Waziri Mkuu Majaliwa amezindua safari ya meli ya MV Mbeya II itakayotoa huduma katika Ziwa Nyasa nchini na nchi jirani za Msumbuji na Malawi

Waziri Mkuu Majaliwa amezindua safari ya meli ya MV Mbeya II itakayotoa huduma katika Ziwa Nyasa nchini na nchi jirani za Msumbuji na Malawi

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amezindua usafiri wa meli ya MV. Mbeya II, itakayokua ikifanya safari zake kutoka Mbeya kwenda Nyasa mkoani Ruvuma kupitia ziwa Nyasa pamoja.

Pia amekagua ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Kilomita 66 kutoka Mbinga kwenda Mbamba Bay huku akisema nia ya serikali ni kupanua shughuli za kiuchumi kwa wananchi kwa kuboresha miundombinu mbalimbali.

Screenshot_20210106_112117.jpg

Chanzo: ITV
 
Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa amezindua usafiri wa meli ya MV.Mbeya II, itakayokua ikifanya safari zake kutoka Mbeya kwenda Nyasa mkoani Ruvuma kupitia ziwa Nyasa pamoja.

Pia amekagua ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Kilomita 66 kutoka Mbinga kwenda Mbamba Bay huku akisema nia ya serikali ni kupanua shughuli za kiuchumi kwa wananchi kwa kuboresha miundombinu mbalimbali.

View attachment 1669523

View attachment 1669522

Chanzo: ITV
Mh mbona kama MV Kasa iliyopakwa rangi upya?!!
 
acha maneno mkuu kitu kipya hicho
Napongeza juhudi zinazofanyika katika kuendeleza secta ya usafirishaji nchini. Ila isiwe kama ile iliyoletwa kwa mbwembwe ifanye safari za Dar - Bagamoyo sijui MV gani vile (jina limenitoka) yakagundulika madudu kibao
 
hv ule mzozo wa "wanyassa" kutaka kijimwambafai ziwa lote uliishia wapi??🤔
Wagomvi ni wamalawi, na asili ya ugomvi ni kwamba wale mabeberu UK na German walivyogawana sehemu za kupiga pesa mkataba waliosaini ni kwamba Germani achukue ziwa lote,Uk achukua ardhi tu kupanda juu milimani sasa kwa sheria sasa ya kimataifa inatambua mpaka upo baharini JIULIZE NANI YUPO SAHIHI MALAWI WANA MKATABA WALIOACHIWA NA BEBERU GERMAN NA TANZANIA TUNAFUATA SHERIA YA KIMATAIFA
 
Kyela, mkuu. Daa umenikumbusha Kyela yaani kunaga watoto wakali ile mbaya. Inabidi nipange siku nifanye utalii wa ndani Kyela.
Karibu sana, ukifika Mbeya mjini hapa nijulishe.
Nilikuwa nikimshangaa huyo jamaa aliuliza hiyo MV inafanya safari za Mbeya mjini mpaka wapi?!
 
Wagomvi ni wamalawi, na asili ya ugomvi ni kwamba wale mabeberu UK na German walivyogawana sehemu za kupiga pesa mkataba waliosaini ni kwamba Germani achukue ziwa lote,Uk achukua ardhi tu kupanda juu milimani sasa kwa sheria sasa ya kimataifa inatambua mpaka upo baharini JIULIZE NANI YUPO SAHIHI MALAWI WANA MKATABA WALIOACHIWA NA BEBERU GERMAN NA TANZANIA TUNAFUATA SHERIA YA KIMATAIFA
Sheria za kimataifa ndizo zitakazofuatwa.
 
Lissu hataki vitu.
Ataki vitu vya maendeleo,anataka uhuru wa watu.
mfano-serikali iruhusu ndoa za jinsia moja kwa watuwake,
-watu wapewe ruhusa ya kumtukana Rais wa nchi.
-Raia waruhusiwe kutorosha rasilimali za nchi watakavyo n,k
 
Tatizo la Lissu ni moja tu amekosa akili ya uchumi ila akili ya sheria anayo.
 
Tatizo la Lissu ni moja tu amekosa akili ya uchumi ila akili ya sheria anayo.
Kwenye kampeni zake kashindwa kabisa kuchambua uchumi kabaki na kelele za kumshambulia JPM(personal attack)badala ya kujikita kwenye ataifanya nini Tanzania akiwa Rais.
 
Wamejiandaaje kuilinda dhidi ya tishio la magaidi wa mtwara & msumbiji
 
Back
Top Bottom