Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye arejea CCM, alijiengua CHADEMA baada ya kuambiwa na Mbowe 'Sumu haionjwi kwa kuilamba'

Huyu mzeee angekaa tu apumzike jamani kwani anahangaika na nini? Kwa umri alionao na Kwa cheo cha uwaziri Mkuu alichokaa nacho Kwa miaka kumi alipaswa akae apumzike sasa maaana sidhani Kama kuna cheo tena anachoweza kuomba Kwa sasa maaana alishashika cheo cha mwisho Kabisa Kwa utendaji wa serikali maana hicho cha urais hawez pata wala hakimfai hafai hata kugombea

Sent using Jamii Forums mobile app


Tufikiri zaida ya marupurupu binafsi May be anamaono ya ki democrasia zaidi ,hebu tu sikilize Mhadhiri mstaafu.
 
Huyu si amesema Havard?
Havard kama chuo cha kata
 
Akiwa ndani ya ukumbi, Mzee Sumaye. amesema:

"Mimi nimekaa ndani ya CCM kwa kuanzia TANU, niliingia chama wakati ule kama TANU Youth League nikiwa sekondari, na nilipomaliza tu nikaingia kuwa mwanachama wa TANU na baadaye kuwa mmojawapo wa wanachama waanzilishi wa CCM. Nimedumu ndani ya chama kwa muda mrefu nikaingia bungeni, kabla ya bungeni nilishika nafasi nyingi za uongozi katika CCM"

Ni kwa nini aliamua kwenda upinzani sasa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Si wawe wanarudi kimyakimya tu? Huu ni utoto sasa. Huyu si alisema amepumzika siasa na hatojiunga na chama chochote cha siasa? By the time anatoa hiyo kauli bila shaka hata mkewe hakumuamini
 
Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye leo Februari 10, 2020 ametangaza kurudi Chama cha Mapinduzi (CCM) Disemba 4, 2019 alitangaza kuachana na CHADEMA huku akidai alikosea kudhani kuna demokrasia ndani ya chama hicho.

Kama Sumaye anadhani hakuna demokrasia Chadema bali kuna demokrasia CCM chini ya Magufuli na hivyo arudi huko, basi yeye ni mtu wa kuhurumiwa sana!
 
hawa wazee kwani mpaka wafie CCM ? umri huo mambo ya vyama ya nini


Sent from my iPhone using JamiiForums
Inabidi tu uwaelewe.

Lowasa alibanwa na TRA akakimbia kurudi CCM.

Masha alikwamishwa Fast Jet akakimbia kurudi CCM

Sumaye kanyang'anywa mashamba kakimbia kurudi CCM.

Yaani tuwahurumie tu hawa wazee, sio chaguo lao.
 
Back
Top Bottom