Richard
JF-Expert Member
- Oct 23, 2006
- 15,692
- 23,038
Leo jioni wabunge wa chama cha wahafidhina watapiga kura ya kutokuwa na imani na kiongozi wa chama hicho na waziri mkuu bwana Boris Johnson.
Hatua hiyo yafuatia barua za wabunge wa chama hicho kwa kamati maalum iitwayo 1922 committee ambazo zilipaswa kufikia asilimia 15 yaani sawa na barua 54 ili kuweza kupiga kura ya kutokuwa na imani.
Zoezi hilo la upoigaji kura litaenda haraka na bwana Johnson ana imani kubwa kuwa atashinda kura hiyo ambapo wengi wa wabunge wa chama chake wana imani nae.
Ili kumtoa bwana Johnson idadi ya wabunge wanotaka kumtoa bwana Johnson yatakiwa ifikie kura 108 huku bwana Johnson akiwa atembea kifua mbele kwa kuwa na wabunge 116 ambao tayari ni mawaziri katika serikali yake.
Katika kipindi cha wiki mbili mfululizo kumekuwa na kauli na wito kadha wa kadha za kumtaka kiongozi huyo ajiuzulu kutokana na kashfa za kufanya tafrija katika ofisi maalum ya namba 10 katikati ya muda wa kujitenga yaani "lockdown" kati ya mwaka 2021 na 2022.
Ushahidi mbalimbali umetolewa ukionyesha bwana Johnson kushiriki kuvunja kanuni na sera za kujitenga wakati wa ugonjwa wa Covid -19 ambapo watu zaidi wa 6 hawakutakiwa kukusanyika ndani ya nyumba moja au ofisi au mazingira ya kukutana katika chumba kimoja.
Baadhi ya wabunge wanoogopa kupoteza kura katika uchaguzi mkuu ujao wamekuwa wakikutana kufanya vikao vya siri kutengeneza mazingira ya kumtoa bwana Johnson kwa kuhofia watashindwa katika uchaguzi mkuu.
Pamoja na tatizo la kashfa bwana Johnson anakabiliwa na matatizo mengine makubwa manne ambayo ni ripoti ya kashfa tafrija ndani ya ofisi ya namba 10, sera ya kuwapeleka Rwanda wakimbizi wengi wenye asili ya Afrika, suala la Brexit na kushindwa kuwa na sera madhubuti za kujikinga na matatizo ya ukali wa maisha kwa wananchi wa Uingereza.