Waziri Mkuu, Majaliwa amuwakilisha Rais Samia kumjulia hali Lowassa

Waziri Mkuu, Majaliwa amuwakilisha Rais Samia kumjulia hali Lowassa

Attachments

  • 20230116_142143.jpg
    20230116_142143.jpg
    26.5 KB · Views: 3
MAJALIWA AMUWAKILISHA RAIS SAMIA KUMJULIA HALI LOWASSA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemwakilisha Dkt. Samia Suluhu Hassan kumjulia hali Waziri Mkuu Mstaafu, Mhe. Edward Ngoyai Lowassa anayeendelea na matibabu Afrika ya Kusini.

Akizungumza na wanafamilia kwa niaba ya Mheshimiwa Rais Samia, Waziri Mkuu amewasilisha salaam za pole kutoka kwa Mheshimiwa Rais na kusema Mheshimiwa Rais anafuatilia hali ya Mheshimiwa Lowassa kwa ukaribu na anamuombea afya njema.

Waziri Mkuu ametoa salamu hizo leo (Jumatano, Desemba 28, 2022) jijini Johannesburg, Afrika Kusini ambako alienda kumjulia hali Mheshimiwa Lowassa.

Kwa upande wake, Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu, Mama Regina Lowassa amemshukuru Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo amekuwa karibu na wanafamilia na namna ambavyo anafuatilia matibabu ya mpendwa wao.

Naye mtoto mkubwa wa Mheshimiwa Lowassa na Mbunge wa Monduli, Bw. Fredrick Lowassa amewashukuru Watanzania kwa maombi yao ya kumtakia afya njema baba yao.

View attachment 2461149
Wapi Chadema na Mbowe wake?

Mlimpiga helaowassa kisha mmemtupa kushoto?
 
Ya kweli hayo?
Yule kaka katika imsni hamuelewi tuuu.....never ever amtose .....labda aharibu mwenyewe .....imani ina nguvu sana upande ule......kuna mtoto kigogo yupo humu anapuyanga mitandao mambo vita hamas na israel kutwa kucha.....anavumiliwa sababu hiyo hiyo la sivyo waziri .....sidhani kana ni maafili mema anayofanya....la atoke serikalini....kuwa active kwenye issue hiyo vita maana ina tafsiri potofu udini....misimamo wa setikali vs msimamo bimafsi na kuwa radicals...
 
Back
Top Bottom