Waziri Mkuu wa Uingereza ndiye mwenye nguvu zaidi kuzidi Mfalme/Malkia

Waziri Mkuu wa Uingereza ndiye mwenye nguvu zaidi kuzidi Mfalme/Malkia

Nguvu au utawala wa malkia auhojiwi popote, na yoyote. Hakuna kuchaguliwa au kuteuliwa na yoyote... ni urithi wa familia.
Si kweli!

Bunge la Uingereza lina uwezo wa kuhoji madaraka ya mfalme au malkia. Isitoshe, limeshawahi kufanya hivyo.

Hata huyo mfalme au malkia alichaguliwa na bunge hilohilo kupitia sheria mbalimbali zilizotungwa zamani na bunge la Uingereza.

Bunge lina uwezo wa kubadili sheria za urithi wa kiti cha ufalme, vilevile lina uwezo wa kuzuia urithishwaji wa ufalme kwa mrithi anayefuata.
 
Hahah eti siku wakijaribu... yaani wapo madarakani toka miaka ya 1600s alafu unasema wakijaribu.
Familia za kifalme pale ulaya zote ni ndugu, soma na fuatilia... wao ndio kila kitu.

Huyo waziri mkuu anapigwa chini mda na saa yoyote, aliyepita hana hata miez 2... sasa niambie nani anaweza kuhoji mamlaka ya ufalme, achilia mbali kuwatoa.
Wapo madarakani kwasababu bunge limewaruhusu kuwepo. Mara ya mwisho mfalme kujihusisha na jambo lolote la kisiasa ni zaidi ya miaka 300 iliopita huko. Sio kila kitu lazima ubishe unaweza ku google tu nini kilimkuta mfalme wa wa mwisho aliejaribu kupingana na bunge la uingereza utaelewa kwanini hawa jamaa hawataki kutumia hayo madaraka yao. Hii familia almost kila kitu wanapangiwa na bunge.
 
Back
Top Bottom