Waziri Mwambe: Mazungumzo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi

Waziri Mwambe: Mazungumzo ya ujenzi wa Bandari ya Bagamoyo kuanza rasmi

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
mwambe.jpg

Waziri wa uwekezaji Mr. Mwambe amesema hakuna mkataba wowote uliosainiwa hapo awali kuhusu bandari ya Bagamoyo zaidi ya minutes tu za vikao.

Mwambe amesema serikali itaanza rasmi mazungumzo na Oman na China ikiwa na maagizo ya Rais Samia baada ya kuwa amezipitia nyaraka zote.

Chanzo: ITV habari

Pia soma
 
Usiwaamini hawa watu.

Sawa amezipitia, swali ni je, ana utaalamu wa mikataba na maswali mengine ya kitaalamu?

Kama ambavyo Mbowe sio gaidi, na sisi wananchi sio wajinga.
Kipindi fulani kwenye issue za negosition kama hizo unakuta timu kama wakina Dr. Chamuriho ambae aliongoza timu ya negosition mradi wa SGR, Ununuzi wa ndege pamoja Bwawa la Mwalimu Nyerere ila kwasasa anaonekana hafanyi kazi vizuri chini ya Rais Samia, pembeni ungemkuta Marehemu Mfugale, wingi ya kulia ungemkuta Engineer Kakoko then unakuta watu wa Tanroads, watu sheria, etc na hao wote walikuwepo kwenye ile team ya mwendazaje iliyosema kwa masharti haya hapana kama vipi ya kwetu ni haya hamtaki rudini mkajipange tena.

Lakini safari hii tarajia kukutana na wanasiasa na wanadiplomasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kipindi fulani kwenye issue za negosition kama hizo unakuta timu kama wakina Dr. Chamuriho ambae aliongoza timu ya negosition mradi wa SGR, Ununuzi wa ndege pamoja Bwawa la Mwalimu Nyerere ila kwasasa anaonekana hafanyi kazi vizuri chini ya Rais Samia...
Who is Dr. Chamuriho....unaambiwa mkataba haukuwepo unaleta undezi hapa simama katika HOJA.
 
Tujipe muda, hatuna sababu za uharaka mradi huo.
 
Usiwaamini hawa watu.

Sawa amezipitia, swali ni je, ana utaalamu wa mikataba na maswali mengine ya kitaalamu?

Kama ambavyo Mbowe sio gaidi, na sisi wananchi sio wajinga.
Umeambiwa hakuna mkataba ni minutes za vikao tu!
 
Kusikia Kwa Kenge Hadi Atoke Damu Puani Na Masikioni

Mabeberu Ya China Yanakuja Kujichotea Vyote Mkataba Wa Miaka 1000 Oops

Yale Ya Loliondo Waarabu Wamechukua Nchi Viongozi Wakiona Na Hawana La Kusema
 
LNG na bandari ya Bagamoyo, huku bado kuna SGR, Nyerere dam, Kigongo Busisi yote miradi mikubwa ya gharama kubwa na bado haijamilika, hii haraka ya nini kama sio nao wanataka 10% zao?
 
Nafarijika sana naposikia maamuzi yenye tija kama haya yanafanyika. Bandari ya Bagamoyo ni mkombozi kwa ajira za vijana wetu wanaomaliza ngazi mbalimbali za elimu
 
Waziri wa uwekezaji Mr Mwambe amesema hakuna mkataba wowote uliosainiwa hapo awali kuhusu bandari ya Bagamoyo zaidi ya minutes tu za vikao.

Mwambe amesema serikali itaanza rasmi mazungumzo na Oman na China ikiwa na maagizo ya Rais Samia baada ya kuwa amezipitia nyaraka zote.

Source: ITV habari
Hapa Kiwete alizindua ujenzi wa bandari ya bagamoyo bila kusaini mkataba wowote?
 
Kipindi fulani kwenye issue za negosition kama hizo unakuta timu kama wakina Dr. Chamuriho ambae aliongoza timu ya negosition mradi wa SGR, Ununuzi wa ndege pamoja...
Mwita Gachuma lazima awemo!
 
Waziri wa uwekezaji Mr Mwambe amesema hakuna mkataba wowote uliosainiwa hapo awali kuhusu bandari ya Bagamoyo zaidi ya minutes tu za vikao.

Mwambe amesema serikali itaanza rasmi mazungumzo na Oman na China ikiwa na maagizo ya Rais Samia baada ya kuwa amezipitia nyaraka zote.

Source: ITV habari
Mnhhh.....

Kifo cha Magufuli kinaanza kufikirisha sasa.

Lohh!!
 
Tatizo la Watanzania ujuaji wa kila kitu hata kwa kile hatuna ufahamu nacho umetujaa. Sikushangaa awamu ya tano kuingia mikataba kimyakimya iliogopa ujuaji wa namna hii. Tuache Tanzania ya kisasa ijengwe walau tutaweza kupata japo hata kakibarua ili familia iweze kuishi
 
Back
Top Bottom