Wanasema Wajerumani walitaka kuwekeza Tanzania katika uzalishaji wa magari type ya VW,lakini wakazungushwa wee na taasisi ya uwekezaji nchini mpaka wakakata tamaa, wakaona hisiwe taabu ndio wakakimbilia Rwanda ambako wawekezaji wanapokelewa kwa mikono miwili bila ya urasimu wa kijinga, ndani ya mwezi mmoja kila kitu kinakamilika - Kagame na uongozi wake wako dead serious kwenye masuala haya, akisikia mwekezaji anewekewa kauzibe anawatimuwa kazi wahusika on the spot na kifungo juu.
Mtu ungetegemea walao TTCL ingechangamkia kutafuta wabia wa kuwekeza kwenye ku-assemble simu janja nchini lakini wapi, hawataki kuchakalika Wachina walisha wajengea mkonga wa mawasiliano wa Taifa wamesambaza huduma mpaka nchi jirani wanaona ya nini kuangahika zaidi - ubunifu wa kumfikia the late mzee Mengi, hilo TTCL hawana kabisa!!