Waziri Mkuu Majaliwa azindua Tume Maalum ya Wajumbe 21 kuchunguza ajali ya Jengo Kariakoo
Wachunguze nini na uzembe wao serikali wanatoa vibali hovyo… hiyo tume wachunguze kwanini hakuna vifaa vya uokozi na huku wanapeana posho kila kukicha?
 
Kwa mujibu wa maelekezo ya Rais Dkt. Samia, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezindua Tume maalum ya wajumbe 21 ambao wamebobea kwenye masuala ya ujenzi kuchunguza chanzo cha tukio la ajali ya jengo lililoanguka Kariakoo, pamoja na kufahamu ubora na uimara wa majengo yote yaliyoko Kariakoo. Tukio hilo lilisababisha maafa makubwa, na Tume hiyo imepewa maagizo mazito, huku ikiongozwa na Mkurugenzi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge na Uratibu, Brigedia Jenerali Hosea Ndagala.

PIA SOMA: Live Updates Kuporomoka kwa Ghorofa Kariakoo Nov 16: Kamati ya Uchunguzi kuporomoka kwa jengo Kariakoo yazinduliwa Nov 21, 2024
Mwongooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooooo Jiwe yuko ofisini anachapa kazi
 
Mbona sioni jina la mmiliki wa jengo, mkandarasi aliye lijenga na msimamizi.
Mmiliki na mkandarasi wangekua na majibu yote.
Sasa wanaitwa watu kutoka Kigoma, Rukwa na Ruvuma
 
TUMEZOEA KUUNDA TUME

Hizi tume zinakuja kabisa na dalili za kupeana moyo.

Kweli, ma engn wahusika tumewakamata, watafikishwa mahakamn.

Mmiliki utasikia amekamatwa kama kama ajafanikiwa kukimbia.

Utaona picha vid wakipelekwa mahakaman.

Mwisho, amtuelezi wanahukumiwaje.

Nchi za Rwanda ujinga kama huu hata mmiliki anakua nusu kaputi mpaka watoe maiti zote.

Ma engn wanawekwa sehemu wakitoka kupelekwa kwenye hukumu. Wale walio nje awarudii tena.

Hizi mamboo mwisho tunaona wahusika wanabadilishwa vitengo ama kuachiliwa, inaumiza sana hawa ndugu wa marehemuu.

Tunaomba wah mawaziri husika hawa watu wakamatwe wapewe adhabu kubwa ya mfano kwa wale wenzao wa ofisin hawatarudia tenaa. Na wengine wakipelekwa kusimamia wanakimbia kabisa.

Tunaomba tume itoe haki ktkt hili.

Bila hivi mjianada e kuzika sana sana na specia
l hire zidumu milele.
 
Kama hakujiuzuru kwenye ajali ya Precision sidhani kama atajiuzuru milele

Ndege inaanguka mita 100 toka airport na haijalipuka na bado watu hawaokolewi wanakufa tena baada ya jinga kujisifu lilivunja mlango wa ndege maji yakaingia??

Achana na mambo ya kujiuzuru wala uwajibikaji nchi hii. Tuishi tu kama maparachichi kwenye tenga, siku ikifika tunajifia tu
 
Hata mimi najiuliza hivi hapo limeporomoka ghorofa moja, je lingekuwa tetemeko la kuangusha ghorofa 10 hivi? Kama kule Ukraine au Gaza yanavyoangushwa majengo!?

Ajali inatokea saa2 asubuhi, uokoaji rasmi unatokea saa7 mchana. Hii kamati yake ya maafa haina nyenzo? Mbona inachangiwaga sana.

NAUNGA MKONO HOJA
 
90% au zaidi ya majengo yote ya Kariakoo ni substandard.
 
kwanza watwambie wataufungua lini ule mtaa maana wameufunga na biashara zmesmama.
 
Unaunda tume halafu kiongozi unamuweka mwajiriwa unategemea nini? Wenyeviti wa tume wekeni watu wasiofungamana na upande wowote ili pasiwe na uoga wowote.
 
Back
Top Bottom