Waziri Mkuu wa Uingereza ndiye mwenye nguvu zaidi kuzidi Mfalme/Malkia

Nguvu au utawala wa malkia auhojiwi popote, na yoyote. Hakuna kuchaguliwa au kuteuliwa na yoyote... ni urithi wa familia.
Si kweli!

Bunge la Uingereza lina uwezo wa kuhoji madaraka ya mfalme au malkia. Isitoshe, limeshawahi kufanya hivyo.

Hata huyo mfalme au malkia alichaguliwa na bunge hilohilo kupitia sheria mbalimbali zilizotungwa zamani na bunge la Uingereza.

Bunge lina uwezo wa kubadili sheria za urithi wa kiti cha ufalme, vilevile lina uwezo wa kuzuia urithishwaji wa ufalme kwa mrithi anayefuata.
 
Waziri mkuu wa sasa na Muhindu
Mwislamu hawezi kuwa Waziri mkuu wa Uingereza, hata mkristo mkatoliki ni Tony Blair tu ndio alifanikiwa, vipo vya kubisha lakini siyo hili.

Dini rasmi ya UK ni Anglican.
 
Wapo madarakani kwasababu bunge limewaruhusu kuwepo. Mara ya mwisho mfalme kujihusisha na jambo lolote la kisiasa ni zaidi ya miaka 300 iliopita huko. Sio kila kitu lazima ubishe unaweza ku google tu nini kilimkuta mfalme wa wa mwisho aliejaribu kupingana na bunge la uingereza utaelewa kwanini hawa jamaa hawataki kutumia hayo madaraka yao. Hii familia almost kila kitu wanapangiwa na bunge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…