Waziri Mkuu Majaliwa, Wahudumu wa Ndege ya Precision Air wanasema Wao ndiyo Walifungua Mlango. Huyu Muokoaji ‘Majaliwa’ aliufungua upi?

Hakuna waliotoka na uhasidi dhidi ya dogo, hao madada wametoa story yao kama walivyotoa wengine. Wamehojiwa nao wakasema kilichotokea wala hawakumtaja dogo na wala hawakujiita wao ni mashujaa.
Wamesema kilichotokea na walichofanya. Sasa raia baada ya kusikia upande wa hao wahudumu ndipo wakaanza kuwa na mashaka ya story na ushujaa wa dogo.
Ila mwisho wa siku, Mungu akikufungulia milango ya riziki anakufungulia kweli kweli na pasipo kutaraji. Ndivyo mambo yanavyokuwa. Hata nyerere hakupigania uhuru peke yake, wapo wengi nyuma ambao hata hatujawahi kuwasikia.
 
Ametukana yeye kwanza. Nika mjibu utumbo wake.

Ila wewe moderators wana kulea sanaaaaa. Hizo account zako kama 3 hivi wange zipiga ban ya miaka 2. Akili itakaa sawa tu
Genius apigwe BAN na Fool ubakishwe?
 
Ndiyo maana mwaka 2013 Rais Paul Kagame wa Rwanda alimwambia Mpuuzi Mmoja ( sasa Mstaafu ) wa nchi niliyoisahau kwa sasa wakiwa Mkutanoni nchini Ethiopia kuwa anaongoza Maiti tu.
Yeye anaongoza mikaratusi!?
 
Kinachokusumbua ni wivu tu mtumainie Mungu akukutanishe na bahati itakayo badili maisha yako, pia zidisha juhudi wivu haujengi zaidi ya kuendelea kuwa mchawi
 
Kwa sababu yoyote ile, Majaliwa amepata umaarufu. Umaarufu huu umeambatana na pesa. Yawezekana ni pesa nyingi ambazo hakuwahi kufikiriria kuzipata kipindi hiki.
Amepata umaarufu uliomfikisha bungeni. Anatembezwa kama mtu wa hadhi fulani ya juu kiasi. Anatembezwa kwenye magari mazuri.
Atahitaji ushauri nasaha wa jinsi ya kuyaendeya maisha yake baada ya pirika pirika hizi kumalizika. Atakuta maisha halisi tafauti na haya ya ushujaa. Kwenye ajira yake mpya atakutana na shughuli za kila siku za jeshi la zima moto.
Ashauriwe vizuri ili aweze kuendana na ukweli wa mambo. Atakuwa mfanyakazi wa kawaida ambaye ataanza ngazi za chini.
 
Hao wanaoanzisha hizo Nyuzi za Kumjadili Muokoaji Majaliwa Jackson huwa wanakulazimisha usome hizo Nyuzi zao?

Juha mkubwa Wewe.
unadhani nitahangaika kukujibu kama unavyojibu hapa, wewe endelea kupoteza muda hunipati hapo ila acha wivu muacheni majaliwa afaidi bahati yake.
 
Njia za mafanikio zilizofunguliwa kwa kubumbabumba huwa hazifiki mbali. Nina uhakika, wahudumu wakitoka hadharani na kusimulia tukio lenyewe majaliwa shujaa atatafuta pa kuficha uso wake.
wala hawawezi kutoka tena maana tayari jambo limeshaisha, na kwa kukutoa hofu huyo kijana hajafanya udanganyifu wala hajaomba hicho alichopewa so hakuna ufanano hapo.
 
Ishu walioshiriki ni wengi kwann awe yy peke yake?? Alizimia, haya aliokolewa na nani??
yeye ametajwa zaidi kwani ndiye aliehusika kufungua mlango na pia kuzungumza na rubani japo kwa ishara, tukirudi kwenye mada hiyo ni bahati ya majaliwa hao wengine haikuwa bahati yao mwacheni apande V8 kidogo ni wakati wake.
 
Bahati ya Mwenzio usiilalie Mlango wazi,.Watakuja Panya Road wachukue kila kitu.Kubalini matokeo.
 
Huyu Mungu ni kichekesho au? Watu 19 wafe waache yatima, wazazi bila msaada ili majaliwa ainuliwe?!!!
Cha ajabu kipi hapo ronaldo enzi zake kasababisha huzuni kwa timu pinzani ili ainuliwe yeye tu,halikadhalika messi
 
Msiowahi kuuona mlango wa ndege live ukifungwa au kufunguliwa ndo mnaweza kuamini Kasia linaweza kufungua mlango wa ndege kwa nje
 
Mlango wa gari tu ukijifunga lazima uvunje kioo au upitishe kichuma kubetua kile kilock .sasa jiulize wa ndege unaufunguaje bila mtu ndani mlango ambayo upo compact hewa isiingie. Tutumieni tu common sense
 
Mlango wa gari tu ukijifunga lazima uvunje kioo au upitishe kichuma kubetua kile kilock .sasa jiulize wa ndege unaufunguaje bila mtu ndani mlango ambayo upo compact hewa isiingie. Tutumieni tu common sense
Pale Ccm Imetupanga Mchana Kweupe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…