Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

Nimejiajiri hapa Ruvu nalima mboga mboga na mahindi ya kuchoma kila wiki najaza pick up ya bidhaa naenda kuuza mjini
Natii sheria za nchi bila masharti
Nalipa kodi zote
Naishi kama sultani katika nchi yangu
Nimejiajiri hapa Ruvu nalima mboga mboga na mahindi ya kuchoma kila wiki najaza pick up ya bidhaa naenda kuuza mjini
Natii sheria za nchi bila masharti
Nalipa kodi zote
Naishi kama sultani katika nchi yangu
mNimejiajiri hapa Ruvu nalima mboga mboga na mahindi ya kuchoma kila wiki najaza pick up ya bidhaa naenda kuuza mjini
Natii sheria za nchi bila masharti
Nalipa kodi zote
Naishi kama sultani katika nchi yangu
Mtaji uliuwokota uwani kwako
 
Katika suala la ajira ( iwe ni kuajiriwa au kujiajiri) viongozi wengi wa Tanzania hawana ubunifu! Wanapiga blah blah tu!

Ukweli ni kwamba nafasi za hao viongozi madarakani ni suala la muda tu kwani wakosa ajira ( vipato) ndo watakao watoa madarakani.

Unatoa bilioni 700 kujenga daraja ( Busisi) wakati alternative ipo ( Panton) badala kuingiza fedha hiyo kwenye uzalishaji kilimo na viwanda .

Hatujitoshelezi kwa mafuta ya kula kwa 55% kwa mfano! Hizo ni ajira ngapi direct na indirect tukiwekeza hapo fedha kwenye kilimo na viwanda tukajitosheleza kwa angalau 85% ?! Bado kwenye sukari na simenti!

Acha watu wajiajiri kwenye kuwanyoa nywele ( salon) na kuwabrashia viatu ( shoe shiners) kwani ndiko uwezo wa viongozi wetu kufikiri ulipo!
Wewe ni nani ata upingane na ilani ya chama yenye kurasa 300.Alisikika kada mmoja wa chama akifoka😂
 
Nimegundua sisi ni maboss tunaopelekeshwa na wafanyakazi wetu.'''''!!

Imagine walituomba kazi af leo wanatuambia hivi.....?? Kwanini maboss wenzangu tusiamke nakuwafuta kazi???
 
Kwa hiyo mnasomesha watu hadi ngazi ya degree ili waje wawe vinyozi, wabrashi viatu, waziba pancha, sijui waokota makopo, waosha magari, kusafisha akina mama kucha nk. nk. kazi ambazo hata ambaye hajaenda shule anaweza kufanya, seriously?
 
kabisa yan, kuna mitoto ya viongozi ipo kwene ajira na ni failure wa mwisho, tunaona mavyeti yao kwene db lakin hatuwez fanya kitu sababu hata wakubwa kabisa wanawaogopa, ukiwaambia watu wa ccm aka mataga wanadhani unadanganya, kwakweli hali ni ngumu sana... jiulize kwanini kwene interview hata moja hujawah kukutana na watoto wa hawa wakubwa ila wengi wao wapo serikalini na wanakazi za maana, walipitia mlango upi ? kwanini mnaokutana kwene mainterview ni makapuku wale wale na bado kazi hampewi [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
swali fikirishi sana
 
Kwa hiyo mnasomesha watu hadi ngazi ya degree ili waje wawe vinyozi, wabrashi viatu, waziba pancha, sijui waokota makopo, waosha magari, kusafisha akina mama kucha nk. nk. kazi ambazo hata ambaye hajaenda shule anaweza kufanya, seriously?
Tukisema hamna haja ya mtoto kusoma zaidi ya O'level tunaonekana vituko ila kweli is it worth it mtu kupoteza mamilioni kulipa ada ukiwa unajua mwisho huyo unaemlipia ada utandelea kumlisha tu sababu hana pa kwenda hana shughuli rasmi.
 
Tunadeka wakati nchi inaendeshwa kwa jasho letu ?, tunatoa michango / kodi zetu (tena sio kutoa tunakamuliwa); alafu bado viongozi wanashindwa ku-create platform ya ku-absorb watu mitaani ?, kama issue ni kuwaambia tu wajiajiri basi tunatengeneza CD inayoimba vijana wajiajiri na sio kuweka watu watatue matatizo

Ni Impossible idea / ndoto za alinacha kudhani majority ya watu wana discipline na uwezo wa kuwa self employed...., unless otherwise employment hio uongezee na vibaka / waporaji
ni kweli
 
Tukisema hamna haja ya mtoto kusoma zaidi ya O'level tunaonekana vituko ila kweli is it worth it mtu kupoteza mamilioni kulipa ada ukiwa unajua mwisho huyo unaemlipia ada utandelea kumlisha tu sababu hana pa kwenda hana shughuli rasmi.

me huwa nawaza sana... hela ni nyingi inakuwa imeondokaa
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Yeye ana mtaji lakini hataki kujiajiri
 
Matamko mengi ya hawa viongozi wa serikalini yanawalenga watoto wa masikini, wale wanaopewa mikopo ya chuo halafu wanatakiwa kulipa na riba juu, tena bila kujua lini watapata ajira, hizo ajira chache anazosema zipo kwa ajili ya watoto wao na wale wengine wenye connection nao.

Wengine tutaishia kutukana humu kila siku lakini ukweli ndio huo, ajira kwa ajili ya watoto wa masikini Tanzania hii hakuna, kama mzazi anauwezo akupe mtaji wa biashara hata ikiwa ndogo sio mbaya kuanzia, au kuungana vikundi kupewa mikopo, hii serikali imefikia mwisho wa kufikiri kwenye suala la ajira kuendelea kuilaumu ni kujipotezea muda.
Serikali ya hovyo kabisa
 
Ofcourse mzee. Mie nadhiri ni kuwa mtoto wangu baada ya form 4 namuingiza kwenye mapambano. By 30 atachagua kama kuoa au kuongeza elimu sasa afikie degree! Ila akiwa kwake na maisha yake yamesimama vizuri.

aisee noma sana hii system ya bongo ni nux, degree unaweza tafuta muda wowote ule
 
Vijana kukosa ajira ni janga na ni ticking time bomb. Boko Haram ilianzishwa na vijana wengi waliokosa ajira. Walikata tamaa na maisha. Hata Arab Spring moja ya sababu zake ilikuwa ni vijana kukosa ajira na kukata tamaa na maisha. Hali itakuwa ngumu sana kama mambo hayatabadilika.
 
Serikali imeshindwa ku create ajira, uwasumbue wawekezaji, uharibu sekta ya kilimo, sekta ya uvuvi, mfumo mzima wa biashara umeuua halafu utegemee watu wataajiriwa. Lazima uwe na akili za zezeta
Shida ni vetting kwenye utoaji wa lesseni ya udereva haikufanyika
 
Ukosefu wa ajira chanzo ni sera mbovu zilizoharibika kushindwa kutengeneza njia za fursa
 
Takwimu za idadi ya watu Tanzania hadi mwaka 2020 58.5M na Kati ya hao watu, zaidi ya watu 30M wako kwenye kundi la wazalishaji mali.

0-14 years: 42.7% (male 12,632,772/female 12,369,115)
15-24 years: 20.39% (male 5,988,208/female 5,948,134)
25-54 years: 30.31% (male 8,903,629/female 8,844,180)
55-64 years: 3.52% (male 954,251/female 1,107,717)
65 years and over: 3.08% (male 747,934/female 1,056,905) (2020 est.)

Kwenye 30M people serikali imeajiri watu watu wasiozidi 1M ikiwa ni pamoja na serikali kuu, serikali za mitaa na agency za serikali.
Waliobaki wako kwenye ajira za sekta binafsi ikiwa ni pamoja na ajira za moja kwa moja toka kwa wawekezaji wazawa na wageni, kilimo na ufugaji kazi ambazo wengi wetu tunazidharau

Kuongeza mshahara ni jambo jema kwa ustawi wa wafanyakazi japo hakuna mshahara uliwahi mtosha mtu.
Nyongeza ya mshahara inategemea sana na uzalishaji mali, ongezeko la kudumu la mapato na vipaumbele katika uzalishaji mali.

Ofisi nyingi za serikali zinahusika na kutoa huduma zaidi ya kuzalisha mali na kutengeneza faida inayoonekana, kwa hiyo kuongeza mshahara sio zoezi la kuamka na kutamka tuu. Usishangae nyongeza ya mshahara kwa hawa watumishi wa umma ikailazimu serikali kutafta trilion2 au zaidi juu ya kile wanacholipwa sasa kila mwezi. Lazima kuwe na uhakika kwamba vyanzo vya mapato vya serikali vitaweza kulipa kiasi cha mshahara kwa wakati.

Serikali yetu ni serikali sikivu, sisi milioni moja tunaosupport wazalishaji mali tuendelee kupambana kwenye maofisi yetu katika kutoa huduma nzuri ili wateja wetu ambao wengi wao ndio wazalishaji mali waweze kuongeza
Maisha yetu wanaume ni mafupi sana ... Gap linaanza kuonekana katika umri wa kuanzia miaka 50...tz ina maajuza wengi kuliko mashaibu..
 
Back
Top Bottom