ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa akizungunza na wakazi wa Igunga, Tabora.

"Tumeendelea kuimarisha sekta ya elimu, Muheshimiwa mbunge ulisema unahitaji VETA tumeleta VETA, hizi VETA tumezijenga ili wewe ukasomee ufundi utusaide katika shughuli za ujasiriamali VETA ile sio tu ya kijana wa darasa la 7 hata wewe uliyemaliza Degree uwe mtaalamu wa Kompyuta nenda kajifunze kushona nguo, uwe fundi cherehani, nenda kajifunze ufundi umeme uwe fundi umeme kwahiyo hata mwanafunzi wa chuo kikuu anaweza kwenda kusoma VETA kwasababu pale unasemea ufundi"

Your browser is not able to display this video.


My Take
Broilers wote mumepewa Mchongo,hamtaki acheni.

View: https://x.com/Jambotv_/status/1900251280368439576?t=1ETPaGpqQEPSYA7o4mkSJA&s=19
 
Nimeangalia takwimu za Vijana wanaomaliza VETA na wale wa Degree

Naona takwimu zinataka kufanana Kwa kiasi

Mathalani Wahitimu wa Degree ni Wahitimu 100,000 Kwa Mwaka

Wakati wale wa VETA wastani wa 157,000 Kwa Mwaka

Kama Serikali inataka hayo, ipunguze kudahiri Wanafunzi wa Vyuo Vikuu

Na Badala yake nguvu kubwa ielekezwe huko vyuo vya Kati na Ufundi

Japo Anayehitimu Degree anakuwa na maarifa makubwa kuzidi hao wa vyuo vya Ufundi ambao ni dhahiri wanaandaliwa kuwa Mafundi
 
Dah imeniuma sana!
 
Ndio muelekeo
 
Kwa ufulu huu mpaka shule za kayumba zina one ya 7. Tarajia kipigo cha ccm
 
Dah imeniuma sana!
Yaani msomi ana digrii ya Udaktari wa Binadamu baada ya miaka mitano; kaenda intern mwaka mmoja; akimaliza aende Veta kusomea ufundi cherehani! Kwa mantiki hiyo, hakuna haja ya kwenda kusomea huo Udaktari wakati waweza kwenda Veta na kujifunza kushona nguo ndani ya mwaka mmoja. Ama kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa.
 
Why huko vyuo vya degree wasiweke na mchepuo wa VETA ili mwanafunzi asome kama optional course ambayo atapata cheti cha veta na degree yake?
 
DHARAU ZIMEANZA SASA
 
Migambo wanaruka na kukanyagana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…