Waziri mpya wa Mawasiliano, anza kazi na Azam Media. Wamepanga kutupiga kwenye vifurushi vipya

Azam waache kuwanyonya wananchi eti kisa ni kampuni inayopendwa na wananchi ndio mnawakandamiza?

Hakuna ubishi kuwa Azam Media ndio baba lao. Sasa msitumie advantage kisa mnarusha tamthila nzuri zinazopendwa na watu kisha kuwaumiza kwenye bei za vifurushi.
 
Mbona unalazimisha watu kwa fedha wanazo tafuta wenyewe, maana kama design unawakalipia kwa kutumia hela zao watakavyo.

Huyo DSTV anaenda kupotea polepole siku hizi kuna Router hizi,kwa 100k+ unapata speed ya kitosha link kibao za kucheck EPL,UEFA na ligi zote za ulaya.
 
Tafuta pesa halafu punguza hasira azam ni ya kuangalia masikini kama wewe
 
Azam wanafanya hivyo kwa sababu hawana mpinzani.
Wenye visambuzi vya Azam WOTE akiacha kulipa kwa miezi miwili atanyooka na kushusha gharama
 
Tafuta pesa halafu punguza hasira azam ni ya kuangalia masikini kama wewe
Sasa mimi na wewe nani ana hasira,hela ya kwakwe mwache aamue Azam TV au Star times unataka kuwapangia watu cha kuangalia si upunguani huo.

Mimi nina Azam na nina Router ya Voda si hitaji DSTV na natizama mechi zote, sina njaa kama ulizokuwa nazo wewe. King'amuzi cha DSTV sijui hata kipo wapi.
 
Wewe unafikiri kuleta Camera ya milioni 500 na VIKURE(VAR) gharama yake ni kidogo? Kifurushi cha juu 35000 hakijaguswa,wamegusa vya chini tu.

Bora Azam ndiyo ya bei rahisi ,hata Startimes nayo bei kubwa tu ila baba yao ni DSTV jini hilo beio zao si rafiki.
 
Hasira unazo wewe ungekua huna hasira ungeupita huu uzi
 
Sio inapendwa bali sababu haiba mbadala ya kuonyesha ligi ya Bongo,ukija kwenye tamthiliya za kibongo na movie za majuu wameachwa mbali sana na Dstv.
 
Sio inapendwa bali sababu haiba mbadala ya kuonyesha ligi ya Bongo,ukija kwenye tamthiliya za kibongo na movie za majuu wameachwa mbali sana na Dstv.
 
Hiyo ni biashara kama biashara zingine, muuzaji anataka faida na mnunuaji anataka huduma, ikiwa utaona ni gharama kubwa bora utafute mwenye kutoa huduma mwingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…