Waziri Mkuu Majaliwa ashangaa kukuta wanafunzi wanakaa chini Mkuranga, atoa wiki mbili madawati yapatikane!

Waziri Mkuu Majaliwa ashangaa kukuta wanafunzi wanakaa chini Mkuranga, atoa wiki mbili madawati yapatikane!

Kweli makada wa CCM Mpya na UVCCM waliopewa vyeo vya Mtendaji wa Kata, Afisa tarafa, DED, DC na RC wanaonesha kukosa weledi wapo kisiasa zaidi badala ya kuangalia mahitaji ya maendeleo ya watu katika maeneo yao.

Kazi yao kubwa ni kusifia Flyovers, Dreamliner/ bombardier n.k zilizopo Dar es Salaam ambazo hazitatui mahitaji ya wananchi ktk maeneo yao.


FAHAMU MAJUKUMU YA WATEULE WA RAIS:
Rais Magufuli Afanya Kikao Cha Kazi Na RC, RAS, DC, DAS Na DED Wote


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Magufuli amewataka Wakuu wa Mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji kujenga ushirikiano na uhusiano mzuri baina yao ili kurahisisha utekelezaji wa majukumu yao.

Mhe. Rais Magufuli ametoa maelekezo hayo leo tarehe 16 Mei, 2019 katika kikao cha kazi kati yake na viongozi hao kilichofanyika Ikulu Jijini Dar es Salaam, na kuhudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, baadhi ya Mawaziri na Makatibu Wakuu.

Mhe. Rais Magufuli amewaonya baadhi ya viongozi hao ambao wamekuwa na migogoro baina yao na hivyo kuathiri utendaji kazi na amesema endapo vitendo hivyo vitaendelea hatasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja kuwaondoa katika nyadhifa zao.

Pamoja na kuwataka kuwa waadilifu na wenye nidhamu kazini, Mhe. Rais Magufuli amewataka kusimamia kwa ukaribu miradi yote ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, kusimamia ukusanyaji wa mapato yote ya Serikali, kusimamia ulinzi na usalama na kusimamia rasimali za umma.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi hao kwa kazi nzuri wanazozifanya zinazowezesha mipango na mikakati mbalimbali ya Serikali kwenda vizuri na amewahakikishia kuwa anawaamini na anatarajia wataendelea kufanya vizuri katika utekelezaji wa majukumu yao.

“Ni matumaini yangu baada ya kikao hiki cha leo sote tutakwenda kwa mwelekeo mzuri zaidi, nendeni mkachape kazi, mimi ndiye niliyewaweka kwenye nafasi hizo na ninafuatilia utendaji kazi wa kila mmoja wenu, sitarajii kusikia tena hamuelewani miongoni mwenu” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Katika kikao hicho Mhe. Rais Magufuli amesikiliza kero na changamoto mbalimbali ambazo zinawakabili viongozi hao katika maeneo yao ya kazi na ameahidi kwenda kuzishughulikia.


Kabla ya kuanza kwa kikao hicho, Mhe. Rais Magufuli amemuapisha Mhe. Juma Zuberi Homera kuwa Mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Mhe. Homera pia amekula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela.

Baada ya kikao hicho, viongozi hao wamekula futari na Mhe. Rais Magufuli aliyoiandaa kwa ajili yao.


Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

16 Mei, 2019
Source: Rais Magufuli Afanya Kikao Cha Kazi Na RC, RAS, DC, DAS Na DED Wote


Nashukuru sana.. 😊 mimi sipo serikalini wala kwa chama chochote.. ila namufatilia Magufuli.. tangu zamani alivyo kikazi..
naona ipo vizuri.. vizuri kuwaita.. wamuone wenyewe.. naamini iliwanyanyua kiutendaji wale wanaojua nini kinatakiwa kwa kazi zao.. migogoro ya viongozi hao.. kama ipo sana.. inakuwa sehemu ya wengi.. kutotambulika kiurahisi wale wasio na uwezo wa kazi walizopewa.. na mfano wa mashule hayo kukosa madawati.. mwalimu mkuu.. afisa elimu etc.. yaani wao inakuwaje.. hawajui kuripoti au wakishindwa kwa wa juu yao.. je wana mwingine juu ya wote kuwataarifu.. muhimu wajuwe waatweza kosa kazi.. wasaini mengine mapya.. yaongezwe na survey ifanyike kujua mengi.. wawe anonymous waweke labda wilaya na mkoa au vyote..
 
Wanajifanya hawajui? Sehemu nyingi tuu madawati hayatoshi, Kuna baadhi ya wilaya wanatoa taarifa za uongo kuwa wanamadawati mpaka ya akiba wakati Hali ni mbaya watoto hawana viti, wakurugenzi ma DC wanajua
Sahihi kabisa, wakurugenzi na wakuu wa wilaya wanaficha ukweli wa upungufu wa madawati, hata pale shule inapotembelewa na kiongozi wa juu basi anapelekwa ktk yale madarasa yenye utoshelevu wa madawati huku wakihakikisha kbs hafiki kwenye madarasa yenye upungufu.
 
Waziri mkuu mh Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza katika moja ya shule za wilaya ya mkuranga na kukuta wanafunzi wa msingi na sekondari wamekaa chini.

Mh Majaliwa ameshangazwa na hali hiyo na kutu muda wa wiki mbili madawati yapatikane na watoto wote wakae.

Majaliwa amesema wilaya hiyo ina viwanda zaidi ya 70 sasa inakuwaje DC na DED wanashindwa kutumia fedha za CSR kununulia madawati.

Chanzo: ITV habari!
Mwezi jana meko so alipita hapo akachangia madawati
 
Magufuli na CCM Mpya wameshindwa kuunda mfumo utakao mpa mrejesho mtendaji kata, afisa tarafa, DED, DC na RC kiasi hata watendaji hao hawajui kinachoendelea / mahitaji ktk maeneo yao zaidi ya kujua wapi kuna mkutano wa chama cha upinzani wawatie ndani watu wa upinzani kuwafurahisha kisiasa wakubwa waliopo Dodoma na Dar esSalaam.

Kama kungekuwa na mfumo thabiti masuala ya madawati, shule, hospitali za wilaya, vituo vya afya, barabara za vijijini, mabwawa ya Umwagiliaji, masoko ya mazao n.k vingepatiwa ufumbuzi ngazi hizo za mikoa / wilaya / Halmashauri na siyo kitaifa na waziri Mkuu au Rais.
 
Hongera Mh. waziri mkuu hili zoezi lingefaa liwe nchi nzima DED, mkuu wa wiliya na afisa elimu ambao wanafunzi wao wanakaa chini au kukosa vyoo ni vyema wakatumbuliwa tu maana ni aibu. Tunahitaji viongozo wabunifu na wenye maono ili Taifa lisonge mbele. Haipendezi kabisa Taifa limeingia uchumi wa kati halafu baadhi ya viongozi wanashindwa kufanya mageuzi katika utendaji wao.
 
wangeacha kununua ndege wakatuachia fastjet yetu kila mtoto angekuwa na dawati lake.
Hakuna kitu kinanikera kama ile biashara ya kuunga juhudi,halafu uchaguzi unarudiwa tena. HIZO PESA ZILIKUWA ZINATOSHA KUJENGA MADARASA NA KUTENGENEZA MADAWATI NCHI NZIMA. Kama kituo Cha afya kinagarimu mil 400 tu,ni vyumba vingapi vya MADARASA vingejengwa huko Tabora,Lindi,Simiyu,Mara etc? Namalizia kwa kusema yeyote aliyeshiriki kwenye hiyo biashara kwa namna moja au nyingine, ni mpumbavu yeye na kizazi chake halafu alaaniwe milele na milele.
 
Nini madawati shule nyingi hazina walimu
Walimu waliyopo hawana nyumba za kuishi, hawajapadishwa madaraja, hawajapewa nyongeza ya mshahara ya mwaka.
Nao wanatakiwa washangilie midege, maflyover, madaraja ya baharini kutoka Upanga kwenda Masaki.
 
Nini madawati shule nyingi hazina walimu
Walimu waliyopo hawana nyumba za kuishi, hawajapadishwa madaraja, hawajapewa nyongeza ya mshahara ya mwaka.
Nao wanatakiwa washangilie midege, maflyover, madaraja ya baharini kutoka Upanga kwenda Masaki.
 
Waziri mkuu mh Majaliwa amefanya ziara ya kushtukiza katika moja ya shule za wilaya ya mkuranga na kukuta wanafunzi wa msingi na sekondari wamekaa chini.

Mh Majaliwa ameshangazwa na hali hiyo na kutu muda wa wiki mbili madawati yapatikane na watoto wote wakae.

Majaliwa amesema wilaya hiyo ina viwanda zaidi ya 70 sasa inakuwaje DC na DED wanashindwa kutumia fedha za CSR kununulia madawati.

Chanzo: ITV habari!
Teh! Siri kali ya viwanda
 
Kumbe kuna wanafunzi wanakaa chini hata baada ya miaka 5 ya majigambo na kelele nyingi za awamu hii?!

DC & DED lazima wapigwe chini, hiyo kazi ilitakiwa kuisha tokea 2017.. Wenyewe wanakaa tu ofisini.
 
Back
Top Bottom