Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu

Waziri Mkuu Majaliwa: Serikali imekamilisha malipo ya ununuzi wa ndege mpya tatu

Narudia tena Serikali hii imejaa waongo tena waongo wakubwa sana. Majaliwa anadai malipo yameshakamilika lakini hajaweka ushahidi hadharani kuonyesha kukamilika kwa malipo hayo. Sasa kutaka ushahidi huo uwekwe hadharani ni politics? 😳😳
Wafute tu hiyo nafasi ya CAG kwani haina umuhimu wowote kama ripoti yake inadharauliwa kiasi hiki. Haina thamani tena kwa hawa wahuni ndani ya Serikali.

CAG ameshakupa investment costs za ndege, model of ATCL financing kati yake na serikali. Kama upo interested na business viability ya ungetaka kuona financial statements ya shirika na supplementary informations za kwenye notes how exactly does their expenses breakdown na kama zinaweza punguzwa. Their business strategy etc kuona shirika linaenda mbele vipi.

Ata ingekuwa malipo yote bado hayajakamilika there are penalties for stepping out of a contract.

Soma hapo juu hilo shirika lilipigwa fine ya karibu $43 million just for stepping out of an agreement kabla hata ndege azijatengenezwa. Iwe hatua za ndege kukamilika.
 
Haya maneno yangekua matamu zaidi kama yangeitangulia report ya CAG! Kazi kubwa ya serikali ni usalama wa watu mali zao, biashara serikali haiwezi! Ukifanya biashara Wewe serikali kwenye ushindani itabidi uuwe kina fast jet ili utawale soko! Shirika la ndege lingeweza kupata wawekezaji, serikali ikapata chake, maisha yanaenda!
Sidhani kama Serikali ndio inafanya biashara, ATCL kama moja ya makampuni ya Serikali ndio wenye jukumu hilo. CAG kazi yake ndio hiyo ya kukagua mahesabu na amefanya sehemu yake, sasa tuwape ATCL nafasi waje watoe maelezo kitu ambacho nina hakika watafanya.

Kuhusu shirika la ndege kupata wawekezaji, mimi nauona mwelekeo huo kwenye mashirika yote ya Serikali yakilitumia vema soko la hisa kupata wawekezaji wa kutosha kutoka ndani na nje, ila kwa wakati huu bado tuko kwenye uwekezaji ambapo pesa inayotumika sasa inaonekana kwenye hasara. Tuwe na mtazamo chanya tujenge chetu.
 
Only in Tanzania kuna this level of incompetence. Pamoja na madudu yote, bado wang'ang'ana na ndege.
Kweli CCM ni Serikali ya Vichaa kwa 100%....!!!
Ni sawa na jitu moja pumbaf mifuko ya suruali imetoboka lakini bado lina lazimisha kuweka pesa mifuko hiyohiyo iliyo toboka......What a nonsense idea???
Huu ni uvivu wa kufikiri wa kiwango cha juu sana.......!! Hivi Biashara au uwekezaji ni katika ndege tu???
 
Again it is better to pay penalty for cancellation instead of buying few more loss making planes. Kama WASINGEKURUPUKA Taifa lisingeingia kwenye huu Mkenge.

Ata ingekuwa malipo yote bado hayajakamilika there are penalties for stepping out of a contract.

Soma hapo juu hilo shirika lilipigwa fine ya karibu $43 million just for stepping out of an agreement kabla hata ndege azijatengenezwa. Iwe hatua za ndege kukamilika.
 
Serikali inapenda ndege kuliko kuboresha hospitali kwa ajili ya matibabu ya wanyonge.
Na hizo hospitali na vituo vya afya, basi viwe kamili kabisa basi, vikiwa na vifaa tiba, wafanyakazi na madawa ya kutosha,
nyumba za madaktari nk.na sio kuishia tu na ' mapagale'.. ikiwezekana pesa ya ndege 2 zilizobaki kati ya 5 tulizoambiwa, zisaidie na kuelekezwa kwenye kuboresha mapungufu mengi ktk sekta hizi ya afya kabla ya kufikiria tu kuongeza ndege zifike 5....ni ushauri tu msirushe ngumi ...Tz ni yetu wote na KAZI IENDELEE..
 
Ingekuwa kodi mnalipa wenyewe ambao mnataka hizo ndege zinazoleta hasara basi asingelalmika mtu. Shida ni hela zetu sote alafu tunaona zatumika kwenye mahali si pa vipaumbele kwa mtanzajia wa leo.
Alafu tambua kila kitu kina faida na hasara ila lazima kupimwe hasara zake kwa jana leo na kesho..
Ukija na fact kuwa zina faida yake basi tambua hasara zipo pia . Shida inakuja pale hasara inapo zidi faida kwa muda usiokoma.
Uwazi upo hatukujipanga na swala la hiyo mindege vema alafu hapo hapo tunaacha mambo ya msingi yenye uhitaji kwa mtanzania

Hujui hata unachoongea.

Hasara isiyo na kikomo kwenye nini, kwani hizondegezimeanza kazi lini mbakaunasema hasara isiyo na kikomo au unalishwa tu maneno hasara hasara.
Hujui kwamba dunia nzima mashirika ya ndege yamepata hasara,kwasababu ya corona? husikilizi vyombo vya habari au unaishi porini.

Serikali ndio kwanza imekamilisha malipo ya ndege nyingine mbili utaziona.

Unasema mambo gani ya msingi yenye mahitaji kwa mtanzania unataka ununuliwe ugali?.

Inchi inamahitajimengi kila mkoa na hayataisha.

Kupanga nikuchagua,kama we huoni umuimu wandege kunawatu wanaona umuhimu na wanazipanda kilasiku na baadhiyenu mnapanda pia.

Kila mtu akitaja kipaumbele chake eti kwasababu analipa kodi nchi si itakuwa kama geto la wahuni.
Tulizeni akili mtaelewatu.
Ingekuwa kodi mnalipa wenyewe ambao mnataka hizo ndege zinazoleta hasara basi asingelalmika mtu. Shida ni hela zetu sote alafu tunaona zatumika kwenye mahali si pa vipaumbele kwa mtanzajia wa leo.
Alafu tambua kila kitu kina faida na hasara ila lazima kupimwe hasara zake kwa jana leo na kesho..
Ukija na fact kuwa zina faida yake basi tambua hasara zipo pia . Shida inakuja pale hasara inapo zidi faida kwa muda usiokoma.
Uwazi upo hatukujipanga na swala la hiyo mindege vema alafu hapo hapo tunaacha mambo ya msingi yenye uhitaji kwa mt
 
Ushamba nao ni mzigo, yaani kujaza ma vitu bado tunaona ni aina ya ufahari hata kama hayana tija

Ni zile akili zetu wasukuma kuwa na mifugo mingi lkn maisha yetu tunayajua wenyewe, kulala kwenye ngozi, mwendo wa ugali wa mtama (ukula) na asubuhi viazi (mandoro/ Manumbu) bila kuwa na mpangilio wa mlo kamili pamoja na utajiri wote tulio nao

Naona hapa ni quantity Vs Quality

Mmeambiwa yanakula hasara hayo subirini mdogo mdogo mpaka yaanze kutengeneza faida pia mkizingatia hiyo biashara kwa sasa ina changamoto za kidunia kutokana na COVID-19 na kuna watu wamebashiri itachukua muda mrefu kwa airlines industry kurudi vizuri labda hata miaka mitatu ijayo

Hivi haiwezekani ku cancel hizo order na pesa ikatumika kwenye madawa na maji plus miundo mbinu na ndege zilizopo zibembelezwe mpaka zikae sawa na pia hata biashara ya utalii inaweza chukua muda kurudi na yote sababu ni COVID-19 kwa hiyo hata usafiri wa anga kuchagiza sekta ya utalii nalo litachukua muda kutokana na mazingira ya kidunia kwa sasa

Kibaya zaidi uamuzi wa kununua ndege unafanywa Ikulu bila kuwa na uwiano na BUSINESS PLAN ya ATCL (kama ipo) kisa ni ndege za serikali. Zitakaa tu kusubiri kukodishwa kwa ATCL watakapohitaji. Sijui serikali inawezaje kufanya biashara ya aircraft leasing?

Hakika tatizo lililoua ATC hapo awali sasa linatengenezwa upya kwa nguvu moja tena kwa gharama ya aina yake.
 
kama unaona Majaliwa hafai ingia wewe
Sio mimi naona hafai bali kwa mujibu wa katiba yetu kitendo alichofanya cha kudanganya uma ni kwamba hafai.Suala la kwamba Majaliwa hafai sio maoni yangu binafsi bali ni kwa mujibu wa Katiba yetu.Umeelewa?
 
Sidhani kama Serikali ndio inafanya biashara, ATCL kama moja ya makampuni ya Serikali ndio wenye jukumu hilo. CAG kazi yake ndio hiyo ya kukagua mahesabu na amefanya sehemu yake, sasa tuwape ATCL nafasi waje watoe maelezo kitu ambacho nina hakika watafanya.

Kuhusu shirika la ndege kupata wawekezaji, mimi nauona mwelekeo huo kwenye mashirika yote ya Serikali yakilitumia vema soko la hisa kupata wawekezaji wa kutosha kutoka ndani na nje, ila kwa wakati huu bado tuko kwenye uwekezaji ambapo pesa inayotumika sasa inaonekana kwenye hasara. Tuwe na mtazamo chanya tujenge chetu.
Serikali haiwezi kuendesha shirika lolote liwe TANESCO au ATCL! Sababu ya msingi ni kwamba siyo jukumu lake la msingi! Serikali ni baba haiwezekani refa naye acheze!
 
Ndegeee tena??

Kama zilinunuliwa enzi hizo sawa ...
 
Ndege ni chanzo cha mapato......
faida itakayopatikana hapo itaendelea kusaidia kuhudumia sekta ya afya infinitely.....
kwako kuwa na akili ya kutafakari ni jambo la anasa!!??
Chanzo cha mapato wakati CAG ametangaza hapa juzi kwamba zinaingiza hasara yangu mwaka 2016?!
 
CAG kafanya kazi yake inatosha, Acha kazi iendelee hiyo hasara ni zaidi ya umuhimu wa kuendelea kuliboresha Shirika letu. Kongole Serikali.
 
Nyerere mwenyewe alianzisha shirika la ndege la ATC hakuwa mjinga.

Hakuna anaekataa kuazisha ila nimesema zilizopo tuziendeleze kwanza na zinavyo anza leta faida na pia kupata routes za uhakika za ndani na nje ndo tuanze kuona kama kuna demand ya kuongeza tena ndege ndo tuanze kununua kidogo kidogo

Tuna ndege tayari bado hazijakaa sawa kwa routes za ndani na nje na zinazalisha hasara bado afu unasema hata baba wa Taifa alianzisha Atcl sasa yapi kilipelekea kufa kwa hiyo Atcl aliyo ianzisha?? Mbona ET/Ethiopian Airline ipo muda tu na wanazidi kukua na shirika letu linaanzishwa likafa, likafufuliwa likafa tena na kama tunafufua lazima tuangalie mapungufu yetu sio kukurupuka na kuchoma pesa zote kwa kitu kinachotaka umakini na utaratibu na kwenda nacho mdogo mdogo
 
Serikali haiwezi kuendesha shirika lolote liwe TANESCO au ATCL! Sababu ya msingi ni kwamba siyo jukumu lake la msingi! Serikali ni baba haiwezekani refa naye acheze!
Hayo mashirika yote na makampuni unayoyalalamikia hayapaswi kuendeshwa na Serikali ndio, na ndio maana yanatakiwa kutoa gawio baada ya kuendeshwa kwa faida... Na huo ndio mwelekeo wa kibiashara. Naona bado unahusisha haya mashirika na upataji wa ruzuku.
 
kaka mimi naiwakilisha Serikali yako ya CCM inavyokuhukumu kuhusu mafao!! mimi ni mjumbe tu hauawi - nilichokisema ndicho Serikali yako ina ki-implement, Ni muda sasa wa kusimama na kusema Serikali ya CCM uonevu huu sasa basi.
Hapo sawa, Sasa Ni Wakati TUCTA wasimame na kuongea Kuhusu FAO LA KUJITOA
 
Back
Top Bottom