#COVID19 Waziri Mkuu Majaliwa: Zoezi la chanjo ya Uviko-19 limefikia zaidi ya asilimia 80

Chanjo ya Korona ni kwa wote,hiyari yashindwa utumwa.
Bora kuchanja kwa hiyari sasa,kuliko kulazimishwa kuchanja hapo baadae.
Tusiochanjwa ni wakati wetu sasa kuchanja,hapo baadae tukilazimishwa
kuchanja kwa mawimbi mengine yajayo hayumkini tukapoteza kinga zetu kwa hofu.
 
Dah!!! Mbona taarifa kwenye database ya dunia inaonyesha tuna asilimia chini ya moja!!!
 
Wanafurahi 80& hehehe watu hawajafika hata 1m kwenye nchi ya watu 60m.🤣🤣🤣🤣
 
Kwa hiyo unabisha? Watu wanachanjwa kwa wingi mitaani. Hata wenyewe JF wameibuka na hashtag #UjanjaKuchanja.
Wameanza kudanganya tena.
JUMApili tu ilikuwa ni 40% na leo ni 80%

Tz tuwe serious.Tuache kudanganya.Tuzidi kuwahamasisha watu.Wananchi walichanganyikiwa na meseji pingana kutoka kwa viongozi.
 
Baada ya kudanganya msikitini kwamba Rais yupo bize anaendelea na majukumu yake, huwa simuamini kabisa huyu mwamba
 
Baada ya kudanganya msikitini kwamba Rais yupo bize anaendelea na majukumu yake, huwa simuamini kabisa huyu mwamba

Katiba mpya ni muhimu sana kuondosha watu kama hawa kwenye nafasi ambazo uaminifu hauwezi kuwa na mbadala.
 
Watanzania milioni zaidi ya 60 chanjo milioni moja tu mpaka kwa mbinde na kulazimishana huoni kama kuna tatizo mahala tangu ziije huu ni mwezi wa ngapi? na bado kampeni zinafanyika ili watu wajitokeze, think big
 
Mhh Mambo mengine ya kufikirika ...hivi Kuna ugumu gani was kuwadanganya the so called MAbeberu kuwa ...niongezee chanjo zile za awali zimeisha...!
Kwaninwataingia store?!
 


Na mnao wakati wa kuwasikiliza CCM na matapishi yao ??
 
Wakitaka hizo chanjo zote ziishe watangeze tu kila atakayechanjwa atapewa sahani ya wali na soda.

Watanzania wengi wanafikiri kwa kutumia tumbo kwahiyo tangazo hili litapelekea hadi watu kuchanja hata mara mbili ili wapewe wali wa bure.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…