Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Kama ndiyo Rais Mtarajiwa huyu halafu ana mawazo ya aina hii, basi tutarajie janga lingine baada ya 2025! Sasa kazi ya Serikali ni nini? Kukusanya kodi na kununulia ma V8 ya milioni 400!!

Badala ya kumshauri bosi wake kutengeneza sera za kuwasaidia hao vijana kujiajiri, anaongea kwa wepesi! Eti ku brush viatu!! Yeye mbona amekimbilia siasa? Si angeanza yeye kwanza ku brush hivyo viatu!! Kweli Shibe ni mbaya sana.
 
Kuna vijana waliojiajiri kama washehereshaji (MC) na wapikaji vyakula kwenye sherehe. Wameanza kuwekewa ADA kubwa kiasi kwamba hawatamudu ajira zao.

Mfumo wa kodi uliopo si rafiki. Hauchochei kujiajiri. Kuongoza vizuri ni pamoja na kuweka mazingira yanayochochea kujiajiri. Sio tu kusema mjiajiri.

It's easy to move around with a large number of expensive vehicles and ask the youth to employ themselves. After all that's your employment. And you need the subsequent taxes. How else will you maintain your perks?
 
Kama ndiyo Rais Mtarajiwa huyu halafu ana mawazo ya aina hii, basi tutarajie janga lingine baada ya 2025! Sasa kazi ya Serikali ni nini? Kukusanya kodi na kununulia ma V8 ya milioni 400!!

Badala ya kumshauri bosi wake kutengeneza sera za kuwasaidia hao vijana kujiajiri, anaongea kwa wepesi! Eti ku brush viatu!! Yeye mbona amekimbilia siasa? Si angeanza yeye kwanza ku brush hivyo viatu!! Kweli Shibe ni mbaya sana.
Mkuu Tatizo Watanzania tulizoea kuishi kiujanja ujanja Ndio maana tunaumia
Tii sheria bila shuruti
Lipa kodi
Utafaidi matunda ya awamu hii ya Rais mwema mwenye Moyo wa huruma na upendo kwa RAIA wake
Vinginevyo utaumia sana maana mianya ya wapiga dili imeziba kabisa
 
Una undugu na Bia yetu ?
 
Ni wazo zuri ila wangetengeneza mazingira ya ajira za mtandaoni pia sio kutaka vijana wote wa kitanzania kuzurura barabarani na mikanda miwili mikononi
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Huyu Mtu ndio maana Magu mwenyewe anamwendesha kama Zezeta
 
Mkuu wewe umejiajiri au umeajiriwa?
Atakwambia amejiajiri hata kama ameajiriwa ili tu kuhalalisha utetezi wake dhaifu wa kuisifia serikali na kunanga vijana wasio na ajira
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Ni kweli kabisa suala la ajira ni changamoto kubwa kwa nchi nyingi duniani hasa zinazoendelea kama yetu ya Tanzania. Lakini wito wa vijana kujiajiri unapaswa kuwa ni ule wenye kutekelezeka zaidi ya kutumia maneno matamu ya kisiasa.

Tunapowataka vijana wajiajiri wenyewe ni lazima serikali iweke mazingira na sera refiki kwa vijana kuweza kufanya hivyo. Yapo mambo kadha wa kadha ambapo yanaweza kuwapa motisha vijana wetu kutamani kujiajiri wenyewe ambayo ni lazima viongozi wetu waweze kuyaainisha vyema na hata kuyafanye vijana waone urahisi kuyaweka kwa vitendo na hata kuweza kupata vipato.

Awali ya yote, kijana anapaswa kuwa na wazo lake binafsi la biashara na hivyo kinachotakiwa ni kumjengea uwezo wa kuweza kulitimiza wazo hilo kwa vitendo. Hapo anapaswa kupata wataalamu wa kuweza kumfundisha stadi za kazi kupitia ujasiriamali ili aweze kupata uthubutu wa kutimiza ndoto zake za kujiajiri kwa vitendo.

Jambo la pili ni hitaji la mtaji na eneo la uhakika la kuweza kuendesha shughuli zake za ajira binafsi. Hili ni eneo ambalo serikali inapasa kuwa karibu na vijana. Tunatambua ugumu wa serikali kumuwezesha kijana mmoja mmoja, lkn kupitia vikundi inaweza kufungua makambi maalum yatakayohusisha makundi ya vijana na ajira mbalimbali. Vilevle iweze kuwasaidia kupata mitaji ya pamoja ya kuendesha shughuli zao mathalani kilimo cha umwagiliaji na ufugaji, pia na kuwawazesha kupata soko la uhakika kwa shughuli zao.

Nafikiri kuna haja ya kuwaonyesha njia ya kuweza kujiajiri wao wenyewe. Kwa kutambua wazo la biashara itakuwa ni namna sahihi ya kuweza kueapa msaada na hatimaye waweze kutimiza ndoto zao, na haya kwa hakika yangaliweza kuwa ni maeneo muhimu ya kuanzia, kama kweli kuna nia ya dhati ya kutaka vijana wetu wapate kujiajiri kwa mafanikio.
 
Kwa nn hawatengenezi mpango kazi wa kufufua viwanda?tuseme kila mkoa uwe na viwanda 5 vya kimkakati, hapo vijana watapata ajira lakini pia hata mpiga kiwi, machinga, muuza vocha, mama lishe, wauza matunda na mbogamboga, maziwa na mayai, wauza sabuni na vifaa vya usafi, stationaries, wote hao watakuwa na uhakika wa ajira,
Zile ndege zimeingiza ajira ngapi na faida kiasi gani?
Tungewekeza hizo hela kwenye viwanda vya kimkakati, eti leo hatuna mafuta ya kula,tunashindwa kulima alizeti na kujenga viwanda vya kukamua?
 
Back
Top Bottom