Waziri mkuu mh Majaliwa ametangaza hitimisho la maombolezo ya msiba wa hayati Magufuli na kwamba kuanzia kesho wananchi warejee katika shughuli za kawaida na kuchapa kazi.
Haki ya nani! Hii nchi kwa sasa haina PM! Kwa hiyo anataka kutuaminisha wakati wote wa hizo siku 21, watu walikuwa wanalala tu ndani kwa maombolezo! Na walikuwa hawafanyi kazi!
Kwanza hakuwa hata na sababu ya kuongea chochote maana kila mtu alikuwa anafahamu kuhusu jambo hilo.
Labda izo ni salamu za kuruhusiwa kwa wale ma-mc na wenye kumiliki kumbi za masherehe kwani kazi zao zilisimamakama ni hao sawa lakini kwa sie machinga zilikuwa hazituhusu izo siku za maombolezo
Huyo hana maana kabisa, hawezi kuaminika tena. Anaweza akalidanganya taifa kwamba rais yupo na anachapa kazi kumbe mtu yuko mortuary. Bure kabisa huyu bwana.