Marco Polo
JF-Expert Member
- Jan 16, 2014
- 11,786
- 18,562
Ile tume aliyeiunda ya kuungua kwa soko la kariakoo hivi ilitoaga majibu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wanazidi kugawana keki ya taifa,Kwa mujibu wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Tume maalum ya wajumbe 21 ambao wamebobea kwenye masuala ya ujenzi kuchunguza chanzo cha tukio la ajali ya jengo lililoanguka Kariakoo, pamoja na kufahamu ubora na uimara wa majengo yote yaliyoko Kariakoo. Tukio hilo lilisababisha maafa makubwa, na Tume hiyo imepewa maagizo mazito, huku ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Brigedia Jenerali Hosea Ndagala.
PIA SOMA: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Kamati ya Uchunguzi kuporomoka kwa jengo Kariakoo yazinduliwa Nov 21, 2024
Halafu majibu yake wakayatia kapuniNI mwendo wa Tume mpaka kieleweke. Lowasa aliunda Tume kama hii ya kuporomoka ghorofa
Kuna jamaa 10 walikuwa wanasafiri kwa ngalawa..maji yakaanza kuingia ndani ya ngalawa yao - walichofanya wakaunda tume ili ichunguze maji hayo yanaingiaje ingiaje kwa ngakawa yao.NI mwendo wa Tume mpaka kieleweke. Lowasa aliunda Tume kama hii ya kuporomoka ghorofa
Ana nywele nyingi nyeusi, Yani mvi zinamuogopa PM wetu,Akili ni Nywele. Waziri Mkuu ana nywele nyingi sana. Hongera kwake.
Hivi hata kuangalia tu kwa macho kunahitaji TUME..., badala ya kuangalia Jengo hili kuanguka wangeangalia kwanini majengo kama haya hatarishi yanaendelea kuongezeka kama Uyoga.
By the way kuna uhitaji wa kuanzisha Tume ya kuangalia Tume zinazoanzishwa kama huwa zina Tija
Hakuna haja ya tume, aliyechimba pembeni ndiye aliyesababisha janga. Unganisha na mkandarasi aliyesimamia jengo.
Atoe taarifa ya tume Ile ya mapendekezo ya wafanya biashara Kariakoo kwanzaKwa mujibu wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Tume maalum ya wajumbe 21 ambao wamebobea kwenye masuala ya ujenzi kuchunguza chanzo cha tukio la ajali ya jengo lililoanguka Kariakoo, pamoja na kufahamu ubora na uimara wa majengo yote yaliyoko Kariakoo. Tukio hilo lilisababisha maafa makubwa, na Tume hiyo imepewa maagizo mazito, huku ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Brigedia Jenerali Hosea Ndagala.
PIA SOMA: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Kamati ya Uchunguzi kuporomoka kwa jengo Kariakoo yazinduliwa Nov 21, 2024
Ni mmoja wa Waziribmkuu anayejali cheo kuliko heshima yake.Waziri mkuu zigo lote la nnya huwa kwake, maagizo yake hayatekelezwagi ata
Uhuni tuIle Tume iliyoundwa na Waziri mkuu kipindi kile(Edward Lowasa) baada ya ajali ya chang'ombe village inn ripoti yake ilifanyiwa kazi? Vp ripoti ya Ile Tume ya Manispaa ya ilala ?
Ni upuuzi mtupu kuunda tume ya kuchunguza Jambo Kisha ripoti yake haifanyiwi kazi..
Ni matumizi mabaya ya fedha za umma.