Waziri Mkuu Majaliwa, Wahudumu wa Ndege ya Precision Air wanasema Wao ndiyo Walifungua Mlango. Huyu Muokoaji ‘Majaliwa’ aliufungua upi?

Waziri Mkuu Majaliwa, Wahudumu wa Ndege ya Precision Air wanasema Wao ndiyo Walifungua Mlango. Huyu Muokoaji ‘Majaliwa’ aliufungua upi?

Alafu yule ni dogo tu kumsaidia namna ile kwa kwa kile alifanya mbna ni haki yake tu!
alivyozidi kupatapata vizawadi threads zikawa zinazdi kuongezeka!
Taifa limegubikwa na wivu mkuu, yaani watu bila aibu wanaumia kijana mdogo yule kusaidiwa. Sugu kaniudhi kweli, yaan hawazi yule kijana mpaka alizirai na kidogo apoteze maisha, yeye anawaza mlango. Nyambafu kabisa, hao wahudumu kwanini hawakufungua na mlango wa mbele?? Si wanakuwaga WAWILI mmoja mbele mwingine nyuma?? Majaliwa alisema ALIWAKUTA wanapambana kufungua mlango, yeye akaupiga na Kasia, manake maji yalilokisha mlango, Kwa kupigwa na majaliwa ndo ukafunguka
 
"Sisi ndiyo tulifungua Mlango wa Ndege kisha tukawaona Wavuvi na Mitumbwi yao wanakuja na kuanza Kushirikiana nao katika Kuokoa Abiria na baadae nasi pia Kuokolewa" Wahudumu wa Ndege ya Precision Air iliyotumbukia tarehe 6 Novemba Ziwa Victoria Bukoba Mkoani Kagera.

"Huyu Kijana tena Wajina wangu Majaliwa Jackson ni Shujaa kweli na lazima tumpe Asante kwani Yeye ndiyo alienda ilipo Ndege na kwa Kutumia Makasia aliyokuwa nayo akafungua Mlango wa Ndege na peke yake Kuokoa Abiria wote" Waziri Mkuu Majaliwa Kassim Majaliwa.

Kazi ipo hakyanani.
Lakini uongo si uko kwenye damu? Bila uongo mambo yake hayaendi!
 
Majliwa,talk of the town.Ngoja na mimi mtoto wangu wa kiume nimpe jina la Majaliwa,maana naona lina neema flani hivi...
 
Ww unae sema ali sema yeye ndie alie fungua mlango. Mtaje jina na weka picha. Ali hojiwa na media gani? Weka video. Coz majina ya Marehemu na majeruhi wa ajali yote yapo hapa ktk uzi mmoja hapa JF na huyo mhudumu hajawahi jitokeza.
Hao hapo
Screenshot_20221114-221028.jpg
 
Hatujui yote. Lakini kule kushiriki uokoaji, na kuchapwa na mpira, kudondokea majini, kunywa maji, kupoteza fahamu, Naye kuokolewa na wengine, akazinduka akiwa hospitali. Mungu akaona bidii yake, AKAMWINUA.
 
Hao wadada wamepata mabasha wao wa kuwaondoa stress ndio leo wanakuja na story hii, walikuwa wapi toka day one kusema hayo!?
Walikuwa wanangojea na Wewe umalize Kubahashiwa na hawa ( hao ) Mabasha uliowataja hapa Kwanza kama Wao.
 
Sawa. Ila issue ya kuokoa tusidanganywe eti ni wao. Mara Wahudumu. Mara Majaliwa, mara sijui Eng, gani. Uongo ni mwingi.
Wavuvi ndio waliokoa, hata yeye pia si kaokolewa na wenzake. Lakini kwamba watu wote kawaokoa yeye, ni uongo wa waziri mkuu.
 
Watu wanawivu wa kipumbavu sana hii nchi badala ya kujadili uzembe wa vyombo vya uokoaji wanajadili issue ya Majaliwa na mlango.
Kwani kuna Mtu amekuzuia Wewe kutokujadili huo Uzembe wa Vyombo vya Uokoaji?

Huna Akili.
 
Wavuvi ndio waliokoa, hata yeye pia si kaokolewa na wenzake. Lakini kwamba watu wote kawaokoa yeye, ni uongo wa waziri mkuu.
Ila na wahudumu kudai wao ndio walifungua mlango ni uongo! Mara majaliwa. Mara Eng. Victor. Hapa watu watulie ripoti ije. Tujue mlango uli vunjwa au ulifunguliwa kawaida.
 
Back
Top Bottom