Nimefurahi kuwa Masanja Kadogosa umeteuliwa kuongoza wizara muhimu sana kwa nchi maana aliyepita alikuwa anazungukwa tu kwa kutokuwa na utalaam wowote kwenye hiyo sekta angalau wewe unauzoefu pengine hutazungukwa kiana.
Sina mashaka na uzoefu wako kwa kuwa ulikuwa uchukuzi wizara inayofanana na wizara ya ujenzi kimajukumu.Wakala wa Barabara kiukweli toka Amafariki Engineer Patrick Mfugale umefanya nchi ikose kabisa mchora ramani.
Kwa sasa Tanroad inaenda kimungu Mungu tu.Mameja wengine wamejisahau na wengine wameshakuwa wakazi wa mikoa na mtu akishakuwa Mwenyeji kuna mambo mawili au matatu lazima yatokee Tender zenye 10% nyingi,Tender za kujuana na baya zaidi Meneja kukompromise na wakandarasi kwenye ubora na muda wa kutekeleza miradi.
Hivyo iko haja ya mtendaji mkuu kujitathimini yeye na Meneja wake maana wananchi wanajua mengi yanayotendeka.Japo muhimu pia la kuangalia ni suala la ubora wa barabara zinazojengwa maeneo mengi umeshuka mno mno.
Mwisho kabisa nikumbushe kuwa kutokana na barabara kupitishwa kwenye maeneo yenye changamoto za maji na udongo Waziri wa wakati huo aliitaka Tanroad kudesign barabara upya ili kupeleka barabara kwenye maeneo yasiyo na changamoto za kimazingira lakini hilo halipo na badala yake mameja bado wanacompromise.
Tunakutakia kila la kheri kwa kuzingatia changamoto itakayo ikumbuka nchi siku za usoni kimiundo mbinu kutokana Mvua za El Nino.Usisahau kumulika miradi ilyopo Mkoa wa Njombe pia kuna uwongo uwongo mwingi kidogo.