Waziri Mkuu wa Haiti ajiuzulu baada ya Makundi ya Uhalifu kumshinikiza aachie madaraka kabla ya kurejea nchini humo

Raia wa Colombia wakavuka kuja kumuua Rais wa Hait kwa malengo yapi mkuu. Tuelimishe
Walitumwa mkuu. Kuna ambao wamefunguliwa mashtaka marekani. Na kule Haiti pia mke wa rais ambaye naye siku anauwawa alikuwepo. Ametajwa na jaji anayesimami hiyo kesi ya mauwaji. Wengine ni waziri mkuu aliyepita, pamoja na mkuu wa polisi aliyepita.

Wengine walioshiriki nao walikamatwa marekani kule Miami kama sikosei.

MKE naye alikimbizwa marekani kwa matibabu. Ila amekuwa β€œindicted” na judge, sijajuwa bado connection yake ni ipi kwenye yale mauwaji.
 
Simu ya mke wa Rais ilifuatiliwa ikagundulika almpigia mume wake ambaye ni rais muda mchache kabla ya kuuwawa

Na kumwambia kwa muda wote uliokuwepo madarakani hukutufanyia chochote

Na maneno mengine km yanayoonyesha km alimpigia simu kumuaga
 
Hv unajua kwamba Haiti haina jeshi? Sasa jiulize jeshi linalofanya kazi haiti linatoka2 wapi?
 
Ingia google andika tu iridium in haiti utajionea mwenyewe. Ukimaliza andika amount of iridium in haiti kisha angalia mzalishaji namba moja wa iridium anazalisha kiasi2 gani
 
Republic of gangsters
 
Ingia google andika tu iridium in haiti utajionea mwenyewe. Ukimaliza andika amount of iridium in haiti kisha angalia mzalishaji namba moja wa iridium anazalisha kiasi2 gani
Acha kuokoteza vipande vipande vya tetesi na kuvifanya kuwa habari. Hivi ninapoandika post hii, Haiti haina active mining industry yoyote. Research zinaonyesha kuwa ina potential ya kuwa na depostis za madini kadhaa ikiwamo iridium, lakini hakuna madini yoyote yanayochimbwa Haiti kwa wakati huu.

Taarifa kamili ya madini kutoka kwenye serikali ya Haiti ni hii hapa, haisemi kuwa wanachimba madini ya aina yoyote.

 
Huu Upumbavu wa kijinga utaisha lini. Kila watu wakipigana USA. Mara sijui wazungu gani wanausika. Mkuu Upumbavu ni WA mtu mweusi mwenyewe ifikie wakati waache ufala kabisa. Wewe mtu anatoka kwao anakugombanisha na raia mwezako unamuua wewe si fala tu.
 
Mkuu ni kwa nn Haiti ni weusi watupu?
 
Mkuu a
Simu ya mke wa Rais ilifuatiliwa ikagundulika almpigia mume wake ambaye ni rais muda mchache kabla ya kuuwawa

Na kumwambia kwa muda wote uliokuwepo madarakani hukutufanyia chochote

Na maneno mengine km yanayoonyesha km alimpigia simu kumuaga
Mkuu5alimpigiaje
 
Mkuu ni kwa nn Haiti ni weusi watupu?
Asilia yao ni watumwa wa kutoka Afrika waliopelekwa huko kulima mashamba ya Miwa na Kahawa wakati wa biashara ya utumwa ya pembetatu ndani ya Atlantic. Watumwa wale waliasi wakapindua utawala wa kiafaransa na kujitanganzia uhuru wao, na ndiyo ukawa mwanzo wa taifa hilo la haiti lililoanza mwaka 1804 takriban karne nzima kabla Afrika haijavamiwa na Berlin conference.
 
Wale waliotunga vitabu vya history walitukosea sana tena sana. Hiyo history ya Haiti ya kupata uhuru mapema ivyo ilitakiwa iwepo kwenye ivyo vitabu. nadhani haikuwekwa kwa makusudi coz mtu mweupe ndiye aliyechakazwa.
 
Sorry swali kingine, je hakukuwa na watu weupe kwenye hiyo nchi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…