Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

Waziri Mkuu Majaliwa: Ajira ni chache, vijana mjiajiri

Serikali imeshindwa ku create ajira, uwasumbue wawekezaji, uharibu sekta ya kilimo, sekta ya uvuvi, mfumo mzima wa biashara umeuua halafu utegemee watu wataajiriwa. Lazima uwe na akili za zezeta
Na lengo kubwa la kuwaambia vijana wajiajiri lengo ni kupata mapato na ushuru. Hakuna cha ziada zaidi ya hilo na ndio maana mazingira ya ukusanyaji mapato umeboreshwa ila wafabiashara wadogo mpaka leo hawana mazingira bora ya kufanya biashara.
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Huyu jamaa huwa namkubali sana,
Ila hii kauli yake ni utoporo mtupu,sasa kuziba pancha kutaweza kunifanya nijenge nyumba?
Nitasomesha mtoto chuo kikuu kwa 1.5Millioni kwa mwaka?nitanunua gari?
Kwanza atuoneshe watoto wake waliomaliza vyuo wamejiajiri kwenye nini?
 
Ni aibu kwa mtu anayekula na kulala bure, kazi yake kubwabwaja tu majukwaani akiniambia nijiajiri.

Sikusomea kuziba pancha mimi.

Anyway mitano tena.
 
Vijana kukosa ajira ni janga na ni ticking time bomb. Boko Haram ilianzishwa na vijana wengi waliokosa ajira. Walikata tamaa na maisha. Hata Arab Spring moja ya sababu zake ilikuwa ni vijana kukosa ajira na kukata tamaa na maisha. Hali itakuwa ngumu sana kama mambo hayatabadilika.
sorry man. hapo kwenye boko haram umelisha pumba. kuna sababu kubwa lakin si hiyo uliyoandika
 
Huyu jamaa huwa namkubali sana,
Ila hii kauli yake ni utoporo mtupu,sasa kuziba pancha kutaweza kunifanya nijenge nyumba?
Nitasomesha mtoto chuo kikuu kwa 1.5Millioni kwa mwaka?nitanunua gari?
Kwanza atuoneshe watoto wake waliomaliza vyuo wamejiajiri kwenye nini?
sorry man. hapo kwenye boko haram umelisha pumba. kuna sababu kubwa lakin si hiyo uliyoandika
Ndo mana Mimi siangaliagi habari za viongozi wetu, maana wana kera
 
Kama kujiajiri ni rahisi mbona yeye alibana mapaka kupita bila kupingwa!
 
trues say PM lakini, serikali haiwezi kukwepa lawama kwa kushindwa kutengeneza ajira.
 
Serikali imeshindwa ku create ajira, uwasumbue wawekezaji, uharibu sekta ya kilimo, sekta ya uvuvi, mfumo mzima wa biashara umeuua halafu utegemee watu wataajiriwa. Lazima uwe na akili za zezeta
Pia mfumo wetu wa elimu sio rafiki kwa ajira binafsi
 
Waziri mkuu ambaye pia anapigiwa upatu wa kuwania urais wa JMT ifikapo 2025 amewataka vijana kuacha kuitegemea serikali badala yake wajiajiri wenyewe.

"Ajira ni chache, muhimu tujiajiri wenyewe maana ajira sio tu ya kushika kalamu ofsini bali shughuli unayofanya kujiingizia kipato cha kujilisha na familia yako. Ukiziba pancha ukapata pesa ni ajira, ukibrashi viatu ni ajira, ukikata nywele za watu saloon ni ajira". Amesema majaliwa
Kwa nini hakuzungumza hivi wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu wa 2020?
 
Pia mfumo wetu wa elimu sio rafiki kwa ajira binafsi
Nafikiri sasa tuoneshwe ni kwa namna gani mfumo wetu wa elimu haumfanyi mhitimu ajiajiri kwa kulinganisha na mfumo mwingine usiokuwa kwenye nadharia tu.
 
kwa nini wazazi hawashtuki. kama unaona ajira hakuna msomeshe mtoto wako la kwanza mpaka la saba baada ya hapo pesa za kumsomesha form 1 na 2 na 3 na 4 na 5 na 6 na chuo unamkusanyia yote pamoja na nauli na ya chakula yote unamtunzia unampa akimaliza la saba unamwambia hizi pesa anzia maisha atakuja kuwa tajiri kuliko kupoteza pesa mpaka chuo anatoka na karatasi ya digrii anaambiwa akajiajiri hana hata pesa anaenda kufanya kazi kituo cha mafuta
 
Eti huyu naye apewe ridhaa ya kupeperusha bendera na kuiwakilisha tanzania nje ya nchi...??

Huyu asie mbunifu kwa changamoto ya ajira atawezaje kutuvusha kwenye swala la uchumi wa nchi...??
 
Ni mpuuzi tuu huyo kama mwendazake,yameharibu mazingira ya kujiajiri afu anapayuka hovyo..yeye na watoto wake wamejiajiri wapi
 
Eti huyu naye apewe ridhaa ya kupeperusha bendera na kuiwakilisha tanzania nje ya nchi...??

Huyu asie mbunifu kwa changamoto ya ajira atawezaje kutuvusha kwenye swala la uchumi wa nchi...??
Hawezi kuwa Rais, huyu hachaguliki labda kama apitishwe kwa mabavu ya dola kama alivyofanya mwendazake
 
Ni mpuuzi tuu huyo kama mwendazake,yameharibu mazingira ya kujiajiri afu anapayuka hovyo..yeye na watoto wake wamejiajiri wapi
Hata huo uwaziri sema ni basi tu ila ilitakiwa lipigwe chini lionyeshe mfano wa kujiajiri kwa vijana
 
Back
Top Bottom