchoma kila wiki najaza pick up ya bidhaa naenda kuuza mjini
Nyie mnataka kukaa mjini shauri zenu
 
Matamko mengi ya hawa viongozi wa serikalini yanawalenga watoto wa masikini, wale wanaopewa mikopo ya chuo halafu wanatakiwa kulipa na riba juu, tena bila kujua lini watapata ajira, hizo ajira chache anazosema zipo kwa ajili ya watoto wao na wale wengine wenye connection nao.

Wengine tutaishia kutukana humu kila siku lakini ukweli ndio huo, ajira kwa ajili ya watoto wa masikini Tanzania hii hakuna, kama mzazi anauwezo akupe mtaji wa biashara hata ikiwa ndogo sio mbaya kuanzia, au kuungana vikundi kupewa mikopo, hii serikali imefikia mwisho wa kufikiri kwenye suala la ajira kuendelea kuilaumu ni kujipotezea muda.

kabisa yan, kuna mitoto ya viongozi ipo kwene ajira na ni failure wa mwisho, tunaona mavyeti yao kwene db lakin hatuwez fanya kitu sababu hata wakubwa kabisa wanawaogopa, ukiwaambia watu wa ccm aka mataga wanadhani unadanganya, kwakweli hali ni ngumu sana... jiulize kwanini kwene interview hata moja hujawah kukutana na watoto wa hawa wakubwa ila wengi wao wapo serikalini na wanakazi za maana, walipitia mlango upi ? kwanini mnaokutana kwene mainterview ni makapuku wale wale na bado kazi hampewi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
W

Watanzania tunapenda kudeka kama mtoto wa mwisho
Mnatakiwa mjiongeze ajira chache
Tunadeka wakati nchi inaendeshwa kwa jasho letu ?, tunatoa michango / kodi zetu (tena sio kutoa tunakamuliwa); alafu bado viongozi wanashindwa ku-create platform ya ku-absorb watu mitaani ?, kama issue ni kuwaambia tu wajiajiri basi tunatengeneza CD inayoimba vijana wajiajiri na sio kuweka watu watatue matatizo

Ni Impossible idea / ndoto za alinacha kudhani majority ya watu wana discipline na uwezo wa kuwa self employed...., unless otherwise employment hio uongezee na vibaka / waporaji
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Wanaulizia vile viwanda vyeti vipiii
 
Kumbe wavulana tupo wengi hivoooo. Kale kamsemo ka wanawake ni wachache kumbe kauongo? Au data zako ndo za uongo😁
Wewe ni mvulana au mwanaume😅😅😅😅 Data za kweli hizi Okwaaa
 
Mkuu wewe umejiajiri au umeajiriwa?
Nimejiajiri hapa Ruvu nalima mboga mboga na mahindi ya kuchoma kila wiki najaza pick up ya bidhaa naenda kuuza mjini
Natii sheria za nchi bila masharti
Nalipa kodi zote
Naishi kama sultani katika nchi yangu
 
Takwimu za idadi ya watu Tanzania hadi mwaka 2020 58.5M na Kati ya hao watu, zaidi ya watu 30M wako kwenye kundi la wazalishaji mali.

0-14 years: 42.7% (male 12,632,772/female 12,369,115)
15-24 years: 20.39% (male 5,988,208/female 5,948,134)
25-54 years: 30.31% (male 8,903,629/female 8,844,180)
55-64 years: 3.52% (male 954,251/female 1,107,717)
65 years and over: 3.08% (male 747,934/female 1,056,905) (2020 est.)

Kwenye 30M people serikali imeajiri watu watu wasiozidi 1M ikiwa ni pamoja na serikali kuu, serikali za mitaa na agency za serikali.
Waliobaki wako kwenye ajira za sekta binafsi ikiwa ni pamoja na ajira za moja kwa moja toka kwa wawekezaji wazawa na wageni, kilimo na ufugaji kazi ambazo wengi wetu tunazidharau

Kuongeza mshahara ni jambo jema kwa ustawi wa wafanyakazi japo hakuna mshahara uliwahi mtosha mtu.
Nyongeza ya mshahara inategemea sana na uzalishaji mali, ongezeko la kudumu la mapato na vipaumbele katika uzalishaji mali.

Ofisi nyingi za serikali zinahusika na kutoa huduma zaidi ya kuzalisha mali na kutengeneza faida inayoonekana, kwa hiyo kuongeza mshahara sio zoezi la kuamka na kutamka tuu. Usishangae nyongeza ya mshahara kwa hawa watumishi wa umma ikailazimu serikali kutafta trilion2 au zaidi juu ya kile wanacholipwa sasa kila mwezi. Lazima kuwe na uhakika kwamba vyanzo vya mapato vya serikali vitaweza kulipa kiasi cha mshahara kwa wakati.

Serikali yetu ni serikali sikivu, sisi milioni moja tunaosupport wazalishaji mali tuendelee kupambana kwenye maofisi yetu katika kutoa huduma nzuri ili wateja wetu ambao wengi wao ndio wazalishaji mali waweze kuongeza
Umeandika upumbavu.
 
Tunadeka wakati nchi inaendeshwa kwa jasho letu ?, tunatoa michango / kodi zetu (tena sio kutoa tunakamuliwa); alafu bado viongozi wanashindwa ku-create platform ya ku-absorb watu mitaani ?, kama issue ni kuwaambia tu wajiajiri basi tunatengeneza CD inayoimba vijana wajiajiri na sio kuweka watu watatue matatizo

Ni Impossible idea / ndoto za alinacha kudhani majority ya watu wana discipline na uwezo wa kuwa self employed...., unless otherwise employment hio uongezee na vibaka / waporaji
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Ukitaka kufaidi awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
LA sivyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
Mimi nipo Ruvu nalima mboga mboga na mahindi ya kuchoma kila wiki najaza pick up ya bidhaa naenda kuuza mjini
Nyie wajanja janja mnataka kukaa mjini tu
Waziri mkuu amesema ajira sio lazima kushika kalamu
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Huu ni ujinga.
 
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Ukitaka kufaidi awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
LA sivyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
Mimi nipo Ruvu nalima mboga mboga na mahindi ya kuchoma kila wiki najaza pick up ya bidhaa naenda kuuza mjini
Nyie wajanja janja mnataka kukaa mjini tu
Waziri mkuu amesema ajira sio lazima kushika kalamu
Sasa kulipa Kodi kunalinganaje na mada hii?Mada ni ajira.
 
Mkuu Tatizo Watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
Utafaidi matunda ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Hilo swala la ajira ni rahisi sana kujiajiri kuliko kusubiri serikali ikuajiri
Hayo Makampuni ya sekta binafsi walikua hawalipi kodi Ndio maana kazi imewashinda
Yaani wapiga dili lazima muumie maana mianya imeziba kabisa
Investment mpya ziko wapi? Brela kila siku wanarekodi makampuni yaliyokiri kushindwa kujiendesha. Ukiwa unaongea vitu sensitive upopoma wa CCM unauweka kando ongea Kama mtu mwenye fikra zako huru
 
Tatizo watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Ukitaka kufaidi awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
LA sivyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
Mimi nipo Ruvu nalima mboga mboga na mahindi ya kuchoma kila wiki najaza pick up ya bidhaa naenda kuuza mjini
Nyie wajanja janja mnataka kukaa mjini tu
Waziri mkuu amesema ajira sio lazima kushika kalamu
Hapa naona napoteza muda tu..., ngoja nikanyoe, nikabrush viatu pamoja na kuziba pancha..., ooh sorry wateja hakuna (sababu ya kutokuwa na mzungoko wa pesa unaotosha)..

Hawa watu wapo pale kutatua matatizo na ajira likiwa mojawapo sio kutuambia jambo ambalo kila mtu anajua (bali kutatua hilo tatizo ambalo kila mtu analijua)
 
tatizo lipo kwenye mitaala yetu inayowaandaa wasomi kutegemea ajira pekee, mitaala ibadilishwe ili iwatengeneze wahitimu wenye uwezo wa kuzalisha ufahamu mpya/elim mpya itakayowasaidia direct kujiajiri bila kuitegemea serikali.
 
Matamko mengi ya hawa viongozi wa serikalini yanawalenga watoto wa masikini, wale wanaopewa mikopo ya chuo halafu wanatakiwa kulipa na riba juu, tena bila kujua lini watapata ajira, hizo ajira chache anazosema zipo kwa ajili ya watoto wao na wale wengine wenye connection nao.

Wengine tutaishia kutukana humu kila siku lakini ukweli ndio huo, ajira kwa ajili ya watoto wa masikini Tanzania hii hakuna, kama mzazi anauwezo akupe mtaji wa biashara hata ikiwa ndogo sio mbaya kuanzia, au kuungana vikundi kupewa mikopo, hii serikali imefikia mwisho wa kufikiri kwenye suala la ajira kuendelea kuilaumu ni kujipotezea muda.
Well said.
 
Investment mpya ziko wapi? Brela kila siku wanarekodi makampuni yaliyokiri kushindwa kujiendesha. Ukiwa unaongea vitu sensitive upopoma wa CCM unauweka kando ongea Kama mtu mwenye fikra zako huru
Nchi hii ni tajiri sana
Tupo Uchumi wa kati
Ardhi Pana tukalime
 
Back
Top Bottom