Waziri Mkuu simamia viongozi, wananchi wamechoka kuchangishwa pesa za madarasa kila mwaka

Waziri Mkuu simamia viongozi, wananchi wamechoka kuchangishwa pesa za madarasa kila mwaka

Patriot

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2008
Posts
5,759
Reaction score
4,872
Tundu Lissu alilaaniwa kwa kuzuia michango ya lazima kwa wananchi. Sasa kila mwaka kuna michango kwa ajili ya madarasa, ni ukweli kwamba michango hii ni ya lazima kwa wananchi.

Sioni taabu sana, tatizo langu ni wasimamizi wa michango hiyo na matokeo duni.

Kundi la viongozi katika wilaya wakiongozwa na wakuu wa wilaya wamegeuka ni wezi wa michango hii wanastahili kudhibitiwa. Hawa ndo wanaoharibu maana ya michango hii. Wananchi wamechoka na hata CCM mumechokwa!

Haiwezekani mwananchi achange pesa kwa lengo zuri halafu wasimamizi wawe ni viongozi wa serikali. Viongozi hawa walistahili kusimamia pesa za serikali na siyo michango ya wananchi.

Madarasa yote yaliyowahi kujengwa kwa michango hii, yana ubora duni kabisa! Hii inatokana na wizi unaofanyika na viongozi hawa wakiwa na uhakika kwamba hawatakaguliwa na CAG kama ilivyo kwa pesa za serikali.

Je, wananchi watachanga hadi lini kwa matokeo mabovu kama haya? Jengo la miaka mitatu leo limeanguka! Waziri mkuu simamia nafasi yako, wadhibiti wakuu wa wilaya ktk hili.
 
rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ni Dr. John pombe magufuli, mtetezi wa wanyonge na mchapa kazi asiyechoka au nasema uongo ndungu zangu?
 
Tanzania ni tajiri
Rais wa Jamhuri Ya Muungano wa Tanzania
Alikataza Michango Yoyote, Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais, Tamisemi Yupo Wapi? Michango Yoyote Serikali Yetu Inatoa Cash
 
Na hao wananchi hawaridhiki kabisa maana wanaowachangisha hawajawachagua kwenye box la kura. Hao viongozi wanawachangisha watu kwa shuruti maana wanajua watu hawako tayari kuchanga kwa hiari, kwani ni viongozi walioko kisheria, lakini wasio na uhalali wa umma.

Na sio kwamba waziri Mkuu hajui kuwa hizo pesa zinafujwa na hao viongozi, ila anaawaachie nao wapate kifuta jasho kama sehemu ya asante ya kusimamia wizi wa kura.
 
5 tena 5 tena
Kufanya Jambo lile lile mara zote kisha utegemee matokeo tofauti ni UPUMBAVU

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
Naamini huwalaumu wnanchi maana uongozi uliopatikana sidhani kama ni matokeo ya wananchi. Muhimu walioko madarakani wamegeuka ni wapiga dili za wazi. Saiamini kama jengo la miaka mitatu iliyopita leo hii linapukutika. Darasa moja linajengwa kwa milioni 20 kwa pesa za michango ya wananchi.

Mbaya kabisa ni mkuu wa wilaya au watendaji wake kusimamia ujenzi wakati pesa ni michango ya wananchi.
 
Tanzania Ni Tajiri
Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Alikataza Michango Yoyote, Waziri Wa Nchi Ofisi Ya Rais, Tamisemi Yupo Wapi? Michango Yoyote Serikali Yetu Inatoa Cash
rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania ni Dr. John pombe magufuli, mtetezi wa wanyonge na mchapa kazi asiyechoka au nasema uongo ndungu zangu?
Au nasema uongo ndugu zangu?
 
Yaani uchangiaji wa Madrasat sasa umegeukia Madarasa
 
Waziri mkuu Majaliwa, kama hatabadili mtindo wa utendaji na kupata taarifa, basi tusitegemee chochote au lolote. Tusiwategemee wakuu wa wilaya ktk mambo muhimu kama elimu na madarasa. Wakuu wa Wilaya walio wengi ni watu wenye tabia zilizo hovyo kabisa, kama yule aliyeshiriki kugombania mwana-dada kule Kahama. Wa aina hiyo ni wengi wilayani, tena ni bora akina mama, Wanaume ubora ni hovyo kabisa kwa tabia ya wizi.

Michango kama hii kwa sasa, wanalazimisha wanavijiji kwa nguvu. Nguvu yaweza kuwa sawa tatizo pesa itaibiwa hadi mwakani tena.
 
Vijijini ni kampeni ya kuwakamua wananchi. For sure, tatizo siyo kuchangia. Tatizo ni hao wanaochangisha. Hao wakuu wa wilaya siwaamini kabisa juu ya uaminifu wao ktk pesa. Wengi ni dropout wa kugombea nafasi za kisiasa.
 
Ninachojua michango yote ilipigwa marufuku na sasa ni elimu bure, wakitumbuliwa wanaanza kulia lia...
 
Waziri mkuu Majaliwa, kama hatabadili mtindo wa utendaji na kupata taarifa, basi tusitegemee chochote au lolote. Tusiwategemee wakuu wa wilaya ktk mambo muhimu kama elimu na madarasa. Wakuu wa Wilaya walio wengi ni watu wenye tabia zilizo hovyo kabisa, kama yule aliyeshiriki kugombania mwana-dada kule Kahama. Wa aina hiyo ni wengi wilayani, tena ni bora akina mama, Wanaume ubora ni hovyo kabisa kwa tabia ya wizi.

Michango kama hii kwa sasa, wanalazimisha wanavijiji kwa nguvu. Nguvu yaweza kuwa sawa tatizo pesa itaibiwa hadi mwakani tena.
Ukiwaangalia watu hawa na lengo la kuwepo kwao, hata haieleweki. Hawana kazi hata majukumu kwa wananchi zaidi ya kuwasweka ndani kwa masaa. Sasa hili la michango wamepata sababu ya kutafuna pesa za wananchi. Zitaliwa ile mbaya!
 
Sasa tunasikia wanatoroka na pesa za michango ya mashule. NI aibu serikali kuwaachia wananchi kukamuliwa na viongozi wa wilaya kwa kisingizio cha michango ya ujenzi wa mashule wakati wasimamizi wa michango ni wezi wakubwa.
 
Back
Top Bottom